TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA


Picha za smartphone mbalimbali

Miongoni mwa masoko magumu kwa sasa ni pamoja na soko la simu janja au rununu (smartphones) ambapo kila kampuni ya utengenezaji wa siku inajitajidi kutoa simu zenye ubora wa hali ya juu. Lakini sio rahisi kama unavofikiria ikiwa utaulizwa ipi ni simu bora kwa sasa sokoni. Kwa sababu simu moja kutoka kampuni flani inaweza kua bora kwenye eneo moja au mawili hivi lakini ikashindwa kua bora katika maeneo mengine. Lakini kati ya vitu virahisi na hua ni kigezo cha watu kununua simu hua ni kamera. Hii hapa ni orodha ya simu 10 zenye kamera bora sana mpaka sasa. 


1. Huawei Pura 80 Ultra

Huawei Pura 80 Ultra

Ni simu ambayo imetoka mwezi Juni 2025 na imekua ni miongoni mwa simu zenye teknolojia ya kipekee katika kamera na upigaji picha. Simu hii inakupa matokeo mazuri ya picha zenye utajiri na uhalisia wa rangi katika hali zote kwenye mwanga na maeneo yenye mwanga hafifu. Ina usahihi wa rangi ya ngozi ya binadamu (color tone), inapiga picha nzuri sana za portrait pia. Picha na vidio angavu huku lensi ya kujibadili na uwezo wa kuvuta vitu vya mbali na kukupa matokeo mazuri inaipa sifa za ziada. Ina alama 175 na kua simu ya kwanza duniania kufikia ubora huo. 


2. Oppo Find X8 Ultra

Ni toleo la hivi karibuni (April) la Oppo na simu iliyokuja kua imenyooka sana katika upande wa kamera na kuwashangaza watu wengi. Naweza kusema kua simu hii imekamilika kila idara linapokuja swala la kamera. Inakupatia matokeo bora katika picha na video, rangi halisi, portrait kali kwa kulenga kitu husika pekee na hatazile picha za ku zoom mbali zimetoka zikiwa hazina dosari za rangi. Ni ngumu kuona dosari katika kamera kwenye simu hii. Ina alama 169 za ubora wa kamera. 

Oppo Find X8 Ultra 


3. Vivo X200 Ultra

Ni moja kati ya simu iliyosumbua mno huko duniani wakati imetoka mwezi April mwaka 2025. Imekuja na kamera ya hali ya juu sana. Ina uwezo mkubwa wa kupiga picha zenye ubora mkubwa katika karibu kila hali na utofauti wa vitu unapopiga portrait mode mi safi. Na pia inafanya vizuri sana katika ku zoom. Ijapo kunaweza kua na kukosekana kwa uhalisia kwenye baadhi ya mazingira ukitumia zoom ila ni kali sana. Ina alama 167 katika viwango vya ubora.


Vivo X200 Ultra

 

4. Google Pixel 10 XL / Huawei Pura 70 Ultra

Hizi simu hapa zimefungana katika nafasi ha 4. Giogle ikiwa ndio toleo la karibuni zaidi kwani imetoka Agosti 20 mwaka 2025 wakati Huawei Pura 70 ilitoka mwama 2024. Simu zote zina uwezo wa kupiga picha nzuri sana latika mazingira magumu.  Licha ya kwamba zinafanana katika maeneo mengi ila Google Pixel 10 Pro XL inakua na shida kidogo kwenye baadhi ya picha kunatokea details ambazo sio na pia uki zoom sana kuna muda inakupatia picha isiyo na usahihi sana wa rangi. Kwa upande wa Pura 70 Ultra kuna mtu haikupi usahihi wa rangi ikiwa katika mazingira magumu sana mfano mwanga hafifu sana picha inaweza kutoka tofauti kidogo. Zina alama 163 katika viwango vya ubora. 


