Wakati flani maisha yanaweza kwenda kombo lakini tunaweza kucheka tu. Hii hapa ni Top 10 ya wachekeshaji maarufu zaidi Afrika.
10. HELLEN PAUL BASIMIL.
Mwanadada huyu kutoka Nigeria anafanya vizuri saana kwenye uchekeshaji lakini pia ni mwimbaji na mwigizaji.
9. TUMI MORCKE
Huyu ni mwanadada kutoka Afrika ya kusini ambaye amepata umaarufu sana Afrika kutokana na kazi zake. Ameshiriki kwenye matamasha makubwa ya uchekeshaji kama vile Heavyweight comedy jam.
8.CARL JOSHUA NCUBE.
Jamaa ni mchekeshaji kutoka pande za Zimbabwe kule. Anafanya uchekeshaji lakini pia ni mtangazaji wa SFM radio.
7. DALISO CHAPONDA
Ni mchekeshaji maarufu sana kutoka Malawi. Jamaa ana kipaji kikubwa cha kuchekesha na kuandika stori za kubuni.
6. DANIEL NDAMBUKI "CHURCHILL"
Huyu ni mchekeshaji kutoka Kenya na ndie host wa kipindi pendwa cha comedy Afrika mahariki cha "Churchill Show" kinachorushwa wa NTV. Kipindi hiki kina watazamaji zaidi ya 11milion.
5. MICHAEL BLACKSON
Huyu mtaalamu anatokea pande za Ghana. Ana kipaji kikubwa cha kuchekesha na kiukweli anakitendea haki kipaji chake.
4.EDDIE KOEL
Alizaliwa katika jiji la Kinshasa lakini alilelewa huko uingereza. Mtaalamu huyu anajua kuchekesha lakini pia ni MC maarufu na ni mtangazaji wa radio.
3. ANNE KANSIIME.
Nani hajawahi kuangalia kipande hata kimoja cha Tunsiime? Anaitwa malkia wa vichekesho vya Afrika. Ni mwanadada maarufu sana. Ana wafuasi zaidi ya 100,000 kwenye channel yake ya you tube na channel hiyo imetazamwa na watu zaidi ya 15Milion.
Ameshinda tuzo kama vile African entertainment award for comedian(2015), The Rising star comedian of the year award (2015), YouTube silver play na African Oscars award for favorite comedian (2015)
2. BRIGHT OKPOCHA.
Huyu jamaa anatokea jimbo la Abia kule Nigeria. Ukiskia watu wanajua kuchekesha basi huyu jamaa pia anajua. Alikua ni mwafrika wa kwanza ku host kipindi cha Apollo mjini London, Uingereza.
1. TREVOR NOAH
Jamaa ndio kiboko ya wachekeshaji wote Afrika. Anatokea Afrika Ya Kusini. Amewahi kushinda tuzo za BBC za mchekeshaji bora wa Afrika mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment