7. Hua hatulii kama wewe ukitoka na marafiki zako?
Hili ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Kumuamini mtu ni jambo la msingi sana, na kama mmeo mtarajiwa hawezi kuvumilia piwewe kutoka ukiwa
8. Je, wakati flani anakuruhusu kwenda kushiriki mambo yenu ya kifamilia?
Kama mmeo mtarajiwa anakutaka kuacha kwenda kwenye matukio ya kifamilia jua wazi inawezekana baada ya kuolewa akakuzuia kabisa kuwatembelea hadi ndugu zako. Hata kama ndoa ni jambo muhimu lakini haimaanishi kua familia au ndugu zako wapuuzwe. Kua na mtu ambae maamuzi kuhusu ndugu yatakua na uwiano hivyo ninyi kutoonekana kituko mbele ya ndugu zenu.
9. Hua unafikiria kua wakati flani inaweza kutokea mkaja kuachana?
Kama una mashaka na mtu unayetoka naye kimapenzi jua wazi kuna vitu flani flani ambavyo hujaweza kuvipatia ufumbuzi. Ikitokea humuoni huyo mumeo mtarajiwa kila pale unapojaribu kufikiria kuhusu maisha ya baadae basi jua kuna tatizo.
10. Unasumbuka kujiweka ili uwe kama yule mtu anaempenda?
Kama jibu la swali hili ni ndio basi unapaswa kujiuliza mara mbili au zaidi. Unapaswa kua na mtu ambaye anakufanya ujiskie furaha na huru, mtu ambaye atakubali wewe kua wewe na sio kua kama flani. Ukianza kujifanya kua kama flani mwisho wa siku unaweza kuishia kua kivuli cha wewe mwenyewe.
No comments:
Post a Comment