Posts

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2017

Image
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2017

Serikali imetoa orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.  Kuangalia orodha hio bofya hapa; 1.  http://www.tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/ 2.  http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/tangazo-1068-20170609-Uchaguzi-kujiunga-kidato-cha-5-vyuo-vya-ufundi-2017/ORODHA-YA-WANAhiFUNZI-WATAKAOPANGIWA-AWAMU-II.pdf

WATU WALIOKATALIWA KUISHI NCHI KAVU.

Image
Wabajui huishi na familia zao kwenye vibanda vyao vya miti vilivyojengwa baharini kwani wamezuiwa kuishi nchi kavu na pia pia wakikaa sana nchi kavu wanajihisi kuumwa.  Dunia ina mambo mengi sana, mengine yanastaajabisha, mengine kuudhi na mengine kufurahisha. Ila hili sijui linaleta picha gani. Bahari ni makazi ya karibu nusu ya viumbe hai waishio duniani ila sisi binadamu sio mojawapo ya viumbe hivyo kwani hatuwezi kukaa ndani ya maji ya chumvi kwa   muda mrefu, hatuwezi kuzama na kukaa kwenye kina cha bahari kwa muda mrefu lakini kinyume na haya yote kuna baadhi ya binadamu karibia maisha yao yote ni baharini! Wamejenga "vijumba/vibanda" vyao vya miti huko na asilimia zaidi ya 90 wanaishi huko na sio nchi kavu! Naam, ni watu jamii ya

KOREA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA JIPYA.

Image
Google Uwezo wa makombora yanayomilikiwa na Korea kaskazini.  Korea kaskazini imerusha kombora jingine mapema leo jumapili ambalo liliruka karibu 700km, hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Korea kusini. Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tu tangu rais mpya wa Korea kusini kushika wadhifa wa urais hapo jumatano. Rais mpya wa Korea alisisitiza kua yuko tayari kufanya mazungumzo na utawala wa Pyongyang kama mazingira yataruhusu.

MTOTO WA OSAMA BIN LADEN AAPA KULIPA KISASI

Image
Mmoja kati ya watoto wa aliyewahi kua kiongozi wa kundi la Al qaeda ameapa kulipa kisasi cha mauaji ya baba yake yaliyotekelezwa na kikosi cha makomando wa kimarekani mwaka 2013 nchini Afganistani.  Picha hii ilipigwa na kituo cha televisheni cha Al jazeera japo haifahamiki ilikua ni lini.  Mtoto wa Osama bin laden anasemekana kua anapanga kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi juu ya kifo cha baba yake kilichotokea May 2013. Mtoto huyo pia (Hamza) anajiandaa kua kiongozi mpya wa kundi la Al Qaeda. 

MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI. (2)

Image
Muendelezo wa vitisho baina ya korea kaskazini na Marekani kwa mwezi wa nne 2017.   Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC) April Korea kaskazini ilirusha kombora jingine kulenga bahari ya Japan na kitendo kilichozua hofu kubwa toka Japan. Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.

MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (1)

Image
DUNIA YA VICHWA VIWILI VISIVYOTOSHANA. Meli ya kubeba ndege na makombora ya Marekani ikiwa njiani kuelekea eneo la bahari la korea kufuatia mvutano mkali baina ya Korea na Marekani. Kuna wasiwasi wa dunia kutumbukia kwenye vita mbaya ya nyuklia kutokana na vitisho baina ya Marekani na Korea kaskazini. Kumekuwepo na vita za maneno na vitisho baina ya Washington na Pyongyang watishiana kupigana baada ya kipindi kirefu cha bila maelewano baina yao.