Monday, 20 November 2017
SAWA, HATIMAE MUGABE AKUBALI KUJIUZULU.
Kwa mujibu wa taarifa ya CNN imeripoti kua chanzo rasmi kinachofuatilia mazungumzo kati ya rais Mugabe na maafisa wa jeshi kimedokeza kua rais Mugabe amekubali kujiuzulu kufuatia hatua ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo kumuweka kizuizini kwa siku kadhaa. Hatua hii inakuja kufuatia hatua yake ya jana jumapili ambapo kwa mara ya kwanza tangu awekwe kizuizini nyumbani kwake alilihutubia taifa kupitia shirika la utangazaji la nchi hio ZBC.
Sunday, 19 November 2017
MUGABE ATIMULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF
Chama tawala cha ZANU-PF cha nchini Zimbabwe kimeridhia kumuondoa Robert Mugabe kama mwenyekiti wake na kumteua aliyekua makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa kua mwenyekiti mpya wa chama hicho. Mnangagwa alifutwa kazi na rais Mugabe siku chache zilizopita na kutaka kumtangaza Grace Mugabe kua makamu wa rais na hatimaye aje kua mwenyekiti na baadae rais wa Zimbabwe kitu kilichoamsha hasira na sintofahamu miongoni mwa wazimbabwe wengi.
Hatua hio ilimlazimu generali wa jeshi la zimbabwe (ZDF) Gen Constantino Chiwenga kutangaza kuingilia kati mzozo huo siku ya jumatatu na siku ya jumatano vikosi vya jeshi kulazimika kuchukua udhibiti wa serikali kwa kumuweka kizuizini rais Mugabe na kutaka atangaze kuachia madaraka hatua iliyosimamiwa na kanisa katoliki lakini taarifa zilidai kua Mugabe alikataa kufanya hivyo na pia vilizingira kituo cha habari cha ZBC.
Hata hivyo leo chama hicho tawala kimeamua kumvua uongozi mwenyekiti wake Robert Mugabe 93, pamoja na mkewe Grace Mugabe ambaye ametimuliwa kabisa ndani ya ZANU-PF. Msafara wa magari ya rais ulionekana ukipita barabarani ukitokea kwenye nyumba la Mugabe japo haikuthibitika mara moja kama rais Mugabe alikuwapo ndani kwenye msafara huo.
UTUMWA BADO UNAITESA DUNIA YA TATU
Wakati dunia ikifurahia na kusherehekea mafanikio mengi na hatua kubwa iliyofikiwa na binadamu, hii sio habari na sio furaha ya kila mtu. Ni wakati ambao baadhi ya jamii zinataabika kwa mabalaa ya umaskini uliokithiri, njaa kali, majanga ya asili na vita vya wenyewe kwa yenyewe na kubwa zaidi ni SULUBU YA UTUMWA!
Thursday, 24 August 2017
DROO YA MAKUNDI YA UEFA 2017/2018
Droo ya kupanga makundi ya UEFA kwa msimu wa 2017/2018 imefanyika leo huko Monaco, Ufaransa.
Shirikisho la soka barani ulaya leo tarehe 24, August 2016 limetoa tuzo kwa wachezaji nyota waliong'ara kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya(UEFA Champions League) kwa msimu wa 2016/2017 pamoja na kutoa orodha ya makundi ya michuano hio mikubwa barani ulaya kwa msimu wa 2017/2018.
Nani kucheza na nani Ulaya? Droo ya Klabu Bingwa Ulaya 2017-18
Droo hii ilikua na timu 32 yametoka makundi manane.
Shirikisho la soka barani ulaya leo tarehe 24, August 2016 limetoa tuzo kwa wachezaji nyota waliong'ara kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya(UEFA Champions League) kwa msimu wa 2016/2017 pamoja na kutoa orodha ya makundi ya michuano hio mikubwa barani ulaya kwa msimu wa 2017/2018.
