Tuesday, 26 July 2016

JINA LA CHRISTIANO RONALDO KUTAWALA VITU VYA MJI WAKE WA NYUMBANI.


Uwanja wa ndege wa mji wa nyumbani kwa mwanasoka bora mara tatu wa dunia kupewa jina lake ili kuuenzi mchango wake katika soka la nchi hio.


Kwa sasa linakua ni swala tu la muda kuamua ni lini hasa uwanja wa ndege wa Madeira utapewa jina la Christiano Ronaldo. Inaonekana vitu vingi katika mji wa Madeira vinapewa jina la Cr7. Raisi wa eneo hilo Miguel Albuquerque alitangaza kua wataubadili jina uwanja wa mkubwa wa kisiwa cha Madeira kua "Madeira christiano Ronaldo Airport" kiriropoti chanzo cha habari cha Mundo Deportivo/(mirror).

Hii inakuja baada ya Christiano Ronaldo kuisaidia Ureno kutwaa taji kubwa la michuano ya ulaya (Euro 2016) mapema mwezi huu. Kumbuka katika mji huu tayari kuna sanamu kubwa ya Christoano Ronaldo.

No comments:

Post a Comment