Kutoka kushoto ni Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Layen, waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Finland Alexander Stubb, Rais wa Ukraine Volodymr Zelenisky, Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, waziri mkuu wa Italia Giorgina Meloni, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na katibu mkuu wa NATO Mark Rutte .
Huenda siku ya Jumatatu 18, 2025 ikawa miongoni mwa siku kubwa kabisa katika siasa za kimataifa na diplomasia. Misukosuko ya Ulaya inawaleta viongozi wa nchi kubwa za Ulaya pamoja na Ukraine nchini Marekani na wote wakisubiri kwa hamu kuweza kusikia kile ambacho Rais wa Marekani Donald Trump alikua akitazamia kuamua juu ya hatma ya vita vya Ukraine na zaidi ya yote juu ya hatma ya Ulaya na NATO. Mgogoro wa Ukraine ni mgogoro mbaya zaidi kwa Ulaya tangu kuisha kwa vita baridi mnano 1991. Wangeliweza kukaa na kusubiri Volodymr Zelenisky na Trump wajadiliane na wapewe mrejesho lakini kamwe hilo halikuonekana kutokea kwani wote walihofia kwamba Volodymr Zelenisky angeweza kufanyiwa kile ambacho kilitokea katika Oval Office mwezi Februari 2025. Walimsindikiza ili kua na ushawishi wa pamoja juu ya Ukraine wakionesha kwamba vita nchini Ukraine inaweza kuisha tu kwa wao kua na nguvu na kumlazimisha Putin kufikia makubaliano ya amani. Sasa hiki kitu chanza Putin hakimfurahishi anataka kuona Ulaya wenye mpasuko mkubwa. Ila ukitazama waliohudhuria ni watu wenye ushawishi kwa Rais Trump. Mfano ni uwepo wa Rais wa Finland Alexander Stubb, huyu sio kwamba nchi ya Finland ni kubbwa la! Ila ameenda lwa sababu ana ushawishi binafsi na wa karibu na Trump. Wengi hawakuelewa kwanini alikuepo pale lakini alienda kuongeza ushawishi wa kundi hilo la viongozi wa Ulaya kwa Donald Trump.
Kuonesha umoja na mshikamano wa nchi za Ulaya juu ya maslahi ya Ukraine linaonekana kua lina nafasi kiasi flani walau kwa sasa. Kila kiongozi wa Ulaya alipofika kwa Trump alimwagia sifa kwa sababu kama nilivyoeleza katika makala zilizopita hicho ni kitu ambacho Trump anakipenda sana. Rais Macron wa Ufaransa alisema "nilimpenda tangu siku ya kwanza, na sasa nampenda hata zaidi", Mark Rutte yeye alisema Trump "ni kiongozi mkuu" wa Ulaya huku Keir Starmer alisema "kila mtu anampenda, sote tunampenda". Unaweza kuona lengo la viongozi wa Ulaya ilikua ni kumfanya Trump ajione sasa ana nguvu na mamlaka ya kufanya maamuzi mazito kwaajili yao. Hata hivyo baada ya mjadala mambo kadhaa yalionekana ni dhahiri na huenda mengine yakamtia Putin kitanzini. Hata hivyo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipendekeza duru ya nyingine ya mazungumzo yamhusishe Putin. Kumbuka viongozi wa Ulaya walimtenga Putin kwamba hawawezi kuongea nae. Kama hili litatokea, Putin atakua kawapiga tobo kubwa na itakua fedheha kwa Ulaya. Lakini tutazame mambo yanayoweza kumkaba kooni Rais Putin wa Urusi.