Nani kucheza na nani Ulaya? Droo ya Klabu Bingwa Ulaya 2017-18
Droo hii ilikua na timu 32 yametoka makundi manane.
Saturday, 19 August 2017
KANDE ZA MPAISHA MTU HUKO KENYA.
Martin Kamotho (Githeriman) kabla na baada ua kupata msaada.
Picha kwa hisani ya Google.
Maisha hayana maana moja na kila mtu atatoa maana ya maisha kwa vile ambavyo yeye anachukulia ni nini maisha yana maanisha kwake. Na kila siku hua tunasikia watu wakisema "Hakuna kukata tamaa" ni kweli lakini mwingine anajiuliza kwanini nisikate tamaa?? Kila mtu ana jibu lake sasa leo tumepata somo jingine zuri sana kutoka Kenya.
Sunday, 13 August 2017
VURUGU ZIMEZUKA KWENYE MAANDAMANO MAREKANI
Waandamanaji wakiwa katika moja ya viunga vya Charlottesville, Virginia.
Mamia ya wamarekani weupe (wazungu) na wale wanaowapinga walitarajia kufanya maandamano leo jumamosi kwa kile kilichofahamika kama "Unite the Right"(Ungana na mrengo wa kulia) huko Charlottesville, Virginia
Saturday, 15 July 2017
MATOKEO KIDATO CHA SITA 2017
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).
Friday, 9 June 2017
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2017
Serikali imetoa orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Kuangalia orodha hio bofya hapa;
1. http://www.tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/
2. http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/tangazo-1068-20170609-Uchaguzi-kujiunga-kidato-cha-5-vyuo-vya-ufundi-2017/ORODHA-YA-WANAhiFUNZI-WATAKAOPANGIWA-AWAMU-II.pdf
Saturday, 20 May 2017
WATU WALIOKATALIWA KUISHI NCHI KAVU.
Wabajui huishi na familia zao kwenye vibanda vyao vya miti vilivyojengwa baharini kwani wamezuiwa kuishi nchi kavu na pia pia wakikaa sana nchi kavu wanajihisi kuumwa.
Dunia ina mambo mengi sana, mengine yanastaajabisha, mengine kuudhi na mengine kufurahisha. Ila hili sijui linaleta picha gani.
Bahari ni makazi ya karibu nusu ya viumbe hai waishio duniani ila sisi binadamu sio mojawapo ya viumbe hivyo kwani hatuwezi kukaa ndani ya maji ya chumvi kwa muda mrefu, hatuwezi kuzama na kukaa kwenye kina cha bahari kwa muda mrefu lakini kinyume na haya yote kuna baadhi ya binadamu karibia maisha yao yote ni baharini! Wamejenga "vijumba/vibanda" vyao vya miti huko na asilimia zaidi ya 90 wanaishi huko na sio nchi kavu! Naam, ni watu jamii ya
Sunday, 14 May 2017
KOREA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA JIPYA.
![]() |
Uwezo wa makombora yanayomilikiwa na Korea kaskazini.
Korea kaskazini imerusha kombora jingine mapema leo jumapili ambalo liliruka karibu 700km, hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Korea kusini. Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tu tangu rais mpya wa Korea kusini kushika wadhifa wa urais hapo jumatano. Rais mpya wa Korea alisisitiza kua yuko tayari kufanya mazungumzo na utawala wa Pyongyang kama mazingira yataruhusu.
MTOTO WA OSAMA BIN LADEN AAPA KULIPA KISASI
Mmoja kati ya watoto wa aliyewahi kua kiongozi wa kundi la Al qaeda ameapa kulipa kisasi cha mauaji ya baba yake yaliyotekelezwa na kikosi cha makomando wa kimarekani mwaka 2013 nchini Afganistani.
Picha hii ilipigwa na kituo cha televisheni cha Al jazeera japo haifahamiki ilikua ni lini.
Mtoto wa Osama bin laden anasemekana kua anapanga kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi juu ya kifo cha baba yake kilichotokea May 2013. Mtoto huyo pia (Hamza) anajiandaa kua kiongozi mpya wa kundi la Al Qaeda.
