TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?
TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?
![]() |
| Rais wa Marekani Donald Trump akiongea jambo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin baada ya mkutano wao huko Alaska 15 Agosti 2025/ picha kwa hisani ya Ikulu ya Marekani |
Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin ni miongoni mwa majina makubwa katika medani ya siasa za kimataifa kutokana na hulka yao na namna wanavyochukua maamuzi magumu katika nyakati ngumu. Na hivyo kufanya dunia kua na viongozi shupavu kama wanne hivi kwa maana ya nyongeza ya Xi Jin Ping wa China pamoja na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini. Ila kwa sasa ni Trump dhidi ya Putin wakikaa wawili nani mbabe wa mwenzake?
Trump anasifika kua ni mtu wa kuongea sana kwa njia ya vitisho ili kumlazimisha mpinzani wake kukubaliana nae na ni mtu asiyeweza kutabirika mara moja. Kwa hio maamuzi yake ni ngumu kubashiri. Lakini kwa Putin yeye ni mtu asiyependa kuongea sana kwa wapinzani ila hutumia njia za siri kupoteza wapinzani wake. Kwa hio Putin huogopwa sana kwani huwezi kujua anawaza nini kwa wakati gani. Sasa wakikutana hali hua ikoje?
Trump mara kadhaa amekiri kua Putin ni mtu "smart" na katika maelezo yake mengi alikua akikubaliana na Putin katika kuendesha siasa za dunia. Tayari unaona Trump kwa wakati mmoja au mwingine alimtazama Putin kama "role model" wake. Ikumbukwe Putin ni kiongozi wa zamani wa shirika la kijasusi la iliyokua umoja wa kisovieti lililojulikana kama KGB. Kwa hio hufanya mambo kwa tahadhari kubwa sana.
MKUTANO WA TRUMP NA PUTIN HELSINKI 2018.
Januari 6 2018, viongozi hao wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani walikutana Helsink huko Finland kwa takribani saa 2 japo walipanga kukutana kwa dakika 90 pekee. Wakati huo ilikua ni katika muhula wa kwanza wa Rais Donald Trump. Mengi yalisemwa kuhusu vita vya Syria ambapo ilikua ni moja ya sababu ya mgogoro mkubwa kati ya Washington na Moscow.
Maswali ya waandishi wa habari na muitikio wa makundi tofauti tofauti baada ya mkutano huo yanatoa taswira fupi ya nani alikua mbabe wa mwenzake. Mwandishi wa habari wa Associated Press (AP) alitaka kujua kana Trump anakubaliana na Putin kwamba Urusi haikuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016 ambapo Trump alishinda. Katika jibu lake alisema Putin alikua amesmhakikishia kikamilifu kwamba Urusi haikuhusika na hivyo Trump alisema anamwamini Putin na anaviamini vyombo vya usalama wa taifa vya Marekani na akasema Putin alitoa ofa ya wataalam wa Washington na Moscow kufanya kazi pamoja. Iwe ni timu ya watu 12. Kwa jibu hilo watu Marekani waliona ni kama Trump amawekwa "mfukoni" na Putin kwani alishindwa kukemea waziwazi kwamba kitendo kilichofanyika hakikupaswa kurudiwa tena na Urusi. Ikumbukwe Trump aliona FBI kuna namna walifeli kwa hio alilaumu zaidi FBI kuliko Putin na Urusi.
Mwandishi mwingine wa Reuters alitaka kujua kama Putin alipendelea Donald Trump kushinda dhidi ya Hillary Clinton na Putin alijibu 'Ndio nilipenda'. Aliongeza kia kwa sababu Trump aliahidi kurejesha Uhusiano wa Marekani na Urusi katika hli nzuri. Na baaadae waandishi waliendelea kuuliza iwapo Urusi walikua na Kompromat (ni neno la lugha ya Kirusi yenye maana isiyo rasmi kua ni kitu au taarifa chochote au yoyote ambacho mtu anakishikilia chenye siri za mtu mwingine kwamba akifanya tofauti na makubaliano taarifa hizo huvujishwa) ila Rais Putin alicheka na kusema Hapana, hawana. Na Trump akaongeza kua kama kitu au taarifa kama hiyo ingekuepo kweli basi kingelikua au ingelikua imetolewa zamani sana. Kwa hio unaweza kuona Putin alipata ushindi kiaiana dhidi ya Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump kushoto na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kulia, Helsinki 2018
MKUTANO WA TRUMP NA PUTIN WA ALASKA 2025
Ilikua ni mara ya kwanza kwa Rais Putin kukanyaga katika ardhi ya Marekani kwa kipindi cha miaka 10. Lakini tuangazie kwanza uhusiano wa Trump na Putin kati ya July 2024 hadi siku ya mkutano.
