Sunday, 31 July 2016

JARIBIO LA KUKUONESHA KAMA HUYO ULIYE NAYE ATAKUA MME MZURI KWAKO.

Jaribio muhimu kujua kama kweli atakua mume mwema kwako.
Ndoa ni safari ndefu na ni muhimu kwa watu kuchagua wenza wao wa maisha ili waweze kuishi nao. Kuna maswali muhimu unapaswa kujiuliza kuhusu huyo mme wako wa baadae ili kujua mahusiano yenu yanaweza kwenda mbali kiasi gani. Kuna viashiria vinaweza kukuonesha ni kipi unaweza kukipata baada ya wewe kumkubali huyo uanaemfikiria kua awe mmeo.

Kua makini sana sana kwenye kuchunguza maswali haya na majibu yake yatakupa fursa nzuri ya wewe kupanga maisha yako ya baadae.

1. Je, wanafamilia wako hawampendi?
Kabla hujapanga mipango ya baadae hakikisha kua umajua ni kipi wanafamilia wako wanafikiri kuhusu huyo mmeo. Ni vema(sio lazma) kuwasikiliza wanafamilia wenzio, lakini kama hawamkubali unaweza kuwapa sababu za wewe kumpenda yeye wanaweza kukuelewa na wao kubadili fikra zao.

2. Anapaza sauti(anakukaripia/kufokea)?
Mwanamme yeyote ambaye anapaza sauti/kukaripa pindi mnapotofautiana tu jua kuna uwezekano mkubwa siku moja akakupiga! Asa ukimuona mtu wa hiKama
napaswa kujua kua ni mtu wa jazba.




3. Ana wapenzi wengine anaotoka nao mapenzi.?

 Kama mpenzi wako yuko na waschana wengine anaotoka nao nje ya wewe basi ujue kua uko katika safari ndefu sana ya kimahusiano. Hakuna hakika kama ana uwezo wa kuwaacha wasichana wote hao mara baada ya ndoa. Hivyo kua makini na mtu wa aina hii. Na wakati flani unapaswa kumuuliza ili kujua kati yenu ni nani ni kipaumbele? (Inaweza kua hatari kidogo lakini huna budi kufanya).



4. Unakua wa kwanza kuomba msamaha baada ya kugombana?

 sababu na hitaji kubwa la kuomba msamaha pale inapotokea kuna mgongano kati yenu. Japo, ikiwa kila siku anasubiri wewe uombe msamaha jua hapo kuna tatizo. Kumbuka kuna siku utachoka kusema samahani, je ni nani atakua tayari kusamehe?? Jihadhari na hili. Na hii itakulazimu kuomba msamaha kwa kile ambacho hata huhusiki nacho. Unapaswa kua na mtu atakae heshimu hisia zako pindi mambo yanapoharibika.



5. Je, unalipia mara nyingi zaidi ghara za huduma mbali mbali?

Mnapokua mmetoka out labda au mmeenda mapumziko nani analipa nauli? Bills za vyakula, vinywaji n.k? (Hii isitumike/isichanganywe na uchunaji). Mwanamme wa kweli kuna mda anapaswa kujua kua sasa anapaswa kutoa pesa nje ya ATM au wallet na kulipia baadhi ya huduma! Ukianza kujizoesha kulipia bills zote kabla ya ndoa basi jiandae kulipia bills zote hata baada ya kuolewa.



6. Je, Furaha yenu inakutegemea saana wewe?
Kama huyo mwenza wako kaushikiza tu furaha yake kwako jua hapo kuna tatizo. Watu hawa wanaweza kujiskia ovyo saana kama wewe haupo. Huu ni upendo sio? Inaonekana km ni upendo lakini sio! Akitegemea sana furaha yako anaweza kukuumiza wewe huku akijaribu kujifurahisha. Kua makini na hili ni zuri kiasi ili lina madhara makubwa.



(Itaendelea.....)

No comments:

Post a Comment