Tuesday, 12 July 2016

MARAISI WA ZAMANI KUSUSIA KONGAMANO KUU LA CHAMA CHA REPUBLICAN

BUSH Snr na Jr, Mitt Romney Kutohudhuria kongamano la chama cha Republican litakalo fanyika mwezi huu.


Nchini marekani makongamano(Mikutano mikuu) ya vyama hufanyika kila baada ya miaka minne ambapo wajumbe humchagua mtu mmoja kua mgombea wao wa uraisi. Kongamano hili huhudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo waandishi wa habari kutoka mashirika mbali mbali duniani. Kila kongamano husimamiwa na kamati kuu ya chama cha Republican na Democrat. Kongamano hili pia huhusisha hotuba za viongozi marufu wa vyama husika. Mgombea mwenza(makamu wa raisi) huchaguliwa kabla ya kongamano kuu na yeye hutoa hotuba yake. Licha ya tofauti ndogo ndogo lakini makongamano ya vyama vyote yanatarajiwa kupitisha majina ya sasa ya wagombea wa kiti cha uraisi, Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat ambao wote wamefanya vizuri katika chaguzi za awali katika majimbo.

Republican watafanya Kongamano lao kuanzia tarehe 18-21 July 2016 wakati Democrats watafanya kuanzia tarehe 25-28 July 2016.

Lakini maraisi wa zamani wa Republican George Bush Snr na George Bush Jr na aliyekua mgombea wa uraisi kupitia Republican mwaka 2012 Mitt Romney wamesema hawatashiriki kongomano hilo kwa kua wakiwa hawakubaliani na sera za mgombea wao Donald Trump.

No comments:

Post a Comment