Jambo la kwanza ni mpango wa Marekani na Ulaya kupeleka wanajeshi katika ardhi huko Ukraine. Donald Trump amesema kua swala la usalama na ulinzi wa Ukraine litakua kwanza la nchi za Ulaya ambazo ziko karibu lakini akasema Marekani itatoa msaada wowote unaohitajika ili kuifanya Ukraine kua salama kutoka kwenye mashambulizi ya baadaye ya Urusi. Hili swala Urusi kupitia kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje wamelipinga wazo hilo kwamba Urusi haitoruhusu wanajeshi wa NATO nchini Ukraine na huu ndio msimamo wa Putin tangu mwanzo. Katika mazungumzo yake Volodmyr Zelenisky amesema garantii ya usalama wa Ukraine itahitajika watu, silaha, mafunzo, misheni na watalaamu mbalimbali. Kwa msingi huo wanahitaji silaha zaidi, wakufunzi wa kijeshi na ushiriki wa Ukraine katika mafunzo ya kijeshi kama ambavyo mataifa ya NATO hufanya. Na wazo hili ndilo ambalo waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer amekua akipendekeza. Na Rais Trump alipoulizwa endapo atapeleka wanajeshi wa Marekani huko Ukraine zaidi ya mara tatu hakuweza kukataa moja kwa moja uwezekano huo. Kwa hio wazo hilo linaweza kua linafikiriwa zaidi. Na ikiwa hili likapita leo huko Washington sijui Putin atakuja na nini hasa. Uwepo wa wanajeshi wa NATO Ukraine bado utakua ni hatari kwa ulinzi na usalama wa Urusi. Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi wanaona huu ni moja ya uchokozi wa nchi za magharibi na hasa ukienezwa na Uingereza.
Jambo la pili lilikua ni swala lililoibuliwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer kwa kusema kwamba usitishaji wa mapigano ni hatua muhimu na ya kwanza ili kuwendelea na mazungumzo ya amani. Kumbuka walipokutana Alaska, Rais Trump na Putin walisema wazi kwamba wanahitaji suluhisho la kudumu la kumaliza vita na sio usitishaji wa mapigano. Na hili lilikua ni wazo la Rais Putin kwamba hakuna usitishaji wa vita bali kumaliza vita. Ila leo viongozi hao wa Ulaya wansema lazima kuwe na usitishaji wa mapigano kwanza. Sasa ni namna gani hili lonawezekana itakua ni juu ya Putin kuamua au la kuboresha wazo hili. Swali la msingi itakua ni lini sasa watafikia makubaliano hayo wakati huo huo Putin ameshatakaa kukutana na Zelenisky katika hatua za mwanzo hivi anataka wakikutana tayari wawe wanakubaliana mkataba wa kumaliza vita sio kujadili tena. Kulingana na Bild gazeti moja huko Ujerumani limeripoti kua mazungumzo yalisitishwa kwa muda ili Trump ampigie simu Rais Putin na kwamba mkutano ungeengelea baadae kidogo baada ya simu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya Trump kupitia mtandao wake wa Truth amesema mkutano huo ulikua "mzuri sana" na kwamba alimpigia simu Putin kumuelexa kile walichokijadili. Kwa hio kwa sasa linasubiriwa jibu la Putin juu ya uwezekano wa kuwepo kwa majadiliano ya watu watatu yaani Putin, Trump na Zelenisky
Ikiwa mambo hayo yatapitishwa kwa namna ambavyo yapo yanaweza kua kikwazo kupata amni ya kudumu kwani Putin atayakataa na kuendelea na vita kwa sababu kwa mujibu wa taarifa ya Trump kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya ni kwamba Urusi bado inapambana kulichukua eneo la Donbas licha ya kwamba Ukraine pia bado wangali na udhibiti kiasi katika eneo hilo. Na labda sasa mkutano wa njia tatu kwa maana ya Ukraine na au Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi unaweza kuamua ni mambo gani haswa yabaapaswa kujadiliwa na marais wa nchi zinazogombana. Kwa hio labda hilo litaweza kutokea katika muda wa wiki moja au mbili hivi kwa mujibu wa Trump.
Lakini kwa yale yaliyojitokeza yanaweza kumaanisha kwamba Trump ana ng'ata na kupuliza pande zote mbili ila sasa Putin sio mtu wa kukurupuka katika maamuzi na ukweli ni kwamba hataki kukutana na Zelenisky peke ake kwasababu anadhani kua Zelenisky ni Rais asiye na uhalali wa kua Rais wa Ukraine na pia Trump aliligusia katika halinya utani jana huko White House. Kwa vyovyote vile bado Putin hawezi kua amefurahishwa na waliyojiri Washington DC.
Maeneo ya Ukraine yanatawaliwa na Urusi. Ramani kwa hisani ya Reuters
Imeandaliwa na;
Erick Jerry karlrck@gmail.com
|
Comments
Post a Comment