Posts

Showing posts from 2023

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU

Image
  'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU K atika ulimwengu wa kijasusi mambo mengi hutokea na wakati Fulani hivi ni ngumu kuamini kama hayo yanayotoka katika ulimwengu huo ni kweli au ni stori za kufikirika. Naam, ni takribani  miaka 50 sasa tangu Israel ilipopata taarifa za shambulio katika ardhi yao ndani ya saa 24 kabla ya tukio kutoka kwa “ANGEL” kwa maana ya “MALAIKA”. Ambapo bila taarifa kutoka kwa huyu "the Angel" kusingekua na Israel na kama ingekuepo basi ingekua tofauti sana na iliyopo sasa. 

BILA HAWA WATANO KUFA, ISRAEL HAIWEZI KULALA GAZA

Image
  Moshi mkubwa baada ya kombora kupiga sehemu ya majengoya Gaza NETANYAHU HAWEZI NA IDF HAIWEZI KULALA KAMA HAWA BADO WAKO HAI Ni zaidi ya miezi miwili tangu Oktoba 7 ambapo wanamgambo wa HAMAS waliweza kuvamia kusini mwa Israel na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu na kibinadamu na kugharimu maisha ya zaidi ya Waisrael 1200 huku wengine zaidi ya 240 wakichukuliwa mateka mpaka ukingo wa Gaza. Benjamin Netanyahu a.k.a Bibi awali alivikosoa vikosi vya jeshi la Israel kwa kushindwa kuzuia shambulio hiilo baya ana la aibu kwa Israel lakini baadae aliomba radhi na ujumbe wake huko X (zamani Twitter) ukaondolewa. Netanyahu aliapa kwamba Israel italipa kisasi juu ya tukio hilo na kwamba Hamas watalipa gharama kubwa na kwamba ni lazima kundi la HAMAS liangamizwe kabisa. J e kauli yake inawezekana? Umeskia nini kuhu Isarel? Inalindwa lakini unajua nini kuhusu HAMAS? Ni kikundi cha magaidi au ni zaidi ya hapo? Fuatilia kwa makini…

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA-3

Image
  HAMAS: KUTOKA KIKUNDI CHA KUTOA MISAADA MPAKA KIKUNDI CHA KISIASA NA KIJESHI.                                  Jeshi la Israel  Ili kuelewa imani na itikadi kali ya Hamas kabla hata kuundwa kwake tuone kidogo ikitikadi ya Waarabu juu ya taifa la Israel hasa kabla ya vita vya siku sita [5-11 June 1967]. Hizi ni kauli za kukupa picha HAMAS wanasimamia nini na Wanapigania nini. Radio Cairo ilitangaza kua " [Watu] Waarabu wamedhamiria kikamilifu kuifuta Israel katika ramani na kirejesha heshima ya watu wa Palestina" . May 25, 1967. May 28, 1967 rais wa Misri Gamal Abdel Nasser anasema   " Hatutakubali uwezekano wowote ule wa Israel na Palestina kuwepo pamoja ". 31 May 1967 rais wa Iraq Abdel Rahman Aref anasema " Uwepo wa Israel ni dosari ambayo ni lazima irekebishwe". Utaona msimamo mkali wa Waarabu dhidi ya Israel kwa hio salama ya Israel ilikua ni kupitia kujua namna gani ataku...

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA SEHEMU YA 2

Image
KUUNDWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA "KUTOWEKA" KWA PALESTINA.   Ramani ya mgawanyo wa maeneo kati ya Israel na Palestina [1948] Jinsi ambavyo Israel na Palestina zilivyo kwa sasa Katika makala hii tutatazama kushamiri kwa mzozo kati ya Waisraeli na Palestina kuanzia 1948 hadi sasa. Hebu tuanze na haya maneno na badae itakusaidia kuelewa vyema.  Nakba ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha "Janga Kuu" yaani "Catastrophe". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kuanzia 1998 siku hii imekua ikisherekewa kama kumbukizi kwa Wapalestina.  Ha'atzmaut ni neno la Kiebrania likimaanisha "Uhuru". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kwa hio tukio lile lile upande mmoja unatambua kua ni Janga kuu na upande mwingine ni Uhuru. Utata unàanza kwamba vita rasmi ya Palestina na Israel ilianza saa ileile ambapo Irael ilijitangaza kwamba ni taifa huru ndani ya taifa huru...

ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?

Image
Picha kwa hisani ya mtandao ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?  "Vita havina macho". Ni msemo tu katika jamii nyingi ukiwa na onyo la kutokushadadia vita.  Tarehe 7 Oktoba 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi kwa saa za Israel, kulitokea shambulio la kushtukiza kutoka kikundi cha HAMAS ambacho kwa tafsiri ya Marekani na washirika wake ni kikundi cha kigaidi.  Tukio hilo lilidhihirisha udhaifu katika idara ya ujasusi ya Israel kwa maana ya Mosad pamoja na Shin Bet. Kikubwa zaidi ni kile kilichokuja kuwa ni kisasi cha Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza. Itoshe kusema mitaa mingi ya Gaza City imekua kama mji wa Kale uliokumbwa na kisa cha kutisha mno. Imekua kama "Ghost City".  Tangu hapo kumekuwa na maoni tofauti juu ya nani yuko sahihi katika hili. Ukweli ni kwamba katika wakati huu ni swali baya ila kikubwa ni nani atasalia? Achilia mbali kua sahihi. 

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA-2

Image
Volume 1 Issue 2 [Muendelezo] 2023/0/25  Rais wa China Xi Jin Ping (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kuliko) China ni Taifa Jeuri na Kiburi Cha Kimya. Ikiwa tunapaswa kuelewa majibu ya China dhidi ya Marekani basi hatuna budi kuangalia hatua mbalimbali ambazo Marekani iliwahi au imezichukua dhidi ya China katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Lakini tutaangazia zaidi hatua zilizochukuliwa katika miaka ya hivi karibuni. Bado ni hoja nyepesi kusema kinachoendelea kati ya Marekani na China ni muendelezo wa vita baridi labda kwa asiyeifahamu vita baridi. Ilikua inatisha kuliko jina lake la ‘vita baridi’. Kuna mambo kadhaa yameweka reheni mahusiano ya China na Marekani na ni muhimu kuyaangazia kiasi.

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA

Image
 Volume 1 | Issue 1 2023/09/24 Meli ya kivita ya Marekani Picha za mtandao Historia ya Taifa la China . Tofauti na Marekani, taifa la China lina umri mrefu sana. Uchina ya kale (“Ancient China”) imekuepo tangu miaka 2000 Kabla ya Kristo/ Kabla ya kipindi cha sasa (2000BC/BCE). Wakati huo Uchina ilikua imegawanyika katika koo mbalimbali kama Zhang, Zhou, Quin, Han na nyinginezo. Ugunduzi wa kale wa risasi, dira, maandishi na uchapaji vilianzia huku. Historia yake ni ndefu mno, hatutoweza kuiandika yote.