DONALD TRUMP KUKUTANA NA KIM JONG UN TENA?
![]() |
| Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini na Donald Trump wa Marekani walipokutana kwenye mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini 2019. Picha na Reuters |
Korea Kaskazini na Korea Kusini hazijawahi kuaa na mahusiano mazuri kwa historia ya hivi karibu na hilo ni sawa sawa kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Narekani. Korea Kaskazini ni miongoni mwa chache duniani ambazo zimetengwa zaidi na zenyewe zinajitenga na dunia nyingine. Ni nadra kuona mikutano ya kidiplomasia kati ya viongozi wakuu wa Kore Kaskazini na mataifa mengine isipokua China na Urusi. Lakini katika utawala wa Donald Trump alijaribu kukutanaa na Kim Jong Un karibu mara tatu huko Hanoi Vietnam, Singapore na katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea kusini kati ya 2018-2019. Ijapo hakuna kilichotokea baada ya mikutano hii.
Na sasa tukio kama hilo linatazamiwa katika siku sio nyingi zijazo kufuatia dokezo la Rais mpya wa Korea Kusoni huko Washington leo Jumatatu. Lee ambae tangu kuingia mdarakani mwezi Juni mwaka huu amejaribh kuchuku hatua kadhaa za kupunguza mvutano kati ya majirani hao wawili lakini hatua zake zilikosolewa vikali na kiongozi wa juu wa Korea Kaskazini anbaye pi ni dada wa kiongozi mkuu, Kim Jong Un.
Kufuatia ziara yake ya Washington amesema anatarajia kuona mkutano baina ya Korea hizo mbili unafanyika na Trump ndio mtu pekee ambaye anaweza kufanya hilo likatkea. Hata hivyo Korea Kaskazini imepuulizia mbali taarifa hizo za kukutana kwa viongozi wa nchi hizo mbili. Ikumbukwe kua, Korea Kaskazini imeendelea kujizatiti kujizatiti katika uboreshaji wa silaha zake ili kukabiliana na kitisho cha Marekani. Mazoezi ya pamoja kati ya Korea kusini na Marekani yameendelea kudhoofisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. Na pia, kitendo cha Korea Kaskazini kuendelea kuipa Urusi silaha na wanajeshi kunafanya Washington kua na wasiwasi mkubwa juu ya Korea Kaskazini.

Comments
Post a Comment