IRAN NA ULAYA ZAINGIA KATIKA MZOZO MPYA HUKU MAREKANI IKITAJWA PIA.
![]() |
| Kiongozi mkuu wa taifa la Iran Ayatollah Ali Khamenei. Picha na New York Times |
Ni takribani miezi miwili imepita tangu kumalizika kwa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran. Katika vita hivyo ilishuhudiwa pia Marekani akiingilia kati kwa kuvishambulia vinu muhimu ya Nyuklia vya Iran ikiwemk kile kinu kikubwa zaidi cha Fordow, Nantaz na Isfahan tarehe Juni 22, 2025 ambapo mashambulizi hayo yaliibua hisia mseto kutoka katika Jumuiya ya kimataifa. Kufuatia mashambulizi hayo Trump alisema wameharibu kabisa uwezo wa Nyuklia wa Iran na kwamba huo ulikua ni ushindi mkubwa sana kwa usalama wa dunia. Lakini kauli ya Trump inapingana na ripoti ya shirika la ujasusi wa kiusalama lililo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) yaani Defense Intelligence Agency(DIA). Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambayo kulingana na unyeti wa taarifa hawakutaka kutajwa walisema mashambulizi katika vinu vya nyuklia huko Iran vilirudisha nyuma mpango wa Nyuklia wa Iran kwa miezi kadhaa tu nyuma. Wakiamini hakukua na uharibifu mkubwa sana kiasi cha kutisha. Japo hilo linapingwa na Trump na baadhi ya vyombo vya usalama wa taifa vya Marekani.
Tathmini hiyo ya DIA ilipingwa mno na Rais Donald Trump akikosoa vikali ripoti hiyo ya kijasusi lakini haijulikani ni taarifa zipi ambazo Rais Trump alizitumia kuthibitisha madai yake. Lakini ikiwa madai ya Trump yakiwa ni kweli kwanini kumekua na mvutano mpya ambapo wanaitaka Iran irudi tena katika meza ya mazungumzo ili kujadili mpango wake wa Nyuklia. Jambo hilo pia Iran imekua ikilipinga kwamba kwa mujibu wa Trump ni kua waliharibu vinu vyote vya Nyuklia sasa mazungumzo ya sasa yatakua kuhusu nini ikiwa hawana silaha za Nyuklia? Na kulingana na Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alisema mgogoro kati ya Tehran na Washington hauwezi kutatuliwa.
Nchi za tatu za Ulaya kwa maana ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani maarufu kama E3 zimeweka mbinyo mpya kwa Iran na wamekua matika mazungumzo ambayo hayajazaa matunda huko Geneva siku ya Jumanne Agosti 26, 2025. Wasiwasi ni mkubwa kwa nchi hizo kwani mkataba wa sasa na Iran ambao ulisainiwa mwaka 2015 unatamatika Oktoba 18, 2025. Na kuna shida mbili kubwa kwa sasa.
Mosi, Rais Trump anaweza kupunguza msukumo wa kufanya mazungumzo na Iran kwa sababu anaamini kua mashambulizi ya mabomu yalifanya uharibifu mkubwa lakini hilo haliungwi mkono sana na nchi za Ulaya japo pia hawafanyi ukosoaji wa wazi ila kuna namna bado Iran anamiliki uwezo flani mkubwa wa Nyuklia na maaarifa yao ya nyuklia huwezi kuharibu kabisa. Na kwamba wakati wa mashambulizi ya tarehe 22 Juni 2025 Iran ilikua imehamisha urani iriyorutubishwa mpka kukaribia kiwango cha kutengeneza silaha. Ikiwa hilo ni kweli je, waliweka wapi? Maana watakua wako hatua chache sana nyuma kabla ya kua na bomu la nyuklia.
Pili, mwezi Oktoba 2025 Urusi atachukua nafasi yake kama mwenyekiti wa balaza la usalama la Umoja wa Mataifa na hivyo jitihada za kuikaba Iran ambaye ni mshirika wa Urusi itakua ni ngumu sana. Kwa hio wanataka Iran kufanya makubaliano mapya kabla ya wakati huo. Lakini mambo wanayoyataka yanawezekanika? Kwa kauli ya kiongozi mkuu wa taifa hilo Khamenei ni kwamba mazungumzo na Marekani kuhusu Nyuklia ya Iran hayawezi kufanyika. Msimamo huu mkali unakwamisha jitihada za suluhu ya kidiplomasia. Ila je ni majigambo tu au Khamenei anamanisha kweli au?
NINI UMOJA WA E3 UNATAKA KUTOKA KWA IRAN?
Mosi wanataka Iran kurudi katika mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wake wa Nyuklia na waseme shehena kiasi gani wanamiliki na kwa madhumuni gani. Japo Iran inaendelea kusisitiza kua mpango wake wa nyuklia ni wa amani.
Pili, wanaitaka Iran kuweka wazi zilipo karibu kilogramu 400 za madini ya Urani iriyorutubishwa kufikia kiwango cha kutengeneza silaha za nyuklia ambacho hakifahamiki kiko wapi. Ikiwa wakiwa wameificha basi huenda ikatumika kuunda bomu la nyuklia mapema kuliko inavyoweza kufikiriwa.
Tatu, wanataka Iran iweze kurusu wataalam wa kimataifa kutoka shirika la Atomiki la umoja wa Mataifa (International Atomic Energy Agency) kuweza kukagua vinu na shughuli za nyuklia za Iran. Kumbuka Iran iliituhiku ripoti ya IAEI mwezi Juni ambayo ilisababisha Iran kuishambuliwa na Israel.
Mambo hayo matatu yanapingwa sana na Iran kwa kua yanakosa uhalali. Wakati hali hio ikiendelea tayari Iran amekua akifanya mazungumzo na China na Urusi ambao ndio wanunuaji wakubwa wa mafuta ya Iran kutafuta uungwaji mkono ili ikiwa vikwazo vipya dhidi ya Iran vitatekelezwa basi yaweze kubakia nguzo tegemezi ya kiuchumi kwa Iran.

Comments
Post a Comment