Wakati wa kampeni za Urais wa Marekani Rais Donald Trump kwa wakati huo akiwa mgombea alijigamba naa kujinasibu kua anaweza kumshawishi Putin na kumaliza vita vya Ukraine ndani ya saa 24. Amerejelea mara kadhaa kauli hio. Kulikua na simu kadhaa ambazo waliwasiliana kipindi ambacho hakua rais wa Marekani lakini haijafahamika mara moja nini walizungumza.
Mara baada ya kuapishwa alitaka kua Rais wa kuleta amani kwa kutatua mizozo mikubwa mashariki ya Kati na ule wa Ukraine. Lakini sasa huku alikutana na Putin tena. Kulikua na mikutano kadhaa iliwemo ule wa mwezi Februari huko Riyadh, Saudi Arabia. Baada ya mkutano Trump akageuka mbogo kwa Rais wa Ukraine Volodmyr Zelenisky kua ndio chanzo cha vita. Hii ni kauli ya Putin na ni tofauti na kauli za viongozi wakuu wa mataifa makuu duniani ambayo yameinyooshea kidole Urusi. Hapa inaonesha tena Putin's anacheza na akili za Trump.
Lakini tangu hapo kumekua na simu na majaribio ya mara kadhaa kumaliza vita huko Ukraine ila Trump hajawahi kupata kile ambacho alitarajia kutoka kwa Putin. Na taratibu akaanza kuelewa kwamba ni Putin alikua akimchezea akili na walaa hakuaa anatilia maana yale ambayo wawili hao walikua wakijadiki. Na hivi karibuni amekua akibadili gia na amekiri waziwazi kua amepoteza uvumilivu wake kwa rais Putin na kwamba kwa sasa kama Putin hatomaliza "vita vyake" huko Ukraine basi atakutana na adhabu kali mno. Na jibu la Putin hua ni kukaa kimya. Awali alitoa siku 50 kwa Putin kumaliza vita na baadaye alipokua Scotland akapunguza mpka siku 10-12 na ikiwa hakuna ukomo wa vita basi Urusi ingekumbwa na dkhahma kubwa ya vikwazo vya kiuchumi, vikali na vikubwa zaidi kuwahi kushuhidiwa. Lakini hilo bado hatujaliona likitokea kwani wamekutana ijumaa ya Agosti 15 2025. Na ilikua hivi katika mkitano huo;
ALASKA 2025
15 August 2015, dunia ilielekeza macho na masikio katika Jimbo la Alaska ambalo kimsingi lilinunuliwa kutoka Urusi mwaka 1867 na Putin anakanyaga kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Marekani tangu 2015. Sasa mengi mno yalitokea ambayo yanaonengea kuliko kama yangeelezewa. Nitayasema machache.
Rais wa Urusi Putin alikua wa kwanza kutua katika kambi ya kijeshi ya Elmendorf-Richardson huko Anchorage, Alasaka majira ya saa 11:05 asubuhi na muda mfupi Trump alishuka katika Airforce One kuungana na Putin majira ya saa 11:08 asubuhi. Kumbuka hua ni kawaida ya Putin kuchelewa lakinj safari hii aliwahi. Na kisha kuliandaliwa Red carpet kati ya viongozi hao. Ila kuna jambo lilitokea; ndege hatari ya B-2 Sprit ikiambatana na F-22 Raptor ama F35 ziliruja juu ya vichwa vya marais hao na katika picha mjongeo zinamuonesha Putin akiwa kama kahamaki kidogo kabla ya Trump kumsihi waondoke. Hii ilikua ni onyo la wazi kwa Putin na ukumbusho kwamba alikua hana udhibiti wa kinachotokea pale.
