Sunday, 23 April 2017
UHASAMA WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (2)
USAHAMA WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (2)
Baada ya kipindi cha mazungumzo kiasi baina ya korea na Marekani mwaka 2008 Korea Kaskazini ilishutumiwa kua imeanzisha tena shughuli zake za nyuklia kwenye kinu chake cha Yongbyon. Hii ilikuja baada ya Korea kaskazini kuiambia Marekani imeshindwa kutekeleza baadhi ya matakwa waliyokubaliana ikiwa n pamoja na kutolewa kwenye orodha ya nchi magaidi. Mwaka huo huo wa 2008 mwez october Korea na Marekani waliingia makubaliano kua itaondolewa kwenye nchi zinazofadhili ugaidi.
Baadae mwaka 2009 Korea kaskazini iliwashikilia wamarekani wawili. Marekani iliishutumu korea kwa kuita hukumu hio ya aibu'.
Mwaka 2010 meli ya kivita ya Korea Kusini CHEONAN ilizamishwa majini na Korea kaskazini ilishutumiwa kufanya tukio hilo. Lakini baadae Korea Kaskazini alisema Marekani ndio waliohusika na tukio hilo.
UHUSIANO WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI BAADA YA KIFO CHA KIM JONG-IL
December 17, 2011 mtoto wa wa Kim Jung Il, Kim Jong Un alirithi uongozi kutoka kwa baba yake na tarehe 29 february 2012 Kim Jing Un alitangaza kua Korea kaskazini ingeachana na mpango wake wa nyuklia, ufyatuaji makombora na urutubishaji wa madini ya uranium kwenye kinu chake cha Yongbyon. Na baadae kidogo kiongozi huyo aliialika jumuiya ya kimataifa na pia kuwaita wataalam wa maswala ya nyuklia waliofurushwa nchini humo mwaka 2009. Baada ya hapo utawala wa Obama ulifurahia hatua hio na uliahidi kuwapa Korea kaskazini tani 240,000 za chakula.
Mwezi March 16, 2012 Korea Kaskazini ilibadili mawazo yake na ilitangaza kutuma satelaiti yake ya Kwangmyongson-3 kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il Sung. Kitendo hicho kiliamsha hasira kutoka Marekani na kusababisha kukatisha kwa msaada wa chakula kwa kua walihofia kua urushaji wa satelaiti huambatana na mpango wa makombora.
December 2012 walifanikiwa kufyatua kombora baada ya kushindwa mwezi march kitendo kilichongeza uhasama baina ya mataifa haya.
Mwaka 2013 maafisa wa Korea kaskazini walisema wangefanya jaribio la tatu la nyuklia na walisema "jaribio hili la juu la nyuklia litailenga Marekani., adui mkubwa wa watu wa korea." Na majasusi wa Marekani walithibisha kua jaribio hilo huenda likawa na uwezo wa kufika Hawaii. Na kwa teknolojia waliyakokua nayo ingewachukua miaka mitatu tu kua na kombora linaloweza kufika kwenye ardhi ya marekani.
March 2013 Kim Jong Un alitangaza kua maroketi yalikua tayari kuzisambaratisha kambi za kijeshi za marekani zilizoko Pasifiki kufuatia ndege aina ya B2 kuruka karibu kabisa na Korea kaskazini. April 2013 John Kerry ambae alikua ni waziri wa mambo ya nje wa marekani kwa wakati huo akiwa jijini seoul alisema "Korea kaskazini haitakubaliwa kua taifa la nyuklia" na jaribio lolote la kinyuklia toka Korea kaskazini litakua ni "kosa kubwa".
Mwaka 2014 uhasama uliongezeka baada ya Seth na wenzake kutangaza kuonesha sinema ya kiongozi wa Korea Kaskazini akiuawa na majasusi wa CIA. Korea waliita kitendo hicho kama uchokozi wa wazi na walitishia kushambulia maeneo yote ambayo hio sinema ya THE INTERVIEW ingeoneshwa. Hili ilipelekea Sonny entertainment kuahirisha urushaji wa movie hio siku ilopangwa na pia SONNY entertainment ilidukuliwa. Mwaka 2015 Obama alisema serikali ya Pyongyang ingeanguka. Na mwaka 2016 wanadiplomasia wa Korea Kaskazini walisema kua Marekani iliuvuka "mstari mwekundu" baada ya kiongozi wa taifa hilo kuwekwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo.
April 12, 2017 baada ya majaribio kadhaa ya makombora kutoka Korea kaskazini Marekani ilichukizwa sana na wakati huu Marekani ikiwa na utawala mpya wa Donald Trump. Awali kulikua na taarifa kua Meli za kivita za Marekani zikiongozwa na USS Carl Vinson zikiwa zimesheheni silaha, kama ndege za kivita, makombora na wanajeshi zilikua zielekee Korea Kaskazini kitu kilichoamsha hasira na vitisho kutoka Pyongyang. Pyongyang ilijibu kua iko tayar kwa vita yoyote ile ambayo ingeanzishwa na Marekani. Vitisho vilifikia kiwango cha juu baada ya ziara ya makamu wa raisi Mike Pence aliyoifanya Korea kusini, Japan na Australia huku akisema "Zama za uvumilivu wa kimkakati zimekwisha" na Marekani iko tayari kuikabili Korea kaskazini na pia kuwalinda washirika wake.
Vitisho na mvutano mkali baina ya Washington na Pyongyang ni wa kiwango cha juu kwa kipindi cha hivi karibuni na ni kioo cha kutazama sura halisi za viongozi hawa wanaoonekana kutokua na mzaha, Donald Trump na Kim Jong Un. Ni wazi lugha zao za vitisho zinaweza kuipeleka dunia kwenye vita ya tatu ya dunia.
Sasa makala ijayo tutaangazia kauli za vitisho kutoka Washington na Pyongyang huku tukichambua kidogo uwezo wa kijeshi wa nchi hizi mbili.
Usisahau ku share.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nzuri sana hii bro najitahidi kufatilia hatua kwa hatua
ReplyDeletenzuri sana hii bro najitahidi kufatilia hatua kwa hatua
ReplyDelete