KAMPUNI YA APPLE IMEISHIWA 'PAWA'. YAOMBA MSAADA KUTOKA GOOGLE
![]() |
| Picha kwa hisani ya mtandao/ Shutterstock |
Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani, Apple Inc ambayo ni kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kielekroniki kama vile simu za iPhone na Laptop za MacBook wako katika mazungumzo na kampuni kubwa pia ya teknolojia ya Alphabet Inc ambao ndio wamiliki wa Google kuhusu uwezekano wa kampuni ya Google kupewa kandarasi ya kuunda mfumo wa akili unde (AI) wa Apple ambao utakaotumika kuendesha Program ya sauti ya Apple maarufu kama Siri ambayo kwa muda mrefu Apple wamekua wakijaribu kuiboresha lakini hakuna mafanikio makubwa kutokana na vikwazo vya kihandisi katika mfumo huo. Apple yuko nyuma ya Google na Samsung ambao wana programu bora kwa sasa.
Ikunbukwe kua program ya sauti ya Apple ya Siri ilitakiwa kushindana na Alexa ya Amazon na Google Assistant ya Google. Lakini wakati Amazon Alexa na Google Assistant zimekua na ufanisi mkubwa, Siri imefeli kufikia matarajio ya waundaji na watumiaji na hivyo kuilazimu Apple sasa kufikiria makampuni yaliyofanikiwa katika teknolojia hiyo ili kuisaidia kurudi katika ubora unaohitajika. Hata hivyo bado Apple hawajafanya masmuzi ya mwisho juu ya hilo. Ikiwa ni vigumu sana kwa wao kuunda Siri basi itakua ni bora kutafuta kampuni ya nje na Apple kufanya kazi hiyo. Kwa huenda Siri ikapata usaidizi wa Gemini AI kutoka Alphabet Inc/Google.
Apple walitoa ahadi mwaka jana kua program ya sauti ya Siri ingekua tayari hivi punde na watumiaji wa iPhone wangeweza kuisanikisha katika vifaa vyao. Lakini hiyo punde imekua si punde tena kwani ni mwaka sasa na hakuna dalili za kwamba Siri inakuja katika simu za iPhone. Hata toleo lao jipya linalotazamiwa kutoka tarehe 9.09.2025 huenda kusishuhudiwe Siri iliyoboreshwa ikitangazwa katika bidhaa hizo. Na ifahamike kua Google walitumia tatizo la Apple kushindwa kutoa programu ya Siri kama mtaji wa soko ambapo waliidhihaki Apple katika kipande cha tangazo la mapema kuelekea uzinfduzi wa Google Pixel 10, kwamba ikiwa unaahidiwa kua kitu kitakujia hivi punde na hiyo punde haifiki kwanini usiache kusubiri na ununue simu nyingine. Walikua wamelenda toleo la iPhone 16 ambalo llilotoka September 9, 2024 na Siri haijawahi kufika.
Kufuatia habari hizo za Apple kuitafuta Google kujadiliana kuhusu hilo kumefanya hisa za kampuni ya Apple jana Ijumaa kuongezeka kwa 1.6% huku zile za Alphabet Inc zikiongezeka kwa 3.7%. Hata hivyo, kampuni zote mbili zilipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hizo hazikuweza kutoa maoni yoyote kwa mujibu wa Bloomberg na Reuters.
Sehemu ya taarifa hii ni kutoka Reuters.
Imeandikwa na kuhaririwa na
Erick Jerry
karlrck@gmail.com
.jpeg)
Comments
Post a Comment