Volume 1
Issue 2 [Muendelezo]
2023/0/25
![]() |
Rais wa China Xi Jin Ping (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kuliko) |
China ni Taifa Jeuri na Kiburi Cha Kimya.
Ikiwa tunapaswa kuelewa majibu ya China dhidi ya Marekani basi hatuna budi kuangalia hatua mbalimbali ambazo Marekani iliwahi au imezichukua dhidi ya China katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Lakini tutaangazia zaidi hatua zilizochukuliwa katika miaka ya hivi karibuni.
Bado ni hoja nyepesi kusema kinachoendelea kati ya Marekani na China ni muendelezo wa vita baridi labda kwa asiyeifahamu vita baridi. Ilikua inatisha kuliko jina lake la ‘vita baridi’. Kuna mambo kadhaa yameweka reheni mahusiano ya China na Marekani na ni muhimu kuyaangazia kiasi.
1. Taiwan na mustakabali wake wa baadae
Hili limekua ni swala kubwa sana katika mahusiano ya kidiplomasia kati ya China na Marekani. Katika makala iliyopita nilikueleza kuundwa kwa Taiwan (ROC) na China (PRC), sasa tangu 1949 mpaka leo China inaitambua Taiwan kama Jimbo lililojitenga na sio kama nchi na naam hata jumuiya ya kimataifa inatambua hivyo unajua kwa nini?
Ilikua 1972 ambapo Marekani na China walisaini Xhanghai Communique ambalo ulikua ni mwanzo wa uanzishwaji wa uhusiano wa Kidiplomasia ya ya Marekani na China ambayo yalianza rasmi 1979 chini ya Jimmy Carter. Mwaka huo China kulikua na Mapinduzi ya Kijamii na Kiutamaduni nchini China kitu kilichopelekea kuruhusu uchumi wa soko. Kilichosainiwa kinaitwa “One China Policy” au “Sera ya China moja” ambapo Marekani ilitambua kua kuna serikali moja tu ya China na Taiwan ni sehemu ya China ila Marekani ilisaini makubaliano na Taiwan kuipa ulinzi na ndio maana hadi leo Marekani inauza silaha kwa Taiwan kitu ambacho China inakipinga kwa nguvu zote.
Uongozi wa Bwana Donald Trump (2016-2020) ulikiuka sana haya makubaliano na kufanya uhusiano na China kuzorota sana katika kipindi hicho. Hata hivyo Joe Biden ameshikiria pale na katika kipindi cha Biden viongozi wa ngazi za juu akiwepo Spika wa Bunge la taifa (Nancy Pelos) na Rais Joe Biden wamezuru Taiwan kwa nyakati tofauti. China ilitishia kudungua ndege za Marekani kwa kufanya mazoezi makali lakini hawakudungua japo walilaani kitendo hicho na kuita kwamba Marekani walivuka ‘mstari mwekundu’. Unadhani ni uoga? China ameoneshs visa vingi vya uchokozi kwa Marekani pia hasa katika bahari ya Kusini mwa China.
![]() |
Picha kwa hisani ya AP |
2. Sera ya kujitanua ya China katika Bahari Ya Kusini mwa China (Southern China Sea)
Ni moja kati ya chanzo cha mvutano kati ya China na majirani zake Philippines, Vietnam na Indonesia. Sasa Marekani anaingiaje? China anajenga kisiwa bandia (Artificial Island) ambako ataweka kambi kubwa ya kijeshi kitu ambacho kitaathiri Marekani na washirika wake kufanya ujasusi dhidi ya China na itaipa ugumu jeshi la Marekani kuidhibiti China ikiwa kutazuka vita kamili. Meli za kijeshi za China na Marekani zimepishana kwa namna hatarishi sana eneo hili kitu ambacho wakati mmoja mwaka 2022 isingelikua Meli ya Marekani kuounguza mwendo basi zilingeligongana ila China alifanya makusudi, kwa kudhamiria. Ila nini kingetokea kama wangegongana?
