BAADA YA MIAKA 113 KANISA LAHAMISHWA BILA KUVUNJWA.
Kanisa la Lutheran la Kiruna huko Sweeden likiwa tayari kusafirishwa. Picha kwa hisani ya ForbesKatika hali ambayo sio ya kawaida kanisa moja la kihistoria huko nchini Sweeden limehamishwa kutoka sehemu mabo lilijengwa na kupelekwa sehemu nyingine baada ya miaka 113 la kuwepo katika eneo ambapo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1912. Kuhamishwa kwa kanisa hilo la Lutheran ni kutokana na kuwepo kwa uchimbaji wa madini ya chuma chini ya kanisa hilo na maeneo mengine ya jirani. Mpango wa kuhamisha kanisa hilo bila kubomoa umekua ukiendelea kwa takribani mwaka mmoja ambapo wataalam wamekiri kwamba haikua kazi rahisi.Kanisa hilo lenye uzito wa takribani tani 741 na urefu wa karibu mita 40 hivi lilipakiwa kwenye gari maalum lenye jumla ya tairi 32 na kulisafirisha umbali wa karibia kilometa 5 hivi ambapo zilitumika siku mbili kutembea umbali huo kutoka eneo la awali mpka katika 'makazi mapya' ya kanisa hilo katika mji wa Kiruna ulioko Kaskazini mwa nchi hio. Kutokana na ukubwa na muundo wa mzigo huo, barabara zililazimika kupanuliwa upya na vizuizi kuondolewa. Mwendo wa gari ilikua ni 0.5km kwa saa zima.Tukio hilo la kihistoria lilihudhuriwa na umati wa karibu watu 10,000 waliokua wana hisia na maoni tofauti juu ya kuhamishwa kwa kanisa hilo kongwe na zuri nchini Sweeden. Baadhi walisifu kwamba kuhamishwa kwa kanisa hilo ni jambo jema kwani ni kulinda historia na urithi wa mji wa Kiruna lakini pia upande mwingine unaonesha athari za uchimbaji wa madini kwa jamii ambazo zinazunguka maeneo ya migodi. Mji huo wa Kiruna ambao una takribani ya wakazi 6000 hivi unatarajiwa kuhamishwa wote kwa takribani kipindi cha miongo miwili ijayo ili kupisha uchimbaji wa madini.Kanisa la Kiruna likiwa kwenye gari maalum la kubeba mizigo mikubwa. Picha na ForbesLicha ya kua majengo mengi katika mji huo yalibomolewa na kujengwa upya katika mji mpya kuna machache waliamua kuyasafurisha kama yalivyo ikiwemo kanisa hili la kihistoria. Baada ya kufika katika 'makazi mapya' litatakiwa kuweza kuzungushwa ili milango yake itazame sehemu jamii ilipo na kifanyiwa marekebisho ya msingi. Kanisa hilo linatarajiwa kufungua milango yake kwa waumini wake mwishoni mwa mwaka 2026.
Imeandikwa na kuhaririwa na
Erick Jerry
karlrck@gmail.com

.jpg)
Comments
Post a Comment