Monday, 18 July 2016

MWALIMU MKUU SEHEMU YA TATU(..3)

MWALIMU MKUU/ HEADMASTER 

SEHEMU YA TATU

Baadae nilimskia mwalimu mkuu kua anataka kupumzika...kila mwamafunzi alifurahi kwa kua aliamini atasoma kwenye shule aliyokua akiiota..

Endelea...

Hatimaye siku silizogea sogea na mwishowe mwalimu mkuu mpya akafika. Hata kabla ya utambulisho nilimtambua mwalimu wetu kama Prof.Viru(Virus) wa kwenye picha ya kihindi ya kuitwa "3 Idiots". Prof Viru yeye mda mwingi alikua akiwadharau wanafunzi wake kwani alikua anafuata sana kanuni zake na hakutaka mtu ambishie hata kidogo. Dr Viru alikua na vikanuni vya ajabu ajabu yaani wanafunzi walikua hawali hawalali. Kuna mwanae mmoja akijiua, kuna mwanafunzi mmoja pia alijiua baada ya kushindwa kumaliza project. Mwanafunzi mmoja "Ranchodas" alimchana Dr.Viru kua yeye ndo sababu ya mwanafunzi yule kujiua lakini Dr.Viru alikoroma na kumtaka aachane na hayo mambo.

Lakini niliwapenda sana wanafunzi wale watatu Rancho, Raju na Farhan lakini pia nilimpenda Pia(Kareena Kapoor).

Wanafunzi walijipambanua wenyewe kua sio kila siku mawazo mawazo ya Prof Viru ni sahihi ndio maana kila siku walimpinga. Ila Prof Viru alipania kuwafukuza shule hadi siku ile Rancho alipookoa maisha ya binti yake ndipo aliamini kua Rancho hakua mwanafunzi wa kawaida.(Hii movie inatuonesha umuhimu wa ushirikishwaji wa kila mtu, asa Prof Viru aliwadharau wanafunzi wake lakini mwisho wa siku wakamsaidia.!)

Na huyu mwalimu wetu aliitwa jina kama la Prof Viru yaani "Silencer". Viru hakukubali mwanafunzi aongee isipokua yeye aliamini pale shuleni wanafundisha uhandisi na sio siasa au falsafa.
Mwalimu mkuu mpya alikuja kwa kufanya mageuzi karibu kwenye kila kitu; kamati ya shule ilivunjwa na kuundwa mpya, walimu walibadilishwa, wanafunzi wakapewa muongozo mpya wakuishi pale shuleni. Kila kitu kikawa kipya ndani ya muda mfupi. Kwa kweli alipongezwa saana kwa hatua hatua zake lakini kama wahenga wasemavyo "ukikubali kushangaliwa kubali na kuzomewa pia na asifiaye mvua jua imemnyeshea". Kwanini nasema haya? Mwalimu mkuu licha ya sifa nyingi lakini alikua akikosea kosea katika maamuzi. Aliongea maneno ya mzaha ambayo mwisho wa siku yaligharimu aidha utu,maisha au ustawi wa wanafunzi pale shuleni.

Mwalimu mkuu wetu aliamini kua "No one above, no one below and no one beside him". Na aliamini hakuna kauli au sauti kutoka nje(juu, kulia, kushoto au chini) inayopaswa kumweleza chochote kwani yeye ndie mwalimu mkuu. Wanafunzi waliingiwa na woga hata mimi pia nilikua mmoja wao. Nilitafakari kesho ya shule na shule ya kesho kama itakua salama nikagundua kuna walaini juu ya usalama wa shule. Kwani bado ningali nakumbuka siku moja tukiwa mistarini nilisikia sauti za wanafunzi kwa mbali zikisema "Aah hapa tumesimama tumechoka njaa zinauma lakini mwalimu hatuangalii, anasema atatushibisha wakati hapa ha tuna njaa". Mining'ono hii haikukoma hapa, nilisikia tena wengine wakilaumu na kulumbana "Aah bwana sogea huko, unanibana, jua kali, kiu," wengne waliongea lakini sikumbuki waliongea nini hasa. Wanafunzi walipoona haifai wakapaza sauti wakiomba kusikilizwa maana wamesikiliza sana lakini lakini sauti ya kuunguruma ilisikika ikisema "Mimi ndiye mwalimu mkuu wewe utaongea nini na nani akusikilize"?

Hii kauli ilikua ni msumari wa moto katika jeraha lililoanza kupona. Maumivu yake sio rahisi kuyaelezea hapa.Mr Silencer hakua mtu wa utani hata kidogo. Shule ikaongozwa kwa kauli na sio kwa kiongozi cha mkuu wa shule kama ilivyozoeleka. Ningali sijasahau madhara yaliyompata kiongozi mmoja wa juu nchini Belarus, baada ya kutoa kauli tata jukwaani wananchi wakautii "utata" ule. Kwa hio madhara ya kutamka mbo kibabe au ovyo ovyo ni makubwa saana. Lakini licha ya ufanisi wa Nr. Silencer kwenye maeneo kadhaa bado amefeli kwa sehemu nyingi tuu. Sio rahisi kumhukumu mtu kwa matendo mawili au matatu lakini ukipanda mbegu ya ngano najua itaota ngano, na ukipanda magugu najua yataota magugu. Iweje sasa upalilie ngano kwa kung'oa magugu huku ukipanda magugu mengne??? Hapo ni kutumia fikra ndogo saana. Akipandacho mjinga ndiyo itakua anguko lake la kesho.

Bado niko shule nasoma na sijamaliza. Nitaendelea kuwapa hadithi hii ya Mwalimu mkuu na sasa kumbuka bado tupo na Mr Silencer.
.....Itaendelea...

No comments:

Post a Comment