YOUTUBE ILITUMIA AKILI UNDE (AI) KUHARIRI VIDEO ZA WATU KWA SIRI



Picha na AFP/Getty Images 


Akili unde (AI) kama inavyofahamika imekua ni mapinduzi makubwa katika sayansi na teknolojia na kwa sasa ni ngumu kuwaza dunia bila Akili unde. AI sasa hivi inatumika katika tafiti za kisayansi, elimu, afya, viwandani, mtandaoni na karibu kila nyanja ya maisha ya binadamu kuna matumizi ya Akili Unde (AI) kwa kiasi fflani. Licha ya kua na fursa nyingi bado AI imeacha mwanya wa changamoto hasa zile zinazohusu hatimiliki na uhalisia wa mawazo au ubunifu kwani kam kitu au wazo litku limesanifiwa na akili unde ni ngumu kudai kwamba ni wazo lako licha ya kwamba uliielekeza namna ya kufanya. Katika changamoto mojawaponkubwa sasa inaikumba kampuni ya Google kupitia bidhaa yake ya YouTube.


Kumeibuka malalamkkko kwamba YouTube ilitumia AI kuhariri picha za video za watu na kubadili kwa namna flani rangi ya ngozi za wahusika na rangi za nguo bila ridhaa ay taarifa kwa wahusika. Jambo hili kimezua maswali mwngi juu ya namna AI inaweza kua na nafasi katika kubadili mkondo wa mambo na namna inavyoweza kuathiri uhusiano baina ya utengenezaji wa maudhui na mtazamaji au mtumiaji wa mudhui kwa sababu utengenezaji maudhui anawajua watumiji wake na anafahamu sana juu ya utambulisho wake kwa hio mbadiliko kiasi tu yanaweza kua na athari kubwa kwa upande mmoja. 

Licha ya utofauti mdogo ambao inaweza kua sio rahisi sana kuuona kwa haraka lakini wazi kwamba sasa AI imeanza kuingili kati kwenye maisha halisia ambayo kwa kipindi kirefu watu tumekua tukiyafurahia na hilo linawezekana kututenganosha sisi na asili. Licha ya kwamba watu walianza kulalamikia juu ya hili walau tangu mwezi Juni 2025 lakini YouTube walikua hawajatoa tamko rasmi hadi hivi karibuni walipokiri kwamba walitumia AI kuhariri picha mjongeo (vidio) kwa baadhi ya watumiaji. Na kulingana na taarifa ya msemaji wa idara ya Watengeneza maudhui (Creators) Rene Ritchie alisema kupitia mtandao wa X (Twitter) kua wamesikia wasiwasi wa watengeneza maudhui juu ya YouTube kuhariri video zao na kusema wanafanyia kazi hilo kwa kuweka kipengele cha watengeneza maudhui kichagua kama wataridhia au kucha endapo hawatoridhia na kusema kwamba watu wakae mkao wa kulabkwani kuna mambo mengi mazuri yaanakuja. 

Ingawa imetolewa taarifa hio lakini bado kuna maswali mengi kwamba kwanini walifanya kwa siri na kwanini hawakuwashirikisha wahusika kupata kibali au maoni yao? Kwa sababu waathirika wengi wamesema hawakufurahishwa  na uharirir huo na kama wangelitaka kufanya ambacho YouTube wamefanya wangweza kudanya wao wenyewe lakini hawakufanya. 

Na pia kwa sasa YouTube wanataka kuzuia kufanya malipo kwa watu wanaotumia vidio zilizotengenezwa kwa AI. Sasa ikiwa hilo ndilo walifanyalo je kwanini waweze kuzuia watu kutumi AI.? Ni sawa wantaka kuona ubunifu wa watu, na kwanini wao wafanye uhariri wa vudio? 

Je, wewe kuna namna yoyote ambayo AI imekuathiri? Tuendelee kuchukua tahadhari wakati wa maatumizi ya huduma na bidhaa za Akili Unde kwani sio kila kitu kinakua kizuri. Na faida zilizopo za Akili Unde basi tuzitumie vyema. 



Comments

Popular posts from this blog

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?