KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.
Kwanza nipende kuwapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo naona swala la teknolojia ya habari na mawasiliano limeweza kua ni chachu ya mabadiliko hapa nchini. Na kama tutaendelea kua na weledi wa matumuzi bora ya maendeleo haya ya sayansi na teknolojia basi, naamini tutafika mbali. **
Katikati mwa wiki hii ya pili ya mwezi Oktoba kuna jambo "Kubwa" lililoibuka na kushika vichwa vya habari, post, comments na shares katika mitandao ya kijamii ikionesha jinsi "Walimu akimuadhibu mwanafunzi" kwa kile kinachoonekana kama ni adhabu isiyostahili au ni shambulizi dhidi ya mwanafunzi. Hili jambo hata mimi limenigusa kwa namna tofauti tofauti.
Kwanza, nimefurahishwa na jinsi ambavyo serikali imelichukulia jambo hili. Maana mara baada video hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii niliona kauli kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi akiagiza vyombo vya usalama kuhakisha wahusika wahusika katika kadhia hiyo wakikamatwa. Nikashuhudia waziri wa elimu, sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi pia akiwafuta chuo "walimu" waliohusika na hilo sakata, lakini pia nilikuta bodi ya mikopo ikisitisha utoaji wa mikopo kwaajili ya ufadhili wa masomo ya hao wanafunzi katika vyuo vyao. Nimefurahia kuona kwamba serikali iko makini na haitaki mchezo mchezo mchezo.
Katika kufurahi kwangu nilipatwa na mshituko na mkanganyiko pia. Nilishtushwa na maamuzi ya papo kwa papo kwa kutoa maamuzi kulingana na video ilotumwa na kusambazwa na wala sio kwa kufuata mzizi wa tukio zima. Binafsi kwa ile video nmeshuhudia mwanafunzi akiadhibiwa vikali lakini sijui kosa lake halisi ni lipi kwani vyanzo mbalimbali vinatoa sababu tofauti tofaut za nini kilisababisha mwanafunzi yule kupewa adhabu kali ambayo hata mimi haikunipendeza. Lakini ni kweli kutofanya kazi aliyoitoa mwalimu mwanafunzi yule angeadhibiwa vile? Kwanini yeye peke yake aliyeadhibiwa ofisini?? Nadhani kabla ya maamuzi yoyote kutolewa walotoa mamuzi walipaswa kuja kutueleza kua walifanya jitihada za dhati kabisa kujiridhisha na chanzo cha adhabu ile na kweli kuonekana watuhumiwa wana hatia ndipo adhabu itolewe. Kwa maoni yangu hapa hawa vijana 'wamesomewa hukumu ya kesi kabla ya kesi kusikilizwa.' Maamuzi kama haya ni sumu kwa ustawi wa haki za binadamu. Kuhukumiwa bila kusomewa kesi naona ni mchezo unaochezwa na waasiopenda michezo! Siungi mkono adhabu alopewa huyu mwanafunzi lakini pia siungi mkono maamuzi yaliyofanywa na serikali kwani imekurupuka.
Waziri wa elimu ina maana haamini wala kuheshimu mamlala za vyuo? Kama anaamini angewaagiza wale kuona ni kwa namna gani wale wahusika wanaweza kushughulikiwa. Na sio yeye kusimama na kuwafuta vyuo moja kwa moja tena sijui nae alifanya wapi upelelezi kujua hatia ya wale watuhumiwa.
Kama sio maisha ya woga ni nini? Tangu lini bodi ya mikopo inatoa orodha ya kuwafutia mikopo wanafunzi kama hivi??? Aah huu ni woga tu.
Tukio limekua overrated na kila kona tukio zima linatazamwa kwa upande mmoja tu mpaka najiuliza kama akili zetu zinafanana au? Hakuna mtu mwenye akili ya tofauti ambaye anaweza kujipindua kufikiri nyuma ya pazia. Hatutaki kuchimba ukweli bali tumeng'ang'ania kukurupuka na kuhemka. Judgements zetu ni za kinafiki na kijinga kwa kua hatuko tayari kuumiza kichwa kuijua kweli. Tunatumia mawazo mgando kujenga hoja. Nani anajua hasa kile ambacho hakikurekodiwa?? Uchwara tu umetujaa vichwani.