Ila sasa la pili la kushangaza ni kwamba Rais Putin anatafutwa kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ana ametengwa na mataifa yote makubwa ila kitendo cha kuwekewa Red Carpet ilikua ni ushindi mkubwa kwa Putin na amefanyiwa na taifa kubwa la Marekani maana yake wengine wote kutomchukulia kama kiongozi mkuu wa nchi ni upuuzi.
Baada ya mkutano kuna mengi hatujui lakini walipanga kua na chakula cha pamoja lakini hilo halikutokea kutokana na pengine kutokufikia makubaliano muhimu. Kumbuka Trump alisema kama Putin hatokubali mpango wa amani basi asingekaa, angekwea Airforce One na asingezungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano. Lakini tunaona wote walisimama kwenye podium zao na wakaongea kwa uchache sana. Na mwisho Putin alitumia kingereza kumkaribisha Trump, Moscow. Trump alisema hilo angelifikiria labda. Na ni kwamba tofauti na msimamo wa awali wa Trump na washirika wake wa kusitisha mapigano ili kujadili mpango wa amani ameenda na kitu cha Putin kwamba itafutwe suluhu ya amani ya kumaliza vita sio kusitisha vita. Hili limewaumiza sana viongozi wa Ulaya na Volodymr Zelenisky mwenyewe waliokua wanahitaji kusitisha vita. Kumbuka vita ikisimama tu inasemekana wanajeshi wa Uingereza wanaingia Ukraine na ikiwa Urusi itaanza vita tena itakua ngumu kwao kwani tayari vikosi vingi vya Ulaya vitakua Ukraine.
Sasa unaweza kutazama kwamba licha ya kua Putin sio muongeaji ila ni dhahiri anapata anachokitaka kwa wakati. Kisiasa Putin yuko mbele ya muda ila Kijeshi na Kiuchumi, Trump yuko mbele ya muda. Lakini jambo moja liko wazi Putin sio muoga wa vitisho na anajua unafiki wa mataifa ya Ulaya na Marekani. Na ameshampatia Donald Trump kwamba ameshikwa na kiburi cha kuonekana yeye ni mpatanishi wa dunia na kwamba yuko tayari kufanya chochote ili vita Ukraine viishe na achukue hizo sifa za upatanishi. Hiki kitu kinamuweka Trump katika shimo ambalo Putin ndio mwenye ngazi ya kutokea na Putin anataka wote wapate kupitia swala hilo hilo. Lakini msimaamo huu unaleta wasiwasi nchini Ukraine na barani Ulaya.
Hata hivyo ikiwa Trump na Putin watafanya kazi kwa pamoja katika kupunguza tofauti zao za kisiasa basi kunaweza kua na kipindi kirefu cha amani Ulaya na duniani. Swala la kujipanua kwa NATO, Wazo la Ukraine kujiunga NATO na Umoja wa Ulaya (EU) na vikwazo vya kiuchumi vinakua ni vikwazo vya wazi kwanini Marekani, Ulaya na Urusi wako mbalimbali sana. Na Umoja wa Ulaya kwa sasa umegundua kwamba haujiwezi bila Marekani. Wanataka baadaye ya Ukraine pia Marekani ahusike kuilinda. Putin anawatisha mno.
Leo Jumatatu Agosti 18,2025 viongozi wa nchi za Ulaya waliounda ushirika usio rasmi wa "Muungano wa Waliotayari" kwa tafsri isiyo rasmi ikiwemo Sir Keir Starmer waziri mkuu wa Uingereza, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Umoja wa Ulaya bi. Ursula Von Leyen wataungana na rais wa Ukraine Volodymr Zelenisky kuelekea Washington ambapo watakutana na Donald Trump wa Marekani ili kujadili mpango wa amani uliokwisha kujadiliwa kati ya Trump na Putin siku ya ijumaa.
Unadhani Putin na Trump wanaweza kufanya kazi pamoja kuleta amani duniani? Tuandikie hapo chini:
Imeandikwa na;
Erick Jerry
karlrck@gmail.com


.jpg)

Comments
Post a Comment