Sunday, 24 September 2023

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA

 Volume 1 | Issue 1

2023/09/24

Meli ya kivita ya Marekani

Picha za mtandao


Historia ya Taifa la China.

Tofauti na Marekani, taifa la China lina umri mrefu sana. Uchina ya kale (“Ancient China”) imekuepo tangu miaka 2000 Kabla ya Kristo/ Kabla ya kipindi cha sasa (2000BC/BCE). Wakati huo Uchina ilikua imegawanyika katika koo mbalimbali kama Zhang, Zhou, Quin, Han na nyinginezo. Ugunduzi wa kale wa risasi, dira, maandishi na uchapaji vilianzia huku. Historia yake ni ndefu mno, hatutoweza kuiandika yote.


Wakati wa uundaji wa mataifa ya Ulaya (Formation of nation-states) katika karne ya 17 na kuendelea Uchina bado ilikua iko nyuma kama taifa. Hakukua na Uchina moja. Hii ilipekea Uchina kubaki katika mfumo wa Ukabaila ambapo unyonyaji ulikua mkubwa kupindukia na hivyo kudumaza maendeleo.

Hata hivyo, upande wa Ulaya na Amerika tayari kulikua kumeundwa mataifa mbalimbali kama vile Uingereza (1707, 1801), Uhispania, Ureno, Ufaransa, Italia (1870) na Ujerumani (1871) na Marekani ya sasa ikiwa imejitangazia Uhuru 1776 kutoka kwa Waingereza.

Mataifa mapya ya Ulaya yalianza kujitanua kwa kutafuta makoloni nje ya bara la Ulaya. Maslahi yao makubwa yaliwekwa Asia hasa katika nchi ya China. Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kwa wakati mmoja au mwingine walijikuta wakijimegea maeneo ya China na kuwafanya wachina watumwa! Ndio, Wachina walitumikishwa saana na wazungu ndio maana kupinga utumwa upo kwenye wimbo wa Taifa la China (The March Of the volunteers)

Marekani ilihitaji pia kupata mgao Uchina, lakini haikupendelea ukoloni. Walikuja na Sera Huria maarufu kama Open Door Policy ambapo mataifa yaliyokua yanatawala China yalipaswa kuacha uhuru wa mataifa mengine kufanya biashara na China kupitia bandari zake.

Karne ya 20 jua la utambuzi ndio likaanza kuangazia katika anga la juu ya Uchina iliyogawanyika na kutawaliwa. Mwaka 1911 mapinduzi ya kwanza ya kuindosha familia ya Quin yalifanyika lakini wahafidhina (conservatives_ikiwa sio tafsiri sahihi/rasmi ya neno basi naomba kusahihishwa) walipinga mabadiliko haya.

Kulikua na kipindi cha umwagaji damu hadi miaka ya 1917. Harakati ziliendelea kupamba moto. Wakati huu Marekani alikua muangalifu sana kwa sabanu kwa mara ya Usoshalisti/Ujamaa wa Karl Marx ulikua sio nadhalia bali uhalisia baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917. Alimtazama China kama adui wa Urusi na kama Mshirika wa Urusi. Kuanzia mwaka 1927 mambo yalianza kuonekana sivyo kama Marekani alikua akitatajia, na hapo akawa na wasiwasi zaidi juu ya Uchina. Kwanini?!

Mwaka 1921 kiliundwa Chama cha Kikomunisti huko Uchina. Chama hicho kilikua ni cha kuleta ukombozi kwa China kwa kuwavutia watu wa hali ya chini kama wakulima wa Vijijini. Walifanikiwa lakini kwa Marekani hilo lilikua kosa kubwa mno. Mnamo mwaka 1927 rafiki yake Mao Tse Dong ambaye alikua ni Chiang Kai Shek aliamuru kuwaua wafuasi wa Chama cha Kikomunisti ambao alipaswa kushirikiana nao. Hapo pakalipuka vita kubwa mno vya wenyewe kwa wenyewe.

Vita hii ilimuingiza Marekani huko Uchina moja kwa moja. Kwanini Marekani alivutiwa na vita hii?! Ilikua ni kuuonesha Muungano wa Kisovieti (USSR) kua Ujamaa haukua na nafasib duniani. Alimsaidi Chiang Kai silaha nzito nzito kuanzia bunduki, risasi na ndege. Wakiamini wataweza kusaidia kuwashinda wakomunisisti. Ambacho wakujua ni kua…

Basi ilipofika 1939 vita vya pili vya dunia vikaanza. Kwa Marekani kuingia vitani moja kwa moja bunge la taifa lilikataa hadi Japan alipovamia Kambi ya Jeshi ya Marekani huko Pacific mwaka 1941(Pearl Harbor). Huku dunia ikiwa na vita vyao, China kulikua pia na vita kali mno. Baada ya vita vya pili kuisha, Marekani akakumbuka kua China wangali wanapigana. 