    Huawei Pura 70 Ultra 

Google Pixel 10 Pro XL 


5. Apple iPhone 16 Pro Max 

Tunafahamu uwezo wa kampuni ya Apple. Ilitoka Septemba 2025 na ni miongoni mwa sinu zilizofanya vizuri sana upande wa kamera na ilikua ndio simu kiongozi kwa upamde wa  kurekodi video. Kamera yake ndio bora zaidi. Inakupatia uhalisia wa rangi katika nyakati zote japo kuna wakati inakua na shida kwa baadhi ya nyakati katika kupiga picha bora ukiwa unatumia tele zoom na shida ya mwitikio baadhi ya nyakati. Ina alama za ubora 161. 


iPhone 16 Pro Max 


6.Google Pixel 9 Pro XL 

Ingizo nyingine kutoka Google ilitoka August 2024 simu hii ina kamera nzuri sana na inafanya vizuri katik video na picha za kawaida. Haikupi kisingizio linapokuja  swala la kamera kwani kwa kusaidiwa na AI tools inatoa picha safi sana. Kasoro kwa baadhi ya maeneo inaweza kua na shida katika portrait mode na maeneo ya mwanga hafifu sana inaweza kukupa matokeo yasiyo bora sana. Ina alama 60 katika viwango vya ubora wa kamera. 


Google Pixel 9 Pro XL 


7.Xiaomi 15 Ultra 

Toleo la Machi 2025 tayari tunaona  Xiaomi ikija na simu yenye kamera kali aana ikiwa na ibora katika upande wa picha za  na inafanya vizuri katika maeneo karibu yote inapo inaweza kukupa matokeo ambayo sio sawa sana linapokuja swala la kurekodi vidio kwani kuna muda inaleta rangi ambazo sio halisi. Ukiwa unatumia simu wakati wa mwanga mdogo pia HDR10 iliyopo haiweki  video kua angavu sana. Ina lama 159 za viwango vya ubora wa kamera. 


Xiaomi 15 Ultra 


8. Honor Magic 6 Pro

Ni moja kati ya simu zenye kamera zilizotimia sana kwa maan kuchukua picha katika hali zote na zaidi zile za ndani lakini pia ina kamera nzuri ya selfie, ni simu nzuri kuchukua picha za familia na katika mazingira yoyote inafanya kazi vizuri sana. Lakini labda kuna baadhi ya nyakati hasa unapochukua video inaweza kukupa matokeo ambayo sio mazuri sana ikiwa hakuna mwanga wa kutosha na pia inaweza kuleta shida mara moja moja kwenye autofocus. Ina alama 158 za ubora wa kamera. 


Honor Magic6 Pro 

9. iPhone 16 Pro 

9. Oppo Find X8 Pro 

9. Huawei mate 60 Pro+ 

9. Oppo Find X8 Pro 

9. Oppo Find X7 Ultra 

Namna 9 ina wateja wengi na sana nitazieleza kwa jumla tu. Simu zote zipo zina kamera nzuri ambazo zinafanya vyema kwa hio unaweza kuondoka na yeyote tu. Apple kama ilivyo kwa iPhone 16 Pro Max inakaribiana kidogo ila ina shida zile zile kwenye telephoto zoom, Oppo iko poa sana kasoro kwenye ku rekodi video kuna muda inaweza ikatoa video sio nzuri sana ila kamera iko safi mno, Huawei pia iko poa sana kasoro kwenye mwanga mdogo, sauti kwenye video na kuna muda haikupi rangi. 

Oppo Find X7 Ultra 


10. Huawei P60 Pro

Inakupa matokeo mazuri ya kamera kwa upande wa picha na video ikiwa ni katika mazingira yoyote ya mwanga. Ni zuri kwa ajili ya kupiga picha matukio ya kifamilia au mkusanyiko wa watu na inakupa picha zenye utajiri wa rangi halisi. Ijapo kua kwa badhi ya nyakati inaweza kushindwa kukupa rangi sahihi ya vitu. Mara chache huweza kutokea. Ina jumla ya alama 156 katika ubora wa viwango vya kamera. 

Huawei P60 Pro

MUHIMU

Mpangilio huu ni kutokana na majaribio ya kisayansi katika maaraba na katika uhalisia lakini tutakua na utofauti kati ya mtumiaji na mtumiaji. Na vimetumika vigezo tofauti tofauti lakini hadi sasa tunaweza kusema hizo ndio simu zenye kamera bora zaidi kwa sasa. 


Samsung S25 Ultra ina alama 151 na iko mbali sana. Kwa sababu wengi najua mngetamani kujua hii. Ina kamera nzuri sana lakini zipo zenye kamera nzuri zaidi. 

Na hii sio kwamba hui ndio list ya jumla ya simu bora hapana. Hii ni katika kipengele kimoja cha kera tu. Subiri vipengele vingine. 

Credit: DXomark 





Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU