OPEN AI YAMKAANGA ELON MUSK NA MARK ZUCKERBERG HUKO MAHAKAMANI



Sam Altiman muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Open AI. Picha na AFP na Getty Images 

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali nchini Marekani zinaonesha kua kampuni ya Open AI ambayo inamilki ChatGPT imetoa maelezo mahakamani kua tajiri namba moja duniani Elon Musk alijaribu kumshawishi hasimu wake kibiashara Mark Zuckerberg ambae ni mmiliki wa kampuni kubwa ya Meta (Facebook, Instagram, WhatsApp na Thread) ili wachanhiane au waingie ubia katika uwekezaji wa kuinunua Open AI ambapo Elon Musk aliweka dau la dola za kimarekani bilioni 97.4, hata hivyo kulinga na Open AI Zuckerberg hakua ameafiki hilo. 

Open AI walimshitaki Elon Musk kua kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na kupitia kutangaza zabuni ya kununua Open AI au bidhaa zake kulilenga kuiua kampuni hiyo ndogo iliyojikita katika kuendeleza Akili Unde (AI). Open AI ilimuomba Jaji wa Serikali Kuu kuiamuru Meta kutoa nyaraka na mawasiliano yake yanayohusiana kwa namna yoyote na zabuni ya kutaka kuinunua Open AI.  

"Mawasiliano ya Meta na wazabuni wengine, au mawasiliano ya ndani, ikiwa ni pamoja na yale yanayoakisi majadiliano na Musk au wazabuni wengine, pia yatatoa mwanga juu ya lengo halisi la zabuni," OpenAI ilisema, ikiita Musk na Meta kuwa washindani wake wawili muhimu.

Meta, katika shauri hilo hilo la mahakama, ilisema OpenAI inapaswa kutafuta hati au nyaraka zozote muhimu moja kwa moja kutoka kwa Musk na  kampuni ya yake ya AI inayochipukia (Start-up ) ikimaanisha xAI na ilimtaka jaji kukataa ombi la OpenAI. Kesi hiyo imeahirishwa hadi baadaye 2026 itakapo tajwa tena. 

Ikumbukwe kua Elon Musk aliwahi kua miongoni mwa wafadhili waanzilishi wa Open AI mwaka 2015 lakini alichana nayo muda mfupi baadaye kwa madai ya kushindwa kuafikiana na uongozi na mwenendo wa kampuni. Madai ambayo Open AI inapinga inasema Elon Musk alitaka kuifanya Open AI kua ya kibiashara kinyume na msingi wa uanzishwaji wake. Open AI wanadai Musk alitaka kuifungamanisha na kampuni ya yake ya Tesla. Walipokataa akaamua kujitoa na mwaka 2020 akaanzisha kampuni yake ya xAI ili kushindana na Open AI. Lakini kwa sasa natafuta kumiliki teknolojia ya Aikili Unde na hivyo anapambana kuiangusha Open AI kwa njia yoyote ile kitubambacho Sam Altiman anadhani hilo haliwezekani kutokea. 

Ila Meta na xAI wote wanamuogopa Open AI ukiangalia jinsi ushindani unavyokwenda ni kwamba ChatGPT mwa mfano kwa sasa ni miongoni mwa Chat bot inayotumika sana duniani. Simu na kompyuta baadhi zinakuja zikiwa na ChatGPT ndani kwa hio inapata watumiaji wengi na kwa kasi sana. Hii ndio sababu Meta imelazimisha Meta AI katika programu zake tumizi hasa WhatsApp. Vita za makampuni makubwa hasara kwa watumiaji tuendelee kua makini sana. 

Imeandikwa na kuhaririwa na 

Erick Jerry 

karlrck@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?