MAANDAMANO MAKUBWA HUKO ISRAEL KUMSHINIKIZA NETANYAHU KUMALIZA VITA


Mtu akionekana kuvuka barabara ambapo matairi yalichokwa moto siku ya maandamano Jumanne 26 Agosti 2025. Picha na Times of Israel/Idit Avishay/Pro Democracy Protest Movement 

Maandamano makubwa yamefanyika leo kote  nchini Israel ambapo waandamanaji wamezuia barabara zote muhimu katika jiji la Tel Aviv wakiwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kukomesha vita huko ukanda wa Gaza na kuweka kipaumbele kuachiwa kwa mateka wa Israel ambao bado wangali wanashikiliwa na wanamgambonwa Hamas huko Gaza. Maandamano hayo yamendaliwa na kuratibiwa na Hostages and Missing Families Forum. 

Waziri mkuu wa Israel anakaniliaa na shinikizo kubwa la umma kufuatia vita ambavyo ukomo wake bado haufahamiki huko Gaza. Hayo yanajiri huku pia kukiwa na msukumo wa jumuiya ya kimataifa wa kumtaka Netanyahu kuamaliza vita vya Gaza vilivyodumu kwa takribani miezi 22 hadi sasa. Jana serikali ya Israel ilikuri kufanya shambulizi katika hospitali ya Nasser huko Gaza ambapo pia waandishi wa habari watano na wahuduku wa afya wanne waliweza kuuwa na kuibua ukosoaji mkubwa wa kimataifa. 


Watu wanaishinikza serikali kufikia makubaliano na Hamas ili kuwaokoa mateka waliosalia. Picha na  Jack GUEZ / AFP

Kwa mujibu wa taaarifa zilizopo ni kwamba naadhi ya waandanaji ambao ndugu zao wamekua wakishikiriwa mateka tangu shambulizi la Oktoba 23, 2023, wamesema serikali ya Israel imekua ikipigana vita huko Gaza bila kua na lengo maalumu na kwamba waziri mkuu wa Israel anaogopa shinikizo la umma. Waratibu wa maandamano hayo pia wamemtaka Rais wa Marekani Donald Trump kuendelea kumshawishi Netanyahu kukubali pendekezo la kumaliza vita huko Gaza. Ijapo waziri mkuu huyo alisisitiza hapo jana kua adui wao ni Janas na watapambana naye hadi watakapo shinda. 

Ikiwa swala la amani linaweza kufikiwa au la ni jambo la kusubiri kwa maana pendekezo la amani ambalo Hamas walilipigia kura wiki iliyopita bado linajadiliwa katika ngazi mbalimbali kabla ya kutolewa kwa uamuzi wa mwisho. Hata hivyo kulingana na waziri wa wizara ya ulinzi ya Israel alidokeza kua pendekezo hilo linaweza kukubaliwa na kwamba kwa sasa liko katika mikono ya waziri mkuu. 

Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?