Wednesday, 6 July 2016

UNAJUA KUFANYA HAYA UKIWA NA SMARTPHONE YAKO? FANYA VINGI NA VIKUBWA UKIWA NA SMARTPHONE.

Unatumiaje "Simu janja" yako? Inawezekana ni mtumiaji mzuri wa smartphone lakini kuna "features" kwenye simu yako hukuwahi kujua kama zipo na labda pengine hufahamu kama simu yako inaweza kufanya jambo flani.

Kila mtu anajua jinsi ya
kutumia smartphone japo wengi wetu tumeanza kutumia smartphone bila kusoma "User Manual" na hivo kushindwa kuitumia simu hadi kiwango chake cha juu cha matumizi. Hivi ni baadhi ya ambavyo wengi hawajui jinsi ya kutumia.

1. UNA UWEZO WA KUPIGA PICHA 10 KWA SEKUNDE.ULISHAWAHI KUFANYA HIVI??  Ndio picha 10 ndan ya sekunde moja! Iko hivi kama wewe unatumia android fanya hivi;
Fungua camera yako > bonyeza kitufe cha "settings" kisha weka "Burst shot ON"(unaweza kutumia pia button ya kuongeza na kupunguza sauti)>> kisha kandamiza(gusa bila kuachia) "Shutter button" hadi utakapoona inatosha au hadi simu itakapofika idadi ya mwishi ya kuchukua izo "continuous pics". Nadhani umeelewa sasa unaweza kuchukua picha 100 nda ya sekunde 30 tu!! Jaribu sasa!!

2. UMECHOKA KUSOMA VITU VILIVYOPO KWENYE SIMU??

Usihofu fanya hivi....
Washa simu yako nenda kwenye "settings" kisha>> Accessibility na bonyeza "TalkBack". Kama hicho kitu hakipo kwenye simu yako nenda kakipakue Play store. Baada ya hapo rudisha simu yako kwenye home screen na simu itasoma chochote utakachokibonyeza pamoja na taarifa zinazoingia. Ili kuweza "Ku swipe" simu yako tumia vidole viwili badala ya kimoja.
Kama hupendi jinsi simu inavyoongea unaweza kubadili sautu na speed kwa kwenda kwenye "Settings" >>>Accessibility >>>text-to-speed options na badili sauti na speed. Na kisha nenda kwenye "Settings" na uweke "Hands-free mode" ili simu iweze kutambua anaekupigia na kukutumia ujumbe.

3. KU BLOCK TEXT NA SIMU YA MTU AMBAE HUTAKI AKUPIGIE AU AKUTUMIE UJUMBE.

Nenda kwenye "Settings" >>>Call settings >>>chagua Incoming calls na bonyeza call block list >>>create. Apo utaingiza namba ya mtu unaetaka asikupate, kama huna kichwani bonyeza kwenye alama ya picha unayoiona kwenye screen yako kisha itakupeleka kwenye phone book au call history na uko utachagua namba ya muhusika.
Ila unaweza kumtoa mtu kwenye kifungo hiki.

Nadhani umeongeza maarifa juu ya kutumia smartphone yako na kama unakitu hukielewi unaweza kuacha comment yako hapo chini au kwenye ukurasa wa facebook. Tukutane wakati mwingine bye byee!!!

No comments:

Post a Comment