HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA
![]() |
| Picha ya pamoja ya viongozi wa Ulaya na Rais wa Marekani ikulu ya Marekani tarehe 18 Agosti 2025. Picha na AFP |
February 2022 Urusi iliivamia Ukraine kijeshi katika kile ambacho Moscow walikiita kama Operesheni Maalumu (Special Operation). Na tangu wakati huo vita hio imeendelea na dalili za kukoma kwake bado zinaonekana ziko mbali kulingana na matokeo ya jitihada mbalimbali za kukomesha vita hivyo. Lakini kwa sasa vita vimeingia katika hatua muhimu na huenda ni hatua mbaya sana ambayo kosa kidogo la kimahesabu limaweza kuigharimu dunia kama ilivyokua Julai 1918 au Septemba 1939 ambapo vita vya kwanza na pili vilianza mtawalia. Kwa sasa vita vya Ukraine vina sura ya tofauti ambayo inahatarisha usalama wa dunia. Na haya ndio mambo ya hatari zaidi ambayo yanaweza kushindwa kuzuilika na kuleta vita ya tatu ya dunia.
1. KUISHIWA SUBRA KWA TRUMP NA PUTIN
Viongozi wote wawili wanashauku kuona vita vinaisha ila kila mtu akiwa na nguvu ya mdukumo ya kipekee na pia ana malengo tofauti. Kinachowaunganisha ni hatma ya vita tu basi mmoja anasukumwa na ufahari na kiburi na mwingine ni historia na matamanio binafsi.
Donald Trump
Kwa sasa anaona yeye ndie "malaika wa amani" na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli (Nobel Peace Prize) kwani anataka kuleta utulivu wa dunia kwa njia yoyote na gharama zozote zile bila kujali madhara kwa wengine. Mfano uvamizi wa Marekani kwenye vinu vya nyuklia huko Iran mwezi Juni ilikua ni lengo la kimkakati kufikia mwisho wa mzozo wa Madhariki ya Kati ambao ungelikua ni mbaya zaidi kama Iran ingebaki na nguvu ile ile. Alifanikiwa kuweka mambo sawa licha ya kwamba nafasi ya Israel pia inabaki kua muhimu.
Lakini sasa vita vya Ukraine vinaweza kumfanya Trump kua na "hasira" lakini pia kua hatari katika maamuzi yake juu ya Putin kwani tayari inaonesha kua Putin hamzingatii sana Trump kama Trump anavyomzingatia Putin. Na mkutano wake wiki jana na viongozi wa Ulaya unampa nguvu nyingine ambayo awali aliikosa. Kwa hio kama atamkosa rafiki yake Putin ataenda na Umoja wa Ulaya na hapa ndipo kunabshida. Shida zinaweza kua hivi;
Mosi, Trump hajafuta kabisa uwezekano wa kuweka majeshi ya Marekani nchini Ukraine na kumbuka wamesaini mkataba wa madini ambapo Marekani anaweza kuingia Ukraine kwa kile ambacho atasema kulinda "assets" za Marekani. Na hilo halitakubalika na Moscow na inaweza kuleta mzozo mkubwa unaoweza kuleta sintofahamu katika amani ya dunia.
Pili, Trump akiona Putin hafikii katika muafaka anaweza kuamua kuipa Ukraine kile inachotaka japo ni hatari sana. Anaweza kuamua kuipa silaha sio tu za ulinzi wa anga bali zile za mashambulizi ya mbali kwa maana ya makombora yanayoweza kupiga ndani kabisa ya ardhi ya Urusi. Na hili linafikiriwa sana na ndio maana Putin anataka kubadili seria na kanuni za matumizi ya silaha za Nyuklia. Kumekuwepo na ripoti kwamba kwa miezi kama miwili hivi Ukraine walikua wanataka kurusha makombora hadi ndani ya Urusi lakini yalizuiwa na Marekani. Endapo uvumilivu wa Marekani utakoma hilo litatokea kwa hakika. Na likitokea basi Moscow na Washington zitakua vitani moja kwa moja.
