WANAJESHI WA URUSI WAPEPERUSHA BENDERA YA MAREKANI KWENYE MSTARI WA MAPAMBANO HUKO UKRAINE
Dunia inastaajabisha sana na wakati flani matukio kadhaa yanaweza kuonekana kama mchezo wa kuigiza au mzaha lakini baadae hugeuka kua ni maisha halisi ya baadhi watu. Katika kisa kimoja cha kushangaza sana imetokea huko katika mstari wa mbele wa mapambano kati ya majeshi ya Ukraine na majeshi ya Urusi ambapo kifaru cha Marekani Armoured Personnel Carrier (APC) kilioneka kikiwa mwendo huku kikiperusha bendera mbili nyuma. Moja ikiwa ni ya Urusi na nyingine ikiwa ni ya hasimu na adui namba moja wa Urusi ambaye ni Marekani. Hili halikutazamiwa kuona kwamba linatokea kwa sasa lakini limetokea na kupokelewa na ukosoaji mkubwa kutoka Ukraine wakilaani tukio hilo. Hayo ni kwa mujibu wa Russia Today (RT).
Kifaru cha Marekani kikipeperusha bendera ya Urusi na Marekani baada ya kukamatwa na wanajeshi wa Urusi. Vidio ni kwa hisani ya Russia Today (RT).Wakati hayo yanajiri huko Ukrane, Rais wa nchi hiyo anafanya mazungumzo na mjumbe wa Trump KeithKellog huko Washington kwa mujibu wa ripoti mbalimbali kutoka vyanzo vya habari vya Ukraine. Na baada ya kuhitimisha mazungumzo yao Rais Zelenisky amesema kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) kua alikua na mazungumzo muhimu ambapo wamejadili hali ya mapambano (vita) na ushirikiano thabiti wa nchi hizo mbili na kuongeza kua ili kumaliza vita wanahitaji nguvu ya pamoja kuilazimisha Urusi kufanya makubaliano ya amani na kwamba Trump ana nguvu hiyo.
Comments
Post a Comment