SHETANI ALIANZA LINI KUA SHETANI?
Hakika sifuri(0) sio sawa na o. Sifuri ni tarakimu lakini o ni herufi. Sifuri na o zinataka kufanana lakini hakuna hata siku moja sifuri iwe o na o iwe sifuri. Huo uwezekano haupo. O itabaki kua O na 0 itabaki kua 0. Wakati fulani tumekua na mazoea ya kutaka kulazimisha vitu vinavyofanana viwe sawasawa. Kufanana hakuna maana ni sawa sawa.
Tukirejea katika biblia tunaona kua wakati flani huyu ambaye tunamuita shetani hakuepo duniani, alikuepo mbinguni ambako ndiko makao makuu ya Mungu. Alikua ni malaika wa Mungu, tena alikua malaika mkuu akipiga vinanda, kusifu n.k. Huyu alikua ni malaika;Kiumbe safi haswa...!! Lakini baadae kwa kua alipewa sifa nyingi huyu Lucifer (Shetani) alipagawa, akalewa sifa akajiona yeye kule mbinguninni bora kuliko wengine wote! Aliona yeye ndio kila kitu... Lakini alisahau kama kule mbinguni kuna MUNGU mmoja ambaye nafasi yake haichukuliwi na yeyote. Akafanya mchezo wa kumjaribu Mungu, lakini Mungu hajaribiwi... Alimuadhibu Lucifer kule mbinguni na kumtupa duniani!! Yes! Mungu aliionesha ukuu wake kwa kua tayari Lucifer alikwenda kinyume naapenzi yake. Na hapo ndipo Lucifer akawa ni shetani na sio malaika.
Tuchukue mbingu tuishushe duniani. Kuna watawala mwanzo walikua ni malaika;watu safi walokubalika machoni pa watu. Wakapendwa, wakasifiwa, ikawa imewapendeza sana. Lakini wamelifanya na au wanafanya makosa ambayo Lucifer aliyafanya. Wamejitwika sifa, wametengeneza kata ya ushindi daima wakiamini wao ni bora kuliko mwingne awaye. Lakini kumbuka yeyote ajikwezaye hushushwa tena kwa aibu kama ilivyokua kwa Lucifer. Kila mwanadamu ana udhaifu na inapendeza kua na udhaifu huo ili sote tukubaliane kushirikiana. Inakuaje sasa tunajivika U-mungu mtu? We ni nani hasa kila neno lako liwe ni sheria?/ Ni nani alokutuma kunena kinyume na walokutuma? Ama kweli aloshiba hamkumbuki mwenye njaa. Gautama Budha alisema "tuwazavyo ndivyo tutakavyokua" na biblia inatwambia "awazavyo mtu ndivyo alivyo". Swali langu ni je hivi ni kweli tunawaza?? Kama mawazo yetu ndio 'blueprint' ya matendo yetu je tunawaza/? Tunawaza nini? Tunachokitenda ndicho tunachokiwaza? Watu wanaongea ambacho hawajawaza mwishowe badala ya kua wasemaji wanakua waropokaji na wapwayukaji. Hii ni hatari hasa kiongozi unapokua mtu usiyejua kuchagua neno. Neno lako linaweza kua ni UKUTA wa kuwatenganisha watu au likawa ni DARAJA la kuwaunganisha watu. Sasa kiongozi unapokua ni UKUTA tayari wewe ni tatizo. Lugha ya matusi itawagawa werevu na waadilifu, lugha ya vitisho itawagawa wanyonge dhidi ya jeuri, lugha ya kejeli itawagawa wambew na wafedhuli...! Ila lugha ikiwa ya staha itawaunganisha waliogawanyika! Unakumbuka lugha ndio ilitosababisha kushindwa kukamilika kwa mnarà wa Babel?? Jifunze matumizi bora ya ulimi wako.
Haijalishi ni mtu wa aina gani isijifanye wewe unaweza kukaa juu ya sindano. Na ukitaka kutembea juu ya maji hakikisha ile kanuni ya kitu kuelea(Law of floatation) inafuatwa.
Sasa najiuliza kama watawala wetu wanaweza kuiepuka adhabu yao kwa kile wanacho/walichokitenda na gharama za kuzima dhamira safi ni ushetani. Shetani ni mtumikishaji, mkandamizaji, mnyonyaji, mlaghai, je watawala wetu hawaoni sababu ya kujihoji wenyewe? Ni mailaika au shetani?
Malaika ni mlinzi na "mtumwa wa Mungu" kwani hutoa taarifa zetu za kila siku. Sasa tangu lini shetani akamlinda binadamu? Unategemea shetani akuokoe?? Hapana labda akutembeze kwenye ziwa la moto. Atakuahidi raha ila kuifikia ni lazma ujitoe kafara bila kujua kama umejiweka kafara mwenyewe. Shetani hana huruma (Ushawahi kuona katuni ikimuonesha shetani akionesha tabasamu la kweli?)
Licha ya raha zote anazokuahidi lakini nyuma ya kila ahadi kuna kimiminika cha machozi, jasho na damu ya wasio na hatia. Ila kwa kutimiza adhma yake ya kishetani hulazimika kufanya hayo. Bila kujali nani anajali kua kuna angamio la wasio na hatia. Tungali tuna akina Lucifer wengi je ni nani atamtupa Lucifer duniani?
Ni jukumu lako wewe na mimi kuijenga mbingu mpya na dunia mpya√.
No comments:
Post a Comment