Vladimir Putin
Sidhani kama Putin alipanga kua na vita ya muda mrefu kiasi hiki huku ikiwa na matokeo yaliyopo sasa. Ukraine ilipaswa kua imeshatwaliwa ama Urusi iwe imeshateka maeneo yote muhimu mpka sasa hasa lile eneo la Donbas. Lakini hilo halijatokea mpaka sasa. Na kadri muda unavyokwenda ndivyo ambayo Ukraine wanapata msaada mkubwa wa ujuzi wa mapambano na silaha. Endapo Putin hatopata matokeo makubwa basi Putin atatakiwa kujiandaa na vita ngumu zaidi na hapa ndipo pia hatari ilipo. Ikiwa Ukraine inatumia silaha zake kuishambulia Urusi itakua ni kama fedheha kwa Putin na kwa hio Putin anaweza kuilaumu Marekani na nchi za magharibi kwa kuisaidia Ukraine kuunda silaha za kuishambulia Urusi. Na hili litamfanya Putin kufikia hatua ya matumizi ya Silaha za Nyuklia. Na tambua kua Ukraine imefanya uvamizi kwenue kinu kimojawapo cha Urusi huko mkoa wa Kurks.
2. UKRAINE INAJIFUNZA NA INAFAULU
Ni watu wachache tulioamini kwamba vita hii haiwezi kua sahihi ukilinganisha na ukubwa wa Urusi na udogo wa Ukraine lakini sipo kubeza juu ya hayo ila ni kuweka sawa kwamba kuna muda uwanja wa vita unazingatia weledi, mipango na unyumbulifu. Ukraine amefanikiwa sana katika teknolojia ya drone za angani na za majini. Kumbuka Urusi imepoteza meli kubwa mbili za kivita na kulamisha kikosi cja jeshi la wabamaji kwenye bahari nyeusi kukimbia na kwenda kujificha. Ni katika hali hii hasara juu ya hasara inaweza kubadili mkondo wa vita na kuivuta zaidi Marekani kumbuka tayari Marekani anahitaji ushirikiano na Ukraine kwenye uundaji wa droni za kisasa.
Ukraine wamefanikiwa kuunda kombora liitwalo "Neptune" ambalo ni la masafa marefu na "Flamingo" la masafa mafupi linalotazamiwa kubadili namna gani vita itapiganwa. Ikiwa likawa na uwezo wa kupenya mifumo ya Ulinzi ya Urusi basi Putin atatakiwa kwenda na silaha ambazo Ukraine hawezi kua nazo na hizo ni Nyuklia na hapo vita ya tatu itakua imefika. Na silaha hizi zinaweza kuwavutia washirika wengine wengi ili kumzuia Putin kufanya hasa uvamizi kwa nchi nyingine. Kwa mataifa mengine vita vya Ukraine na Russia sasa ni fursa kubwa mno.
Ni jambo la kuhofia pale Urusi ikithibitika kwamba haiwezi kujilinda yenyewe. Kumbuka silaha za Urusi zilizotumika mpka nyingi zimeoneka kushindwa kupenya maeneo ya karibu na ilipo mifumo ya ulinzi ya Patriots kutoka Marekani na washirika wake. Na mdio maana ndege za kivita ziliruka juu ya kichwa cha Putin kule Alaska tarehe 15, Agosti 2025. Lilikua ni onyo la wazi la Trump kwa Putin kua hawezi kujilinda na B-2 bombers, F22 Raptor na F35s.
![]() |
| Kombora jipya lililooneshwa na wizara ya ulinzi ya Ukraine. Picha na BBC/ KB LUCH |
Na haya yanaanya mazungumzo ya amani kua mzagumu. Ukdraine kama ambayo Zelenisky alisema hapo jana kua Ukraine bado haijashinda lakini pia bado haijapoteza kwa hio kuna namna anaiona vita ikiwa katika uwanja ulio sawa sawa kila mtu anaweza kupata ushindi kiasi flani. Wakati flani umaweza kupata ushindi katika uwanja wa vita au nje ya uwanja wa vita. Hiki ndio kitu kipo nsani ya Zelenisky. Na namna gani atapata uungwanmji mkono kunaweza kubadili sura ya vita.
Imeansikwa na;
Erick Jerry
karlrck@gmail.com


Comments
Post a Comment