Wednesday, 30 September 2020

DALILI ZA SIRI AMBAZO ZINAASHIRIA MWILI WAKO HAUKO SAWA.


 

Wakati flani sote hua tunaamini kwamba tuko bukheri wa afya njema kabisa, lakini kwa kiasi kikubwa bado tunaweza kua sio sahihi. Swala la kuhakikisha unakua na afya njema ni la msingi kabisa na ni lazima lipewe kipaumbele. Kuna dalili kadhaa ambazo mwili huonesha lakini wengi wetu huzipuuzilia mbali kwani hua hawaoni kama dalili hizo hazina madhara makubwa kwenye afya yao. Lakini ukweli ni kwamba dalili ndogondogo zina maana kubwa kwa afya yako hivyo basi chukulia tahadhari na umakini mkubwa kuhusiana na vitu hivyo vidogo vidogo zinavyotokea katika mwili wako. Hizi baadhi ya dalili za siri zinazoashiria hauko sawasawa kiafya. 

1. HARUFU MBAYA YA KINYWA 

Ikiwa utakua una tatizo la harufu mbaya mdomoni basi inaweza kua ni kitu ambacho si cha kupuuzia bali kuzingatia kwa sababu wataalamu wa afya wanaamini kua harufu mbaya mdomoni inawezakua ni kitu cha aibu lakini je ni tatizo gani linapelekea hali hiyo? wataalamu wa afya wanaamini kua inawezekana maambukizi ya bakteria katika koo, mdomo au pua huenda yakasabibisha hali hio lakini tatizo kubwa zaidi huenda hio ikawani ni dalili ya aina flani ya kansa. kwa hio ukiona unapatwa na tatizo la harufu mbaya ya kinywa usichukulie poa fanya uchunguzi wa afya yako. 



2. KUCHA NGUMU NA KUNYOFOKA KWA NYWELE 

Tatiozo la kukatika kwa kucha hasa za vidole vya mkono kuvunjika kirahisi inaweza kua ni njia ya mwili kutoa taarifa kua mwili wako unaugua au una tatizo la utapiamlo, anemia au matatizo ya ini kwa hio tilia mkazo juu ya kuchunguza afya yako. pia kunyofoka kwa nywele kusichukuliwe kirahisi kwani endapo nywele zitakua zinanyofoka kwa wingi inaweza kua ni dalili ya ugonjwa wa tezi. 



3. KUKOROMA 

Swala la kutoa sauti kubwa wakati mtu ukiwa umelala linaonekana kama ni jambo la kawaida japo huwakera walio wengi. Tatizo hili linaweza kuashiria kwamba muhusika anaweza kua na tatizo ambalo kitalaamu huitwa "sleep apnea" (tatizo ambalo hufanya mtu asiweze kupumua kwa kipindi flani cha muda). Wakati mwingine huashiria kua muhusika anaweza kua na tatizo la moyo au shinikizo la juu damu. 



4. KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI MAPENZI 

Kuna sababu nyingi ambazo hupelekea tatizo hili ikiwamo matatizo ya akili, matumizi ya baadhi ya dawa na msongo wa mawazo. Kwa hio kukosa hamu ya kushriki tendo la ndoa linaweza kua jambo ambalo ni zaidi ya hizo sababu hapo kwani kupungua au kukosekana kwa msukumo mkubwa wa kushiriki tendo la ndoa kunaweza kua dalili za kisukari, cancer, kuto kuwiana kwa homoni mwilini na jongo. 



5. INSOMNIA (KUKOSA USINGIZI)

Sisi sote tunahitaji muda flani wa kupumzika kwa maana ya kwamba tunahitaji muda kiasi ili kuweza kulala na kuruhusu mwili kufanya kazi yake katika hali ya kawaida na kwa ufanisi mkubwa. Inapotokea mtu anashindwa kupata usingizi kwa masaa mengi mfululuzo maana yake hii sio dalili njema sana kwa afya yake kwani wakati mwingine kukosekana kwa usingizi kunaweza kuashiria matatizo makubwa kama msongo wa mawazo, athma, au ugonjwa wa "Parkinson's"(ugonjwa wa ubongo lakini hujulikana sana kwa dalili ya muhusika kutetemeka mikono na kushindwa kutembea vizuri).  

6. MAUMIVU YA KICHWA 
Maumivu ya kichwa ni kitu ambcho karibu kila mtu humpata wakati flani na mara nyingi maumivu hayo hutoweka yenyewe baada ya muda kiasi au kwa matumizi ya dawa. Hii sio shida sana alakini pale ambapo maumivu ya kichwa yatakua yakijirudia mara kwa mara basi tambua ya kwamba unapaswa kuichunguza vema afya yako kwa maana inawezekana ikawa ni maambukizi, shinikizo la juu la damu, au kiharusi. Ila pia kuna wakati inaweza kua uvimbe katika ubongo au matatizo ya uti wa mgongo (japo haya hutokea mara chache sana lakini muhimu yakazingatiwa pia). 


Help me to share this post. Help me to grow!

No comments:

Post a Comment