Mwaka 1946 waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Gen. George C. Marshall alizuru China na baada ya kupiga hesabu zake za kina akakubaliana na ukweli ambao kwa Marekani haukupaswa kuonekana unatokea lakini kulikua hakuna namna .. alisema Wachina ambao walikua ni wakomunisti walikua wanashinda ile Vita na sio Chiang Kai Shek ambaye Marekani ilikua ikimsaidia…

Uhasama kati China na Marekani.

Hapo Marekani akaachana kabisa na msaada wake kwa Chiang Kai Shek na mwaka 1949 mapinduzi ya pili yakawa yamekamilika. Na tarehe 1/10/1949 taifa jipya la Jamhuri ya Watu Wa China (PRC). Sasa bwana Chiang Kai Shek hakuuawa wala kukamatwa. Yeye na wafuasi wake walikimbillia katika mojawapo ya Visiwa vya Karibu na China. Kisiwa hicho kwa leo kinaitwa Taiwan na jina rasmi ya serikali ya huko Taiwan kwa kipindi hicho ilikua inaitwa Republic Of China (ROC). MAarekani ilikataa kuitambua serikali ya PRC ikipendelea ROC na ilimkatalia China kua mwanachama wa Umoja wa mataifa hadi mwanzoni mwa 1970s.

Hata hivyo ni muhimu kuelewa kwamba hatua ya Marekani kukubaliana na uwepo wa China ya Kikomunisti ilikua ni sera ya kimkakati ili kuidhoofisha Urusi. Na China kwa wakati huo ilionekana kama taifa ambalo Marekani angeweza kulidhibiti na kulitumia kumdhibiti hasimu wake mkuu ambae ni Urusi. Waziri wa mambo ya Nje Wa Marekani kwa wakati huo Henry Kisinger aliitembelea China na kuandaa njia ya rais wa Marekani kuzuru China (PRC) mwaka 1972 na Richard Nixon anakua rais wa kwanza waarekani alieko madarakani kuitembelea China ambapo walifanya mazungumzo na Mao Ze dong na Zhou Enlai.

Hatua hio ilifungua ukurasa mpya wa mahusiano kati ya China na Marekani lakini yamekua mahusiano ya homa ipanda. Leo mazuri kesho mabovu kulingana na sababu lukuki kama vile mauaji ya Tianjin na kushurutishwa na kukandamizwa kwa waislamu wachache waishio China.

Marekani hajawahi kuona kama China ni tishio kubwa hadi pale ambapo ilikua amechelewa sana kwamba wakati amaewekeza nguvu nyingi kumdhibiti Urusi had kusambaratika kwa Shirikisho la Kikomunisti mwaka 1991 lakini China ilikua iko katika hatua nzuri ya ‘kumjaribu’ na pengune ‘kumuumiza’ Marekani kiuchumi na kisiasa.

Kuanzia 2010-2023 imekua ni kipindi kigumu mno ambapo Marekani anajaribu kumzuia China ambaye tayari ni taifa lenye nguvu kubwa kijeshi na kiuchumi. Uhusiano wao umekua mbaya zaidi na viongozi wa Marekani wanapishana kila mwezi China ili kunusuru nchi hizi kuingia katika vita au kuangusha uchumi wa dunia.

Hadi sasa Marekani amekiri kwamba ni China sio Urusi ambae ni adui namba moja kwao kijeshi na kiuchumi. Kifupi Marekani haelewi afanye nini hasa kumbana China. Hatari kubwa ni kwamba China anajitanua sana Asia hili Marekani lina mtisha sanaa.

Lakini China anajibu nini kutoka katika hatua kali za Marekani dhidi yake? Mambo gani yamezifanya nchi hizi kukaribia vita kamili? Kwanini bado dunia inaogopa kuzorota kwa uhusiano wa China na Marekani?

China ni Taifa Jeuri na Kiburi Cha Kimya.

Mojawapo ya meli za kivita za China


Fuatilia sehemu ijayo kujua majibu ya maswali haya na mengine mengi.

Erick Jerry

Dar Es Salaam

1135

Tanzania

+255629293768 (WhatsApp Pekee)

karlrck@gmail.com


5 comments:

  1. Kuna vita tuitarajie kati ya China na Marekani hivi karibuni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mahasimu wakubwa. Kila nchi imekua na uangalifu ila kuna makosa yanawyeza kusababisha vita. Swali la lini hapo halina majibu. Usikose sehemu ijayo kuona makosa yanayofanyika na kwanini huenda kukawa na vita baina yao.

      Delete
    2. Na ikitoke huenda ikawa vita itakayokumbukwa zaidi. By Mtutu

      Delete
    3. Hupatikani kwa mawasiliano yako mkuu...0763004352

      Delete