Posts

SAWA, HATIMAE MUGABE AKUBALI KUJIUZULU.

Image
Kwa mujibu wa taarifa ya CNN imeripoti kua chanzo rasmi kinachofuatilia mazungumzo kati ya rais Mugabe na maafisa wa jeshi kimedokeza kua rais Mugabe amekubali kujiuzulu kufuatia hatua ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo kumuweka kizuizini kwa siku kadhaa.  Hatua hii inakuja kufuatia hatua yake ya jana jumapili ambapo kwa mara ya kwanza tangu awekwe kizuizini nyumbani kwake alilihutubia taifa kupitia shirika la utangazaji la nchi hio ZBC.

MUGABE ATIMULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF

Image
Chama tawala cha ZANU-PF cha  nchini Zimbabwe kimeridhia kumuondoa Robert Mugabe kama mwenyekiti wake na kumteua aliyekua makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa kua mwenyekiti mpya wa chama hicho.  Mnangagwa alifutwa kazi na rais Mugabe siku chache zilizopita na kutaka kumtangaza Grace Mugabe kua makamu wa rais na hatimaye aje kua mwenyekiti na baadae rais wa Zimbabwe kitu kilichoamsha hasira na sintofahamu miongoni mwa wazimbabwe wengi. Hatua hio ilimlazimu generali wa jeshi la zimbabwe (ZDF) Gen Constantino Chiwenga kutangaza kuingilia kati mzozo huo siku ya jumatatu na siku ya jumatano  vikosi vya jeshi kulazimika kuchukua udhibiti wa serikali kwa kumuweka kizuizini rais Mugabe na kutaka atangaze kuachia madaraka hatua iliyosimamiwa na kanisa katoliki lakini taarifa zilidai kua Mugabe alikataa kufanya hivyo na pia vilizingira kituo cha habari cha ZBC. Hata hivyo leo chama hicho tawala kimeamua kumvua uongozi mwenyekiti wake Robert Mugabe 93, pamoja na mkewe G...

UTUMWA BADO UNAITESA DUNIA YA TATU

Wakati dunia ikifurahia na kusherehekea mafanikio mengi na hatua kubwa iliyofikiwa na binadamu, hii sio habari na sio furaha ya kila mtu.  Ni wakati ambao baadhi ya jamii zinataabika kwa mabalaa ya umaskini uliokithiri,  njaa kali,  majanga ya asili na vita vya wenyewe kwa yenyewe na kubwa zaidi ni SULUBU YA UTUMWA!

DROO YA MAKUNDI YA UEFA 2017/2018

Image
Droo ya kupanga makundi ya UEFA kwa msimu wa 2017/2018 imefanyika leo huko Monaco,  Ufaransa.  Shirikisho la soka barani ulaya leo tarehe 24, August 2016 limetoa tuzo kwa wachezaji nyota waliong'ara kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya(UEFA Champions League) kwa msimu wa 2016/2017 pamoja na kutoa orodha ya makundi ya michuano hio mikubwa barani ulaya kwa msimu wa 2017/2018. Nani kucheza na nani Ulaya? Droo ya Klabu Bingwa Ulaya 2017-18 Droo hii ilikua na timu 32 yametoka makundi manane. 

KANDE ZA MPAISHA MTU HUKO KENYA.

Image
Martin Kamotho (Githeriman)  kabla na baada ua kupata msaada.  Picha kwa hisani ya Google.  Maisha hayana maana moja na kila mtu atatoa maana ya maisha kwa vile ambavyo yeye anachukulia ni nini maisha yana maanisha kwake. Na kila siku hua tunasikia watu wakisema "Hakuna kukata tamaa" ni kweli lakini mwingine anajiuliza kwanini nisikate tamaa??  Kila mtu ana jibu lake sasa leo tumepata somo jingine zuri sana kutoka Kenya.

VURUGU ZIMEZUKA KWENYE MAANDAMANO MAREKANI

Image
Waandamanaji wakiwa katika moja ya viunga vya Charlottesville, Virginia.  Mamia ya  wamarekani weupe (wazungu) na wale wanaowapinga walitarajia kufanya maandamano leo jumamosi kwa kile kilichofahamika kama "Unite the Right"(Ungana na mrengo wa kulia)  huko Charlottesville, Virginia

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2017

Image
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).