Sunday, 13 August 2017

VURUGU ZIMEZUKA KWENYE MAANDAMANO MAREKANI



Waandamanaji wakiwa katika moja ya viunga vya Charlottesville, Virginia. 

Mamia ya  wamarekani weupe (wazungu) na wale wanaowapinga walitarajia kufanya maandamano leo jumamosi kwa kile kilichofahamika kama "Unite the Right"(Ungana na mrengo wa kulia)  huko Charlottesville, Virginia
mara baada ya uamuzi wa majaji kuruhusu tukio hilo kufanyika.  Maamuzi hayo ya mahakama yalipelekea kufanyika kwa  matembezi  jana(ijumaa) na yaliyopelekea kuzuka kwa vurugu kati ya watembeaji,  wapingaji wa matembezi hayo na polisi.
Hali hio ilipelekea gavana wa jimbo la Virginia kuweka tayari vikosi vya ulinzi na usalama ili kudhibiti hali ya usalama.

Muda mfupi baada ya matembezi hayo kulizuka vurugu kubwa baina ya waandamanaji ambao ni kundi kubwa la wamarekani weupe dhidi ya wanaopinga maandamano hayo ambao wengi ni wamarekani weusi.  Vyombo vya habari nchini marekani vimeripoti kua katika maandamano hayo kulitokea mtu mmoja akaendesha gari katikati ya umati wa watu na kupelekea kifo cha mtu mmoja na wengine 19 kujeruhiwa.

Viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu wa Marekani wametoa wito kwa wamarekani wote na kutaka kuwepo na mshikamano na pia kuacha chuki dhidi ya rangi tofauti.

No comments:

Post a Comment