SERIKALI SIKIVU ILA SIO MAKINI.
Kwa namna ambavyo serikali imelishughulikia hili swala kuna mambo mengi tu ambayo imefeli.
Serikali imefanya maamuzi ikiwa imechanganyikiwa haswaaa! Kwa sababu hakuna utafiti wa kina juu ya kisa hiki cha kutisha na kusikitisha. Mpaka sasa sijaona serikaki imejifunza nini na imegundua nini kutokana na hili swala. Kama kweli maamuzi yao yana msingi basi tungeona hata kwa mbaali kuna maelekezo juu ya uhusiano kati ya walimu na wanafunzi.
Swali la msingi la kujiuliza ni funzo gani serikali imetoka nalo kuhusu jambo hili?
Kuna ushabiki wa maamizi yalotolewa kila mtu kawa fundi wa kumlaumu "mwalimu", hatukatai kua walikosea ila mbona hakuna anayethubutu kuonesha upande nwingine wa shilingi kuona ni kwa vipi hali ya mmonyoko wa maadili kwa wanafunzi imefikia kiwango gani. Hivi kwa akili ya kawaida unadhani ni mwanafunzi mmoja pekee ambaye hakufanya zoezi? Ni kutofanya zoezi pekee ingepelekea kupigwa na "walimu" watatu? Vitu vingine tujiongeze wenyewe sio kusukumwa na kauli za watu flani flani. Yaani ikitokea mtu kala samaki sio habari ila ikitokea samaki kamla mtu basi hio ndio habari. Hivi ni lini tutakua huru na kufikiri kwa vichwa vyetu badala ya kufikirishwa? Ifikie hatua tuwe wakweli; tuwe wahalisia kuliko kua chanya tu au hasi tu. Tukubali changamoto na fikra mpya.
Hivi unadhani walimu wakiamua kua kuanzia sasa hatutatumia adhabu yoyote ile kwa mwanafunzi kesho na keshokutwa mtakua na jamii adilifu? Au watu tunaongea vitu kwa mizuka?
Nilitegemea jamii yetu iwe ni daraja lakini cha ajabu jamii imekua ni ukuta. Walimu wanapigwa, wanaonewa,wanadhalilishwa ila hili kwa jamii yetu sio tatizo hata kidogo.
Licha ya kazi ngumu na kubwa ambayo walimu mnaifanya, licha ya mzigo mkubwa mnaobebeshwa kupewa "vilaza" muwabadilishe kua "vipanga" lakini bado hakuna anaejali kama mna mzigo. Ila kitu kikubwa ni kua bado mmeendelea kujitoa kwa ajili ya hao ambao hawawathamini. Hongera walimu wa Tanzania. Naamini pepo na jehanamu havijatosheka...yafanye unayopaswa na yaache yaaiyokupasa. Maana mchezo huu ni sawa na mchezo pendwa wa soka refa anapotoa maamuzi mabaya shida kubwa iko kwa mashabiki inayobaki inakua kwa wachezaji. Mtoto akirudi toka shule na tabia mbaya sijui kaziokota wapi utaskia "hivi siku hizi walimu wenu sijui wanawafundisha nini?", mtoto akirudi kafeli mtihani bado lawama kwa mwalimu kumbe muda wenzake wanasoma darasani yeye alikua anasoma mfuko wa kiroba una alcohol ngapi? Hii inaitwa MTAJIBEBA.
WITO
Kwa jinsi ambavyo nafahamu malezi ya kiafrika yalivyo hatuwezi kufuta adhabu japo sisemi adhabu itolewe kwa mazingira kama haya HAPANA. Namaanisha tuwe na adhabu zenye staha lakini pia nitoe ONYO kwa jamii kutokukurupuka kuwahukumu walimu wote kwa skendo hii. Na wakitaka kuhukumu basi wajiulize kama walishawaadhibu watoto wao kwa fimbo/makofi. Kama jibu ni NDIO jiulize kwanini ulitumia fimbo au makofi na kama ni HAPANA kuna mawili. Mosi, yawezekana hukai sana na mwanao na pili, basi hongera mwanao anafuata kila unachokitaka na au unamdekeza kwenye misingi ya maadili yasiyofaa kwa kutaka kuonekana mwanao haadhibiwi(adhabu sio viboko pekee).
Mwal Erick
No comments:
Post a Comment