UEFA IMEFANYA MABADILIKO YA MUDA WA KUCHEZA SIKU YA FAINALI





Shirikisho la mpira barani Ulaya linalosimamia mashindano ya Ligi ya mabingwa Ulaya kwa maana ya UEFA wametangaza mabadilko katika muda wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu huu ya 2025/2026 ambayo itachezwa pale katika uwanja wa Puskas huko Budapest nchini Hungari. Mabadiliko haya ya muda yanafuatia tathmini ambayo UEFA wameifanya na kuamua kuweza kuwapa burudani mashabiki ambao hapo awali wamekua wakisumbuka kutokana na mechi baadhi kuchelewa kuisha hasa pale michezo hiyo inapoenda katika muda wa nyongeza na mikwaju ya penati. 

Kuanzia msimu wa 2025/2026 mchezo wa fainali utakua ukichezwa kuanzia saa 12:00 jioni badala ya 3:00 usiku kama iliyokua awali. Kulingana na Rais wa UEFA Alexander Ceferin amesema kwamba muda wa saa 3 usiku ni mzuri kwa michezo ya katikati ya wiki lakini kwa siku ya Jumamosi inakua ni changamoto kwa mashabiki ambao baadhi yao hulazimika kuondoka mapema uwanjani kurudi makwao na kushindwa kushudia sherehe za mwisho za timu inayoshinda taji.

Je, mabadiliko haya ya muda yanweza kua na athari chanya au hasi kwa upande wa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla? Au ni kwamba muda kwa sisi hukua na changamoto yoyote.? Unaweza kutuandikia maoni yako katika blog au kuacha comment kwenye mitandao yetu ya kijamii. 

Comments

Popular posts from this blog

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?