Wagombea wawili wa chama cha Democrat nchini Marekani, Ben Sander na Hillary Clinton wanatarajiwa kuungana pamoja kwa kile kinachoonekana ni kujaribu kuunganisha nguvu ya chama chao dhidi ya Republican.
Mahasimu hao wa kisiasa waliochuana vikali kwenye kura za awali za majimbo kuwania kugombea nafasi ya uraisi wa marekani kupitia Democrat kwa kwa sasa wanataka kumaliza uhasama wao kwa kuungana pamoja. Haikuwa hatua rahisi na iliyokuja mapema lakini leo hii jumanne wawili hao wanategemewa kuonekana kwa pamoja huko New Hampshire, Marekani.
Clinton anajaribu kuwapata wafuasi wa Sanders aliowapata kipindi cha kura za awali ili kumshinda mpinzani wake Donald Trump wa chama cha Republican. Sanders ambaye alijipambanua kama mjamaa kwenye chama cha Democrat alipata wafuasi wengi hasa vijana kipindi cha kura za awali. Muungano huu kati ya Sanders na Clinton utaenda kutuliza hali ya kisiasa ndani ya Democrat kwani kwa sasa kulikua na wasiwasi huenda labda Sanders angesimama mwenyewe au asiweze kumuunga mkono Clinton. Wafuasi wengi wa Clinton wanaamini Sanders atakua ngao muhimu dhidi ya Trump.
No comments:
Post a Comment