Justin Bieber ambaye ni star aliyeanza muziki akiwa na umri mdogo na mpaka sasa anafanya vizuri katika game ameingia kwenye headlines baada ya kufuta account yake ya Instagram ambayo ilikuwa na followers milioni
77.8 .
Kisa kimeanzia pale Justin Bieber alipokuwa anapost picha na msichana ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Lione Richie mwanamitindo Sofia Richie mwenye umri wa miaka 17 ambapo ameonekana akiwa na Justin bieber kwenye mitoko mingi hivi karibuni.
Baada ya Justin Bieber kupost picha akiwa na msichana huyo mashabiki wake wamekuwa wakicomment maneno yalioonesha yana chuki na nia ya kutopendezwa na Justin kuwa karibu na msichana huyo, maneno yalizidi na msanii huyo kuamua kupost picha na kuandika maneno haya …
>>>’Nitaifanya account yangu iwe private kama hamtaacha chuki, kama nyie kweli ni mashabiki zangu hamuwezi kuchukia watu ninaowapenda mimi ‘
Mkasa ukazidi pale mwanamuziki Selena Gomez ambae ni Ex wake Justin kupost picha na kuandika maneno yaliomlenga Justin Bieber na kuandika hivi …….>>>’ Kama huwezi kuvumilia chuki acha kumpost girlfriend wako, wekeni iwe muhimu kwenu wawili tu usikasirikie mashabiki wako wanakupenda na walikuwa na wewe kabla ya mtu yeyote yule ‘
Na baada ya majibizano katika comments Justin na Ex wake, Justin amechukuwa maamuzi ya kufuta istagram account yake na kwa sasa imebaki facebook na twitter yake tu.
No comments:
Post a Comment