Zaidi ya wanawake waislamu 10,000 wameomba watafutiwe waume watakaowaoa.
Wanawake hao wameomba shirika moja la kiislamu Hizba linahudumu katika eneo la Kano lililoko kaskazini mwa Nigeria kuwaunganisha na kugharamia ndoa ya halaiki.
Kamati maalum ya Hizba ndiyo iliyopewa jukumu hilo la kuwaondolea upweke maelfu ya wanawake waislamu.
Madhumuni ya kamati hiyo ya Hizba ni kupunguza idadi ya wanawake waislamu ambao hawajaolewa.
Hizba huwakutanisha wanawake na wanaume waislamu kwa lengo la kuwaoza kama watakubaliana kwa misingi ya dini ya kiislamu.
Wanawake wengi walimueleza muandishi wetu mjini Kano kuwa wamekuwa wakitafuta waume wazuri wa kuwaoa lakini hawajabahatika.
No comments:
Post a Comment