Ikiwa hilo halitoshi ndege za kijasusi za Marekani zimeweza kutambuliwa na Kufurushwa “scrambled” na ndege za kivita China na tena mwaka huu 2023 ndege ya kivita ya China ilifanya manuva mbele ya ndege ya Marekani ambapo wizara ya ulinzi ya Marekani ilikiri kua kitendo kile kilikua ‘hatari’ na kisicho cha ‘kitaalamu’ na kuonya kua China inapaswa kuacha mara moja. Lakini kwa China aliskia?, Naam, ni Jeuri mkimya.
Vitendo hivi vimeifanya Marekani kuunda muungano usio rasmi wa kuweza kukabiliana na China. Muungano huu unaoitwa UKUSA unahusisha United Kingdom (Uingereza), USA(Marekani na Australia. Hii ni kujiandaa ikiwa kutakua na ulazima wa Jeshi la wanamaji kupambana na China katika bahari ya Pacific.
![]() |
Maeneo ambayo yanazozaniwa katika Bahari ya kusini mwa China |
3. Haki za binadamu na vilwazo vya kibiashara
China iko katika shinikizo kubwa la utesaji wa raia wachache hasa jamii ya Waislamu wa Urghls lakini China inakataa. MAarekani analazimisha China ionekane ina makosa na China nasema Marekani inaichokoza kwa kuichafua katika jumuiya ya kimataifa kwa shutuma za uongo na kwamba hayo ni maswala ya ndani ya China.
Tangu 2018 China imewekewa vikwazo vya kibishara mfano HUAWEI haipaswi kutumia teknolojia ya Marekani ndio maana simu zao hazina Google services kama Gmail, YouTube. Hazitumii chip za Snapdragon katika vifaa vyao. Makampuni mengi yamefungiwa kufanya biashara na Marekani kwa madai ya kua yanatumika na serikali ya China kuchunguza Marekani. Hili limekua na athari kubwa mno katika uchumi wa China ambao kwa sasa ni kama bomu la ku set muda wa kulipuka.
China imekua mara kwa mara ikijibu vikwazo vya kiuchumi kwa kuweka vikwazo kwa bidhaa za Marekani hii imepelekea mahusiano mambovu na uhasama baina yao. Lakini kugokana umuhimu wa China kwa uchumi wa dunia wizara ya biashara na hazina imefanya juhudi kuhakikisha wanaondoa vikwazo na wameanza kulegeza mwaka huu 2023. Licha ya athari kwa pande zote ila katika hili China kaathirika zaidi.
4. Kujiimarisha kijeshi kwa China
Marekani ina hofu kubwa mno juu ya usiri wa matumizi ya Jeshi la China na uwekezaji ambao China inaufanya jeshini. Kumekua na kuongezeka kwa kasi ya juu mno ya bajeti ya Ulinzi ya China. Maeneo makubwa ni kuimarisha jeshi la wanamaji (Chinese Navy), Jeshi la Anga (Air Force) na Silaha za kimkakati ikiwepo Silaha za Nyuklia. Na hakuna uwazi wa kutosha. Marekani anashindwa kua na taarifa sahihi za uwezo wa kijeshi wa China hivyo anajaribu kupata taarifa nyeti lakini mara zote imekua ngumu na hii inayumbisha uhusiano wao. Lakini mzozo wowote wa kijeshi ni hatari si kwa mataifa hayo mawili bali kwa dunia nzima.
Lakini pia China ilituma balloons za kijasusi na kibaya zilifika hadi nchi Marekani na Marekani ilichelewa kujua kwamba ni wachina wanakusanya taarifa za kijasusi hili lilionekana kua China alikua ndani ya Marekani katika mission kubwa. Tangu hapo kumekua na vizuizi vingi sana kwa Wachina nchini Marekani.
Jeshi la China (Juu)Jeshi la Marekani (Juu)
Wanaweza kuingia katika mzozo wa kijeshi lakini nani naweza kushinda vita? Si rahisi kuingia vitani na si rahisi kujua nani anaweza kushinda. Sehemu inayofuata itakua nguvu za kijeshi baina yao na kwanini bado ni tishio kwa dunia yetu.
Erick Jerry
Dar Es Salaam
1135
Tanzania
+255629293768
karlrck@gmail.com
Marekani ulimwengu unakwenda kumchoka kwa vitimbi vyake dhidi ya washindani wake kibiashara na hapa tutashuhudia machafuko makubwa sana.
ReplyDelete