Monday, 4 July 2016

MAUDHUI YA JUMLA YA KITABU CHA REPUBLIC [PLATO]

WAKATI FLANI NI VEMA TUJIHUKUMU WENYEWE NA BAADA YA HUKUMU TUJIADHIBU KWANZA KABLA HATUJAADHIBIWA. KATIKA MAISHA KUKOSEA KUPO LAKINI NAFAS YA KUJISAHIHISHA PIA IPO PALE PALE.  UONGOZI NI MAISHA YA MAKOSA LAKIN LAZMA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA YETU. HUWEZI KUA BORA PASIPO KUKOSEA. 

#REPUBLIC ni moja kati ya vitabu maaruf saana duniani. Kiliandikwa na Mwanafalsafa nguli #PLATO yapata takriban karne 4K.K (Kabla ya Kristo). Kitabu kimeshehen mazingumzo ya wanafalsafa nguli akiwemo #Socrates ambae pia ni mwalim wa #Plato. Kitabu hiki kinaeleza maana ya HAKI, utawala wa hak na hak ya mtu. watu weng wakiongozwa na Socrates waltoa maana ya hak kua n kutoa kile unachodaiwa,
wengne wakasema hak n kulipa wema au jema kwa rafk na kulipa baya kwa adui. Maana iz znatafsir hak kama kumpa mtu anachostahl,kiwe kzur au kbaya. Ila Socrates na Plato wakasema haki ni kutimiza kile ambacho mtu unapaswa kukitimiza na kuupa mji kile unachostahili. Chanzo cha hak n makubaliano ya kijamii na uoga wa watu na n tendo lisilo la hiar alifanyalo mtu kwa hofu ya kupata adhab!
Taifa la hak hujengwa na wat wene hak. Ili mtu awe na haki Socrates alisema inawapasa wazaz au walez kuwafundisha watoto mambo mema makuu (Nguzo kuu za utu wema) manne yan HEKIMA/BUSARA, HAKI, KUJIAMINI, na UVUMILIVU. Na pia ili kuondoa udhaifu wa mwili watoto wafundishwe gymnastic education ( Elimu ya viungo/ mazoezi).

 Kwanini Socrates alisisitiza yale mambo makuu manne?? Hekima/ Busara utazipata kwa walezi-watawala, kujiamini kutoka kwa walezi-walinzi(jeshi n.k), Uvumilivu kutoka kwa matabaka yote katika jamii yaan watawala na wataliwa na Haki kutoka kwa "serikali" ambapo kila sehem ya kitu kamili inawajibika kwa katika ñafas yake pekee. Mfano km n Bunge, Mahakama, Serikali basi kila kile kifanye kazi yake bila kuingiliwa hapo ndipo Haki itakuepo, vingnevyo HAKUNA HAKI. Angalia nchin kwako kupoje, km kuna mwingiliano jua hakuna haki. Lakin Socrates alikuja kutafsir "katiba" ya mji na ile ya akili/ubongo... Na hapa ndipo seem niliyotaka kuieleza hasaa....hio itakua n sehemu ya pili ambayo itakujia kesho. Na hapo utajitathimin wewe na viongoz wako, jijue na wajue viongozi wetu na wapi wanatosha katika mfumo upi wa utawala. Usifikirie kukosa post ya kesho

@Ricson_Jr Big Oppa ©2016.

No comments:

Post a Comment