Saturday, 19 August 2017

KANDE ZA MPAISHA MTU HUKO KENYA.


Martin Kamotho (Githeriman)  kabla na baada ua kupata msaada. 
Picha kwa hisani ya Google. 

Maisha hayana maana moja na kila mtu atatoa maana ya maisha kwa vile ambavyo yeye anachukulia ni nini maisha yana maanisha kwake. Na kila siku hua tunasikia watu wakisema "Hakuna kukata tamaa" ni kweli lakini mwingine anajiuliza kwanini nisikate tamaa??  Kila mtu ana jibu lake sasa leo tumepata somo jingine zuri sana kutoka Kenya.
Ilikua ni jumanne tarehe 8 mwezi August 2017, siku ya uchaguzi wa Kenya.  Kuna jamaa alikutwa akila Githeri(makande) akiwa kwenye foleni ya kupiga kura.  Muda mfupi baadae picha yake ili trend kwenye mitandao ya kijamii kwa jina au hashtag ya #Githeriman

Lakini Githeriman ni nani?!  
Anaitwa Martin Kamotho,  mfanya usafi kwenye county ya Nairobi. Bwana Kamotho ameteka hisia za watu wengi wa taifa la Kenya baada ya picha yake akila kande kwenye foleni ya kupiga kura.  
Licha ya maisha duni ya bwana githeri lakini amegeuka kua kivutio kikubwa siku na baada ya uchaguzi nchi Kenya.  Watu wengi wali hariri picha yake na kuitumia sehemu mbalimbali labda kwa lengo la kujifurahisha tu,  lakini unajua nini kwa sasa?!  
Kwa sasa githeriman amepewa mikataba ya matangazo kutoka kwa makampuni kadhaa ya kutengeneza vyakula,  lakini pia amepewa ardhi jijin Nairobi na kampuni ya Ngong Crescent yenye thamani ya Ksh269,000.
Lakini pia kampuni ya Safaricom imempa simu aina ya Samsung Galaxy s8+ yeye pamoja na mkewe. Huku mwanae akipewa Tecno Camon x.




No comments:

Post a Comment