Usain Bolt akiwa na mama yake wakishangilia moja ya ushindi wake.
MAMA YAKE USAIN BOLT AMTAKA MWANAE KUOA.
Usain Bolt ameweka historiabya kua mwanariadha pekee aliyeshinda medali tatu za dhahabu katika mashindano ya Olympic kwenye mbio za mita 100. Licha ya mafanikio haya makubwa ya usain Bolt mama yake mzazi amemtaka mwanae kuanza kutafuta mwanamke baada ya kuhitimisha maswala ya mbio. "Natumaini atatulia na kuoa" alisema mama yake Bolt kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Akiongea kwenye mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha CNN Jenifer Bolt, ambaye ni mama mzazi wa Usain Bolt alisema kua yuko tayari mwanae kumpatia mjukuu mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Olympics yanayoendelea huko Rio nchini Brazil. "Nina matumaini kua atatulia, ataoa na kuanzisha familia yake", alisema Jenifer Bolt. "Najua atatulia kwasababu alisema hilo. Ameniambia mara nyingi kua ataanzisha familia yake".
No comments:
Post a Comment