Thursday, 13 September 2018

TOP 5 YA MAMBO AMBAYO SIO LAZIMA UMUELEZE MTU.

Imekua ni kawaida sana watu wawili au zaidi mnapokutana basi hua kuna uhitaji wa kujua kwanini mwenzako anafanya hiki au anaoneka vile au anasema kile.  Na ni hadhiri kua binadamu hua tuna tafuta namna ya kuweza "kujitetea" wenyewe.  Lakini je kuna sababu ya wewe kujitetea kwa mtu kwa kila jambo?  Jibu ni HAPANA sio kila jambo ni lazma kulizea.  Wakati flani jitahikunyamaza hususani kwenye mambo haya:


1. KIWANGO CHAKO CHA ELIMU. 
Ni kawaida baada ya kukutana na mtu au kufanya jambo flani wengi hupenda kuzungumzia kiwango chake cha elimu.  "Aah unajua nafanya hivi mimi nina shahada ya kwanza ya... ". Sio lazma kumwambia mtu.  Ongea kitu kingne sio kiwango chako cha elimu .
2. IMANI YAKO. 
Pia,  mara kadhaa watu hujikuta wakiziongelea imani zao baada ya kufanya jambo flan,  mathalani jambo likawa sio la kawaida sana.  Hupaswi kutumia imani yako ya dini kujitetea una/lichokifanya.
3. MUONEKANO WAKO. 
Inawezekana ulikurupuka kuondoka nyumbani asubuhi kwa bahati mbaya hukuweza kutengeneza nywele zako,  hukufunga vizuri tai au vifungo vyako . Kwanini uanze kumuelezea mtu muonekano wako wa siku hio?  Kwanini siku ukiwa sawa humwezei mtu?  Ukigundua usitafute kujitetea ila tatua kinachotatiza pasipokutaka kujieleza.  
4.KAZI NA MSHAHARA WAKO
Imezoeleka watu wageni mkikutana kati ya maswali yatayohusika ni unafanya nini sio?  Ikiwa ni muhimu kusema sema kwani utakua umeulizwa lakin kukutana na mtu na kuanza kumsimulia kazi au kipato chako ni utumwa,  hupaswi kumweleza mtu.

5. MAHUSIANO YAKO.
Ni tatizo pia kwa baadhi ya watu wakikutana na watu wengine kuanza kuzungumzia mahusiano yao ya kifamialia na mapenzi.  Kwani ni lazma?  Utasikilizwa lakini jua kwa kua watu watapenda kusikia ujinga wako lakini hawapendi.  Si vema na busara kujieleza kuhusu mahusiano yako bila sababu.

Share na wenzako waipate. 

No comments:

Post a Comment