Posts

TAJIRI WA DUNIA VITANI TENA JUU YA AI. MUSK AZISHTAKI APPLE NA OPEN AI

Image
Picha kwa hisani ya mtandao  Mwishoni mwa wiki iliyopita niliandika kuhusu Open AI kumkaanga Elon Musk na Mark Zuckerberg juu ya kutaka kuiua kampuni chipukizi ya Open AI ambayo inamiliki programu maarufu ya ChatGPT. Na jana Jumatatu tunashuhudia kesi nyingine inayovutia miongoni mwa wataalamu wa kesi za teknolojia kwani tajiri namba moja duniani, Elon Musk amezishtaki kampuni za Apple na Open AI kwa kujimilikisha soko la Akili Unde (AI). Kwa mujibu wa Elon Musk Apple na Open AI ambao wanamiliki 65% ya soko la simu Marekani na 85% ya Chat bot huko Marekani mtawalia wamejimilikisha soko la huduma na kufanya iwe vigumu kwa kampuni nyingine kama vile xAI ambayo inaimiliki Grok kushindwa kushindana katika hali ya usawa. 

DONALD TRUMP KUKUTANA NA KIM JONG UN TENA?

Image
           Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini na Donald Trump wa   Marekani               walipokutana kwenye mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini 2019. Picha na Reuters Korea Kaskazini na Korea Kusini hazijawahi kuaa na mahusiano mazuri kwa historia ya hivi karibu na hilo ni sawa sawa kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Narekani. Korea Kaskazini ni miongoni mwa chache duniani ambazo zimetengwa zaidi na zenyewe zinajitenga na dunia nyingine. Ni nadra kuona mikutano ya kidiplomasia kati ya viongozi wakuu wa Kore Kaskazini na mataifa mengine isipokua China na Urusi. Lakini katika utawala wa Donald Trump alijaribu kukutanaa na Kim Jong Un karibu mara tatu huko Hanoi Vietnam, Singapore na katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea kusini kati ya 2018-2019. Ijapo hakuna kilichotokea baada ya mikutano hii. 

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

Image
Picha ya pamoja ya viongozi wa Ulaya na Rais wa Marekani ikulu ya Marekani tarehe 18 Agosti 2025. Picha na AFP  February 2022 Urusi iliivamia Ukraine kijeshi katika kile ambacho Moscow walikiita kama Operesheni Maalumu  (Special Operation). Na tangu wakati huo vita hio imeendelea na dalili za kukoma kwake bado zinaonekana ziko mbali kulingana na matokeo ya jitihada mbalimbali za kukomesha vita hivyo. Lakini kwa sasa vita vimeingia katika hatua muhimu na huenda ni hatua mbaya sana ambayo kosa kidogo la kimahesabu limaweza kuigharimu dunia kama ilivyokua Julai 1918 au Septemba 1939 ambapo vita vya kwanza na pili vilianza mtawalia. Kwa sasa vita vya Ukraine vina sura ya tofauti ambayo inahatarisha usalama wa dunia. Na haya ndio mambo ya hatari zaidi ambayo yanaweza kushindwa kuzuilika na kuleta vita ya tatu ya dunia.

VITA YA WAJUMBE VS KAMATI KUU YA CCM MWAGA MBOGA, NIMWAGE UGALI. MBUNGE WAKO ULIYEMTARAJIA YUKO SALAMA?

Image
Hatimae mchakato wa kuchuja majina kwa wagombea nafasi ya wagombea katika ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefikia tamati baada ya kamati kuu ya CCM hapo jana kuweza kupitisha majina ya wagombea wake katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyanyika mwezi Oktoba mwaka 2025. Katika mchujo huo kumeshuhudiwa mapinduzi baada ya majina ambayo wajumbe waliyakataa na katika ngazi ya taifa kamati kuu ya CCM yaani (NEC) imewarudisha tena kwa wananchi.  Bofya kwenye maandishi ya bluu (PDF) kusoma zaidi majina ya walioteuliwa kugombea 2025.  Majina ya waliopitishwa na NEC ya CCM kugombea ubunge 2025 Je mbunge wako uliyemtarajia "kaliwa kichwa" na kamati au wajumbe sasa ndiyo wameliwa kichwa? Tungefurahi kupata maoni yako. 

OPEN AI YAMKAANGA ELON MUSK NA MARK ZUCKERBERG HUKO MAHAKAMANI

Image
Sam Altiman muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Open AI. Picha na AFP na Getty Images  Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali nchini Marekani zinaonesha kua kampuni ya Open AI ambayo inamilki ChatGPT imetoa maelezo mahakamani kua tajiri namba moja duniani Elon Musk alijaribu kumshawishi hasimu wake kibiashara Mark Zuckerberg ambae ni mmiliki wa kampuni kubwa ya Meta (Facebook, Instagram, WhatsApp na Thread) ili wachanhiane au waingie ubia katika uwekezaji wa kuinunua Open AI ambapo Elon Musk aliweka dau la dola za kimarekani bilioni 97.4, hata hivyo kulinga na Open AI Zuckerberg hakua ameafiki hilo. 

KAMPUNI YA APPLE IMEISHIWA 'PAWA'. YAOMBA MSAADA KUTOKA GOOGLE

Image
  Picha kwa hisani ya mtandao/ Shutterstock   Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani, Apple Inc ambayo ni kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kielekroniki kama vile simu za iPhone na  Laptop za MacBook wako katika mazungumzo na kampuni kubwa pia ya teknolojia ya Alphabet Inc ambao ndio wamiliki wa Google kuhusu uwezekano wa kampuni ya Google kupewa kandarasi ya kuunda mfumo wa akili unde (AI) wa Apple ambao utakaotumika kuendesha Program ya sauti ya Apple maarufu kama Siri ambayo kwa muda mrefu Apple wamekua wakijaribu kuiboresha lakini hakuna mafanikio makubwa kutokana na vikwazo vya kihandisi katika mfumo huo. Apple yuko nyuma ya Google na Samsung ambao wana programu bora kwa sasa. 

MAJARIBIO YA JESHI LA MAREKANI YAMEENDA NDIVYO SIVYO. HII NI MBAYA SANA.

Image
MAJARIBIO YA JESHI LA WANAMAJI WA MAREKANI LIMEENDA OVYO VIBAYA MNO. SIO DALILI NJEMA. Picha na Petty Officer 2nd Class Clayton/ Us military   Wanasema 'siku njema huonekana  tangu asubuhi 'lakini hii sio kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani. Ikiwa ni miongoni mwa majeshi yenye nguvu zaidi duniani, mara zote hua liko mbele ya muda lakini kwa hiki kilichotokea hivi karibuni kinaacha maswali mengi miongoni mwa wataalam wa kijeshi.  Mwezi uliopita jeshi hilo lilikua likifanya majaribio ya boti zinazojiendesha zenyewe ambapo lengo kuu lilikua ni kua na kweza kua na uwezo wa kulidhibiti jeshi la wanamaji wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limeshuhudia maendeleo makubwa na ya haraka ya kimuundo, silaha na teknolojia. Sasa wakati wa majaribio hyo huko Pwani ya California kulitokea matukio yaliyotilia mashaka uwezo wa Jeshi la Marekani kumudu vita vya kisasa ambavyo vinahitaji teknolojia za kisasa zaidi na hilo tayari limegahrimu kazi za wa...