AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? HATIMAYE AFRIKA IMEANZA KUZINDUKA.

Ramani ya dunia 


Tulipokua shuleni tulijifunza mengi juu ya Afrika lakini mengi ilikua ni upotoshaji wa kukusudia au kutokukusudia. Hilo linajidhihirisha pale unapotazama ramani ya dunia. Utaambiwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani nyuma ya Asia lakini ukitazama ramani utagundua Amerika ya Kaskazini inaonekana kuwa ni kubwa kuliko Afrika. Lakini je Afrika ina ukubwa gani? Na kwanini sasa Umoja wa Afrika unahitaji taasisi kuu ulimwenguni kote kutumia ramani mpya ya Afrika kulikoni? 

Tunarejea takribani miaka 456 hivi nyuma kuanzia sasa. Tunakutana na mwaka 1569, na hapo tunakuja kukutana na mtu mmoja aliyepata kua ni mwanajiografia na mchora ramani kutoka Flanders (Kijiografia eneo hili liko Ubelgiji na kijamii na kiutamaduni limekaliwa na watu asili ya Wadachi). Mtu huyu alitwa Gerardus Mercator ambaye ndiye aliyechora ramani hii ya dunia ambayo katika karne ya 18 ilirasmishwa kutumika katika maswala ya usafiri wa majini. 

Imekua ni ramani ambayo inatumika sana katika taasisi za elimu, taasisi za kimatifa kama Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa. Lakini ramani hii ina madhaifu makubwa katika uwiano halisi na ramani kwa maana ya mfumo ambao Mercator aliutumia kuchora ramani unafanya maeneo karibu na ncha za dunia kuonekana makubwa kuliko yale ya Ikweta ilihali uhalisia wake ni tofauti. Kutokana na hali hio bara la Afrika limejikuta linaonekana dogo ukilinganisha na uhalisia. Kwa mfano katika ramani bara la Afrika linakaribiana na kisiwa cha Greenland katika ncha ya Kaskazini lakini uhalisia ni kua Afrika ni kubwa zaidi ya mara 14 ya ukubwa wa Greenland kwa misingi ya kwamba ukiichukua Greenland ni sawa na ukubwa wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tu. Ndio ni hivyo. 

Sasa kutokana na makosa hayo kumekua na jitihada mbalimbali za kusahihisha ramani ya Afrika na sasa swala hilo limefikia hatua za juu ambapo Umoja wa Afrika unashinikiza mabadiliko hayo. Katika program za ramani ya Google kuanzia mwaka 2018 wameweka ramani zote mbili ya maana ramani maarufu ya Mercator Projection na ramani iliyosahihishwa ya "Equal Earth". Hata hivyo hii inapatikana katika mfumo wa talakirishi ya mezani. Katika programu za simu bado ramani ya Mercator inaendelea kutumika. 

Ramani ya Mercator (kushoto) na Equal Earth (kulia)


Lakini katika hatua hizi kwanza na mimi naungana na makundi yote pamoja na Umoja wa Afrika kutaka Afrika ipate kuwasilishwa kwa usahihi na niunge mkono kauli alipyoitoa Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika bi. Selma Malika Haddadi alipoongea na shirika la Reuters kua "inaweza kuonekana kama ni ramani tu, lakini kiukweli sio hivyo". Aliongeza pia kua "kuendana na lengo pana la Umoja wa Afrika (AU) la kuirejeshea Afrika nafasi yake inayostahili katika jukwaa la kimataifa, kupinga simulizi potofu na kutoa uwakilishi sahihi na wa usawa kwa bara la Afrika, na kampeni hii inaendana na [haya] malengo makubwa, aliongeza Selma Malik Haddadi (Tafsiri sio rasmi). Historia ya Afrika inahitaji marekebisho makubwa na hivyo hivyo mageuzi ya kifikra kuhusu mwafrika na U-Afrika wake. Hili sio tu swala la ramani linaenda zaidi ya ramani ni ishara ya mapambano mapana dhidi ya dhulma, kitengwa, kudharauliwa na kudogoshwa kwa Afrika au Waafrika katika maeneo mengine.  Kwa hiyo naamini leo, vuguvugu la ramani ya Afrika linabeba dhana flani ya kiukombozi. 

Ni jukumu la kila Mwanamajumui wa Afrika kuona kwamba mambo yanayohusu Afrika yako sawasawa hata kama yamezoeleka ni lazima kuchungguza upya turudi kwenye asili. Na nitoe Rai kwa walioko katika nafasi za kufundisha kuanzia shule za misingi mpka vyuo tuhakikishe tunahamasisha matumizi ya ramani ya Equal Earth ili kuendelea kua na usawa. 

Unaweza usoma zaidi hapa

https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&opi=89978449&url=https://correctthemap.org/&ved=2ahUKEwjP35iFt5uPAxWOVKQEHcd2DVEQFnoECAoQAQ&sqi=2&usg=AOvVaw1lkGD27d7KpnxPoXomQCKw

Imeandikwa na:

Erick Jerry 
karlrck@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU