TAJIRI WA DUNIA VITANI TENA JUU YA AI. MUSK AZISHTAKI APPLE NA OPEN AI
Picha kwa hisani ya mtandao
Mwishoni mwa wiki iliyopita niliandika kuhusu Open AI kumkaanga Elon Musk na Mark Zuckerberg juu ya kutaka kuiua kampuni chipukizi ya Open AI ambayo inamiliki programu maarufu ya ChatGPT. Na jana Jumatatu tunashuhudia kesi nyingine inayovutia miongoni mwa wataalamu wa kesi za teknolojia kwani tajiri namba moja duniani, Elon Musk amezishtaki kampuni za Apple na Open AI kwa kujimilikisha soko la Akili Unde (AI). Kwa mujibu wa Elon Musk Apple na Open AI ambao wanamiliki 65% ya soko la simu Marekani na 85% ya Chat bot huko Marekani mtawalia wamejimilikisha soko la huduma na kufanya iwe vigumu kwa kampuni nyingine kama vile xAI ambayo inaimiliki Grok kushindwa kushindana katika hali ya usawa.
Kesi hio ina mvuto wa kipekee kwani Elon Musk ameendelea kuiandama tena Open AI ambayo alishiriki kuianzisha na baadae kuamua kuachana nayo na sasa anaitaka tena. Hata hivyo, Open AI imeendelea kusema kesi hio ni muendelezo wa Elon Musk kuendelea kuishurutisha kampuni hiyo na kwamba wao hawajafanya kitu cha kuvunja sheria.
Karltika majibu ya awali ya Apple walisema kua kampuni hio haifanyi ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote ile kupitia App Store. Licha ya Trump kusema kua App Store haiioneshi Grok kua juu ya ChatGPT licha ya Grok kua na wastani wa ukadiriwaji wa utendaji wa kufikia nyota 4.9/5.
Tambua kua Apple na Open AI wameingia katika makubaliano ambayo yanaifanya ChatGPT kuweza kua kuunganishwa na vifaa vya Apple kama vile simu za iPhone, MacBooks na iPads. Kw mtazamo wa kisoko ni kwamba Apple ndiye muuzaji wa simu Marekani na hivyo basi kuunganishwa na ChatGPT kutaifanya kua na watumiaji wengi zaidi Marekani wakati huo huo ChatGPT itakua imepata wateja wa lazima wa Apple kirahisi maana yake Marekani watubwatakua wakitumia zaidi ChatGPT zaidi kuliko AI Chat bot nyinginezo. Ili kuleta uwiano wa kisoko huenda Apple wakalazimishwa kufanya mabadiliko katika upangiliaji wa programu za akili unde katika Apple Strore.
Endapo kesi hii itaamuliwa maana yake itakua ni kipimo kwa mahakama kuweza kua na tafsiri ya sheria kuhusu Akili Unde na mipaka yake. Na hili ndilo linaowavutia wengi kwamba ni nink hasa kitaamuliwa na hapa inaweza kua ni mwanzo wa msusuru wa kesi nyingi sana kuhisiana na Akili Unde. Mpaka hapo kesi itapoamuliwa kwa sasa tunaendelea kusema AI imekua ni keki ya moto miongoni mwa wadau wakubwa wa teknolojia na hakuna anaetaka kukosa fursa hio.

Comments
Post a Comment