Sunday, 17 July 2016

UFAFANUZI WA TCU JUU YA VIWANGO VYA UDAHILI.

Kufuatia tangazo lililotolewa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) wiki iliyopita kumekua na sintofahamu miongoni mwa wadau na wanafunzi juu ya sifa na vigezo vitakavyotumika kwenye udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Mapema wiki iliyopita TCU ilibanisha kua ili kujiunga na chuo lazima uwe na alama D ambazo ni pointi 4.


Sifa hizo zilizowekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU, Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa ‘D mbili’ pointi 4.0. Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokan na ufaulu wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1 .

 Taarifa hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 ili wawe na sifa za kudahiliwa z, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa ‘C mbili’ pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B+=4; B=3; C=2; D=1. Kupitia tovuti hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu watahitajika kuwa na ufaulu wa alama ‘D mbili’ 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1. Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F=0-38.

Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na baraza ka Taifa la mitihanai ‘NECTA’ na mafunzo ya ufundi ‘VETA’ Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.

Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udaahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA. Lakini ufafanuzi uliotolewa jana unaonesha kua hata wale wanafunzi wenye point 4.0 lakini hawana D mbili mfano C na E wanaweza kujiunga na chuo kwani kwa mchanganuo (C=3 na E=1: 3+1=4)

No comments:

Post a Comment