HATARI YA "AI" YA ELON MUSK: IMETOA SIRI JINSI YA KUMUUA BOSS WAKE ELON MUSK

Picha kwa hisani ya mtandao/ Nacional.hr

Kitu kikubwa kinachozungumzwa kwa sasa katika Ulimwengu wa teknolojia ni Akili unde au Akili mnemba maarufu kama Artificial Intelligence (AI). Makampuni makubwa kama Alphabet Inc. (Google) ,wana AI yao ambaayo ni Gemin AI, Microsoft wana Copilot, Open AI wana ChatGPT, xAI wana Grok, Meta wana Meta AI na pia kuna Deep Seek kutoka China. Kwa sasa biashara kubwa ni AI. Hakuna kampuni imekua ikitaka kua nyuma katika hili. Lakini kuna jambo moja kubwa la kitisha ambalo bado watumiaji hatuweza kuwekwa wazi juu ya dhamira halisi ya hizi akili unde na wengi wanatumia kwasabau zipo bila tahadhari. Lakini hivi majuzi kumeshuhudiwa mambo ya hatari ambayo Akili Unde imeweza kujaribu kufanya. 

Grok ni AI ambayo imetengenezwa na xAI na inatumika katika mtandao wa X zamani Twitter unaomilikiwa na bilionea namba moja duniani, Elon Musk. Mara kadhaa Elon Musk amesem Grok ilikua ni AI bora sana na yenye kufuata maadili. Lakini hili linaonekana liko mbalima ukweli kulingana na taarifa ambazo Forbes wamezifangia kazi na kuzichapisha. 


Kwanza Grok ilikua ukitafuta kitu na kubonyeza kiungo (link) ya kushirikisha (share) ni kwamba kile ambacho wewe ume 'chati' na hio AI kinachapisha kwa siryi bila wewe kua na taarifa katika wavuti wa xAI ambapo sasa yote uliyoyafanya yanaweza kuonekana katika "Search Engine" kama vile Google, Bing na DuckduckGo. Kwa hio mazungumzo yako na hizo AI chat bot yanaweza kutazamwa na mtu yoyote ambaye ametafuta kupitia Google labda. 

Kulingana na takwimu zilizopo ni kua Google wamefanikiwa kuhifadhi zaidi ya mazungumzo 370,000 kutoka kwa watumiaji mbalimbali. Na humo kuna taarifa za dawa, watu kuomba ushauri wa kitabibu, namna ya kuweza kujidhuru kwa mfano kujiua, namna ya kutengeneza madawa kama Fentanyl na namna ya kutengeneza mabomu au vilipuzi. Mambo mengine yamekiuka kile ambacho watengenezaji wake wanaita kutokua taarifa ambazo zinaweza kua na mdhara kwa bidamu kama taarifa za mdawa haramu, silaha za kibaolojia, kikemikali na zile za maangamizi. Kwa hio mfumo wao haufuati kile watengenezaji walitaka iwe nia u kwa bahati mbaya au makusudi. 


Na katika hali ya kushangaza zaidi ni kwamba Grok AI ilitoa maelezo ya kina jinsi ya kuweza kumuua mmiliki wa xAI ambaye pi ndio tajiri namba moja duniani, Elon Musk. Yaani Grok ambayo inamilikiwa na Elon Musk mpango madhubuti wa kuweza kumuua Elon Musk ambaye pia ndio boss wake. Jambo hili bado linafikrisha sana na kwamba taarifa kama hizo zilikua zinaweza kupatikana kwa kuzitafuta tu Google. Ni hatari kubwa mno. Lakini hadi naandika taarifa hii Forbes walikua hawajachapisha maelezo hayo ya Grok ambayo waliyapata Google na xAI walikua hawajaweza kuwajibu Forbes walipotaka ufafanuzi wa kina juu ya hayo yaliyotokea. 


Hivyo basi, wakati AI ina nafasi kubwa ya kuchochea maendeleo, ni vyema kukumbuka kwamba inaweza kua na mapungufu kwa hio ni vema kua na tahadhari wakati wa kutumia AI. Miongoni mwa yale unaweza kuyafanya ni kutokuweka au kujadiliana mambo yako ya siri sana na AI kwa sababu Grok iliweza kutoa hadi nywila (password) ya mtumiaji mmoja. Lakini pia taarifa za utambulisho wako wote basi usiamini zikae na AI kwani siku inaweza kuiba utambulisho wako na kufanya jambo ambalo itakua ni ngumu au utakua umechelewa pindi utapojaribu kumuaminisha kila mtu kwamba sio wewe au wewe hukuhusika. Na mwisho tumia AI kwa ajili ya kutafuta vitu chanya pekee. 


Imeansikwa na

Erick Jerry 

karlrck@gmail.com 


Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?