Friday, 5 June 2020

HISTORIA FUPI YA UBAGUZI WA RANGI NCHINI MAREKANI


HISTORIA YA UBAGUZI WA RANGI AMERIKA (MAREKANI)

Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha/imani ya kumbagua/kumtenga/kumchukia mtu kwa misingi ya asili yake na rangi ya ngozi yake. Hii sio kitu kigeni sana na ni vigumu kusemea kirahisi ni lini hasa ubaguzi wa rangi ulianza hasa kabla ya karne ya 15. Wakati wazungu wanakuja Afrika kwa mara ya kwanza kutoka Ureno (Portugal) walidhan kua Waafrika ni jamii hasimu kwao kwa maana ina uwezo sawa na wao lakini punde wakajua waafrika walikua dhaifu kwenye baadhi ya maeneo na hapo waafrika wakaanza kuchukuliwa jamii dhaifu (Inferior race). Hali hii ndio iliopelekea kuzaliwa kwa biashara haram na ya kishenzi_biashara ya utumwa.


Kwa hio licha ya Afrika kua na mahusiano na jamii nyingne kama wachina na waarabu lakin vitendo vya ubaguz wa rangi vianzishwa na kupeperushwa na wazungu. Swali ni je kwann uzunguni kwenyewe hakuna ubaguzi uliokithiri kama Marekani? Ubaguzi wa rangi ilikua ni moja ya nyenzo muhim za kutawala maeneo mbalimbali kama Africa, Amerika na Asia kuanzia karne ya 18 mpka mwanzoni mwa karne ya 20. Wazungu walitumia nadharia ya mwanabiolojia Charles Darwin (Social Darwinism theory_Kutoka kwenye kitabu chake cha Evolution of species by means of Natural selection_1859) pamoja na wazo la mshairi wa kipindi hicho Rudyard Kipling aloandika White Man's burden (1899) kuhalalisha ukoloni wa Marekani kwa Ufilipino.

Baada ya kushamiri kwa biashara ya utumwa 85% ya watumwa walipelekwa Amerika (kusini, Caribbean na kaskazini) ambako huko waliwakuta wazungu wengi kutoka Ulaya (kwa sababu kihistoria hakukua na wazungu Amerika kabla wa ugunduzi wa Christopher Columbus mwaka 1492). Hivyo wazungu walishajua hawa ni wadhaifu baada ya hapo ubaguzi ukaendelea kukua kwasababu wazungu waliwatumia waafrika hadi kiwango cha mwisho ili kutimiza malengo yao ya kibepari.

Kutokana na kukomaa kwa ubepari Marekani ilibidi utumwa ukomeshwe kwa kua maslahi ya ubepari yalihitaji watu huru watakaonyonywa kwa ridhaa yao bila wao wazungu kutumia gharama. Baada ya marekani kupata uhuru wao kutoka Uingereza 1776 kulikua na msukumo mdogo saana kwa kukomesha biashara hio dhalimu ya utumwa. Mwaka 1863-1865 Marekani ilitumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe baina serikali ya Muungano na serikali ya majimbo ya kusini yaliyotangaza kujitoa kutoka muungano wa majimbo yaliyounda Marekani.Majimbo ya muungano yakiunga mkono kukomeshwa kwa biashara ya utumwa na kusini wakisema iendelee. Baada ya vita uhasama ulizidi dhid ya Waafrika na hapo vuguvugu la Waafrika kujikomboa likapamba moto na ndio maana moka leo kuna nchi za kiafrika huko Amerika km vile Haiti, Jamaica na Barbados.

Sasa tatizo kubwa ni kua wakati waafrika wanapigania kua huru kutoka na manyanyaso pale Marekani wakawa wanabezwa saana na wazungu na kwa sababu ubaguzi wa rangi umebebwa na dhana ya kua watu wa asili flan ni bora kuliko wengine basi wazungu waliwacheka waafrika wakiojaribu kua na usawa na wazungu kwa kuona ni kituko na kitu kisichowezekana kwa hio vikawekwa vigogo vingi mno. Waafrika hawakuchangamana na wazungu katika maeneo ya umma kama kanisani, usafiri wa umma, hospitali na shuleni. Sheria ziliwabagua waafrika kwan walionekana kama ni binadamu ambao 'hawajatimia' kwa hio kuna haki wazungu waliona hazipaswi kutolewa kwa Afrika. Kadri waafrika walivoongeza nguvu na ushawishi wa kujikomboa ndivyo wazungu walivongeza chuki dhidi yao. Japo swala hili ni swala la mtazamo na imani ambayo jamii inalishwa kwan ukichunguza watoto hawabaguani sana huku mwanzoni ila kwa ngazi ya high school ubaguzi unakua mkubwa kwan ile chuki inajengwa kwa vijana kupitia wazazi wao.

Hadi kufikia miaka 1950s hivi licha ya Marekani kua taifa la kidemokrasia ila haki hizo nyingi zilikua za wazungu sio waafrika. Kinachoendelea sasa hivi Marekani sio kwamba kuna suluhu ya mapema kiasi ambacho watu wana/ngetemea la hasha. Itachukua muda kwani ubaguzi wa rangi ni imani inayoaminishwa miongoni mwa watu waliotofauti juu ya asili zao na imani hio inabebwa nakua 'internalized' kwa muhusika kwa hio mtazamo na imani yake inajengwa kuamini yeye ni bora kuliko mwenzake. Kwa hio vita ya ubaguzi itaenda kwa vizazi na vizaz had pale watoto wa leo watakavyokuzwa na kukua katika misingi ya usawa japo changamoto kubwa nani atawakuza katika misingi ya usawa?!

Nitapitia comment zako ni vipa Amerika inaweza kujijenga katika misingi ya haki na usawa wa rangi. 

#HistoryGuru #LiveThePresentFromThePast

#HistoryHeadquarters 

1 comment:

  1. Njia pekee ya kuleta haki nikuwaenz haki ya mtu mweusi na wale watu wachache weus wachache wenye ushawishi Mkubwa ndani ya mataifa yenye ubaguzi kutumia nafasi zao kuleta mabadiliko chanya ytakayo wapendeza watu wote weupe na weusi na hili wengi wao wameliweza mf mohammed alii, ndio maana hta baadhi ya watu weupe wamekua mstali wa mbele kupinga ubaguzi wa rango kutokana na watu weusi kuonyesha ukarimu na mchango wao katika kujenga mataifa hya yloghubikwa na ubaguzi (watu weusi mifumo Ya maisha yetu ndiyo yatakayochangia kwa kiasi kikubwa kuleta ukombozi wa mtu mweusi)

    ReplyDelete