MAJARIBIO YA JESHI LA MAREKANI YAMEENDA NDIVYO SIVYO. HII NI MBAYA SANA.

MAJARIBIO YA JESHI LA WANAMAJI WA MAREKANI LIMEENDA OVYO VIBAYA MNO. SIO DALILI NJEMA.







Picha na Petty Officer 2nd Class Clayton/ Us military 


Wanasema 'siku njema huonekana tangu asubuhi 'lakini hii sio kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani. Ikiwa ni miongoni mwa majeshi yenye nguvu zaidi duniani, mara zote hua liko mbele ya muda lakini kwa hiki kilichotokea hivi karibuni kinaacha maswali mengi miongoni mwa wataalam wa kijeshi. 

Mwezi uliopita jeshi hilo lilikua likifanya majaribio ya boti zinazojiendesha zenyewe ambapo lengo kuu lilikua ni kua na kweza kua na uwezo wa kulidhibiti jeshi la wanamaji wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limeshuhudia maendeleo makubwa na ya haraka ya kimuundo, silaha na teknolojia. Sasa wakati wa majaribio hyo huko Pwani ya California kulitokea matukio yaliyotilia mashaka uwezo wa Jeshi la Marekani kumudu vita vya kisasa ambavyo vinahitaji teknolojia za kisasa zaidi na hilo tayari limegahrimu kazi za watu na mikataba ya baadhi ya kampuni zilizoaminiwa kuunda mifumo kwa ajili ya kazi hio. 
Katika tukio moja boti moja ya kivita ilishindwa kufuata maelekezo sahihi kutokana na hitilafu ya 'software' yaani kulitokea software glitch kitu kilihopelekea mtaalam wa mifumo kwenda kurekebisha hilo. Katika hatua nyingine ambapo lilinaswa na kamera na baadae kusambazwa na shirika la habari la Reuters ilionesha droni ya boti inayojiendesha ikienda na kugonga sehemu ya boti nyingine ambayo ilikuepo tu majini na haikua sehemu ya zile zinazofanyiwa majaribio. 

Ikumbukwe kua kumekua na msururu wamatukio ya mifumo ambayo jeshi la Msrekani linaitaka kwaajili ya vita zake za baadae na nchi ya China. Imekua ni ngumu kuweza kupata mfumo thabiti na hii huenda ikawa imechangiwa na kitendo cha kuondolewa mara kwa mara kwa maafisa wa ngazi za juu za jeshi la wanamaji wa Marekani. Kitu hiki hata Pentagon (Wizara ya Ulinzi ya Marekani) wamekua wakishtushwa nacho. Baadhi ya kampuni zilizoingia makubaliano na wizara ya ulinzi kama L3Harris kusitishiwa mkataba. 

Swali kubwa je, Marekani itafikia adhima yake ya kua na jeshi la droni za boti ambazo zitafanya kazi kwa ukamilifu bila kuhitaji msaada wa kibinadamu? Jawabu la hili bado libakia kwa wahandisi wa mifumo na wataalam wa akili unde. 

Taarifa hii kwa hisani ya REUTERS 

https://www.reuters.com/business/aerospace-defense/us-navy-is-building-drone-fleet-take-china-its-not-going-well-2025-08-20/


Comments

Popular posts from this blog

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?