Posts

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA-3

Image
  HAMAS: KUTOKA KIKUNDI CHA KUTOA MISAADA MPAKA KIKUNDI CHA KISIASA NA KIJESHI.                                  Jeshi la Israel  Ili kuelewa imani na itikadi kali ya Hamas kabla hata kuundwa kwake tuone kidogo ikitikadi ya Waarabu juu ya taifa la Israel hasa kabla ya vita vya siku sita [5-11 June 1967]. Hizi ni kauli za kukupa picha HAMAS wanasimamia nini na Wanapigania nini. Radio Cairo ilitangaza kua " [Watu] Waarabu wamedhamiria kikamilifu kuifuta Israel katika ramani na kirejesha heshima ya watu wa Palestina" . May 25, 1967. May 28, 1967 rais wa Misri Gamal Abdel Nasser anasema   " Hatutakubali uwezekano wowote ule wa Israel na Palestina kuwepo pamoja ". 31 May 1967 rais wa Iraq Abdel Rahman Aref anasema " Uwepo wa Israel ni dosari ambayo ni lazima irekebishwe". Utaona msimamo mkali wa Waarabu dhidi ya Israel kwa hio salama ya Israel ilikua ni kupitia kujua namna gani ataku...

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA SEHEMU YA 2

Image
KUUNDWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA "KUTOWEKA" KWA PALESTINA.   Ramani ya mgawanyo wa maeneo kati ya Israel na Palestina [1948] Jinsi ambavyo Israel na Palestina zilivyo kwa sasa Katika makala hii tutatazama kushamiri kwa mzozo kati ya Waisraeli na Palestina kuanzia 1948 hadi sasa. Hebu tuanze na haya maneno na badae itakusaidia kuelewa vyema.  Nakba ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha "Janga Kuu" yaani "Catastrophe". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kuanzia 1998 siku hii imekua ikisherekewa kama kumbukizi kwa Wapalestina.  Ha'atzmaut ni neno la Kiebrania likimaanisha "Uhuru". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kwa hio tukio lile lile upande mmoja unatambua kua ni Janga kuu na upande mwingine ni Uhuru. Utata unàanza kwamba vita rasmi ya Palestina na Israel ilianza saa ileile ambapo Irael ilijitangaza kwamba ni taifa huru ndani ya taifa huru...

ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?

Image
Picha kwa hisani ya mtandao ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?  "Vita havina macho". Ni msemo tu katika jamii nyingi ukiwa na onyo la kutokushadadia vita.  Tarehe 7 Oktoba 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi kwa saa za Israel, kulitokea shambulio la kushtukiza kutoka kikundi cha HAMAS ambacho kwa tafsiri ya Marekani na washirika wake ni kikundi cha kigaidi.  Tukio hilo lilidhihirisha udhaifu katika idara ya ujasusi ya Israel kwa maana ya Mosad pamoja na Shin Bet. Kikubwa zaidi ni kile kilichokuja kuwa ni kisasi cha Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza. Itoshe kusema mitaa mingi ya Gaza City imekua kama mji wa Kale uliokumbwa na kisa cha kutisha mno. Imekua kama "Ghost City".  Tangu hapo kumekuwa na maoni tofauti juu ya nani yuko sahihi katika hili. Ukweli ni kwamba katika wakati huu ni swali baya ila kikubwa ni nani atasalia? Achilia mbali kua sahihi. 

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA-2

Image
Volume 1 Issue 2 [Muendelezo] 2023/0/25  Rais wa China Xi Jin Ping (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kuliko) China ni Taifa Jeuri na Kiburi Cha Kimya. Ikiwa tunapaswa kuelewa majibu ya China dhidi ya Marekani basi hatuna budi kuangalia hatua mbalimbali ambazo Marekani iliwahi au imezichukua dhidi ya China katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Lakini tutaangazia zaidi hatua zilizochukuliwa katika miaka ya hivi karibuni. Bado ni hoja nyepesi kusema kinachoendelea kati ya Marekani na China ni muendelezo wa vita baridi labda kwa asiyeifahamu vita baridi. Ilikua inatisha kuliko jina lake la ‘vita baridi’. Kuna mambo kadhaa yameweka reheni mahusiano ya China na Marekani na ni muhimu kuyaangazia kiasi.

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA

Image
 Volume 1 | Issue 1 2023/09/24 Meli ya kivita ya Marekani Picha za mtandao Historia ya Taifa la China . Tofauti na Marekani, taifa la China lina umri mrefu sana. Uchina ya kale (“Ancient China”) imekuepo tangu miaka 2000 Kabla ya Kristo/ Kabla ya kipindi cha sasa (2000BC/BCE). Wakati huo Uchina ilikua imegawanyika katika koo mbalimbali kama Zhang, Zhou, Quin, Han na nyinginezo. Ugunduzi wa kale wa risasi, dira, maandishi na uchapaji vilianzia huku. Historia yake ni ndefu mno, hatutoweza kuiandika yote.

DALILI ZA SIRI AMBAZO ZINAASHIRIA MWILI WAKO HAUKO SAWA.

Image
  Wakati flani sote hua tunaamini kwamba tuko bukheri wa afya njema kabisa, lakini kwa kiasi kikubwa bado tunaweza kua sio sahihi. Swala la kuhakikisha unakua na afya njema ni la msingi kabisa na ni lazima lipewe kipaumbele. Kuna dalili kadhaa ambazo mwili huonesha lakini wengi wetu huzipuuzilia mbali kwani hua hawaoni kama dalili hizo hazina madhara makubwa kwenye afya yao. Lakini ukweli ni kwamba dalili ndogondogo zina maana kubwa kwa afya yako hivyo basi chukulia tahadhari na umakini mkubwa kuhusiana na vitu hivyo vidogo vidogo zinavyotokea katika mwili wako. Hizi baadhi ya dalili za siri zinazoashiria hauko sawasawa kiafya. 

HISTORIA FUPI YA UBAGUZI WA RANGI NCHINI MAREKANI

Image
HISTORIA YA UBAGUZI WA RANGI AMERIKA (MAREKANI) Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha/imani ya kumbagua/kumtenga/kumchukia mtu kwa misingi ya asili yake na rangi ya ngozi yake. Hii sio kitu kigeni sana na ni vigumu kusemea kirahisi ni lini hasa ubaguzi wa rangi ulianza hasa kabla ya karne ya 15. Wakati wazungu wanakuja Afrika kwa mara ya kwanza kutoka Ureno (Portugal) walidhan kua Waafrika ni jamii hasimu kwao kwa maana ina uwezo sawa na wao lakini punde wakajua waafrika walikua dhaifu kwenye baadhi ya maeneo na hapo waafrika wakaanza kuchukuliwa jamii dhaifu (Inferior race) . Hali hii ndio iliopelekea kuzaliwa kwa biashara haram na ya kishenzi_biashara ya utumwa.