Wednesday, 3 August 2016

RAISI AMTEUA MKEWE KUA MGOMBEA MWENZA



Managua. Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega amemtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwingine.

Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhifa maarufu wa msemaji wa Serikali. Amekuwa akionekana katika televisheni ya Nicaragua kila siku
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wamekuwa wakiwakosoa wanandoa hao kwa kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao cha kibinafsi.
Rais Ortega kama hajitokezi kwenye vyombo vya habari basi mkewe huonekana mara kwa mara akijadili sera na kujikuza .
Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo ana uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi. Pia, ana sifa za kuvaa mavazi yenye rangi nyingi na vito vya miaka ya sitini.
Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo wanamuona Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika taifa lake kutokana na hadhi yake katika umma.
Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri wakili wa chama chao cha Sandinista.

No comments:

Post a Comment