Saturday, 6 May 2017
MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI. (2)
Muendelezo wa vitisho baina ya korea kaskazini na Marekani kwa mwezi wa nne 2017.
Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC)
Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC)
April
Korea kaskazini ilirusha kombora jingine kulenga bahari ya Japan na kitendo kilichozua hofu kubwa toka Japan.
Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.
Korea kaskazini ilirusha kombora jingine kulenga bahari ya Japan na kitendo kilichozua hofu kubwa toka Japan.
Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.
Tuesday, 2 May 2017
MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (1)
DUNIA YA VICHWA VIWILI VISIVYOTOSHANA.
Meli ya kubeba ndege na makombora ya Marekani ikiwa njiani kuelekea eneo la bahari la korea kufuatia mvutano mkali baina ya Korea na Marekani.
Kuna wasiwasi wa dunia kutumbukia kwenye vita mbaya ya nyuklia kutokana na vitisho baina ya Marekani na Korea kaskazini. Kumekuwepo na vita za maneno na vitisho baina ya Washington na Pyongyang watishiana kupigana baada ya kipindi kirefu cha bila maelewano baina yao.
Sunday, 23 April 2017
UHASAMA WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (2)
USAHAMA WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (2)
Baada ya kipindi cha mazungumzo kiasi baina ya korea na Marekani mwaka 2008 Korea Kaskazini ilishutumiwa kua imeanzisha tena shughuli zake za nyuklia kwenye kinu chake cha Yongbyon. Hii ilikuja baada ya Korea kaskazini kuiambia Marekani imeshindwa kutekeleza baadhi ya matakwa waliyokubaliana ikiwa n pamoja na kutolewa kwenye orodha ya nchi magaidi. Mwaka huo huo wa 2008 mwez october Korea na Marekani waliingia makubaliano kua itaondolewa kwenye nchi zinazofadhili ugaidi.
Tuesday, 18 April 2017
HISTORIA YA UHASAMA KATI YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI.
Rais wa marekani (kushoto) na rais wa korea kaskazini(kulia).
UJUE KWA UNDANI UHASAMA WA MAREKANI NA KOREA KASKAZINI.
Siku za hivi karibuni kumeibuka mvutano mkali na vitisho baina ya mataifa hasimu kihistoria moja kutoka rasi ya korea na jingine kutoka amerika ya kaskazini. Mvutano huu umeongeza hofu ya kutokea kwa vita ya tatu ya dunia na imechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kila mahali. Lakini wengi hatufahamu hasa kwanini mataifa haya yamekua hasimu kwa kipindi kirefu na labda ndio uhasama mkali zaidi duniani. Maelezo haya yatakusaidia kuelewa kwa undani uhasama huu.
Sunday, 5 February 2017
SHULE IMEFUNGA CCTV CAMERA KUDHIBITI NIDHAMU YA WANAFUNZI.
Tafakari haya, ndani ya shule ya upili, kuna kamera zilizotundikwa katika kila pembe ya shule ili kuboresha nidhamu. Mwanafunzi anapokiuka sheria na kanuni za shule basi hana lake kwani ushahidi utanaswa kwenye kamera. Ndivyo mambo yalivyo katika shule ya upili ya wavulana ya Karima katika eneo la Othaya. Isitoshe, kando na kamera hizo, kuna mashine zinazotambua alama za vidole za mwanafunzi na kutuma ujumbe mfupi kwa mzazi iwapo mwanafunzi huyo anaingia au kutoka shuleni.
Lakini jambo kubwa la kujiuliza ni je hii ni njia sahihi ya kudhibiti nidhamu ili kama inafaa basi shule nyingine pia ziige mfano huu kwenye maeneo yetu?
Unaweza kuandika maoni yako kwenye blog au kwenye tweeter na facebook.
Friday, 3 February 2017
MAREKANI YAIONYA IRAN KWA KUIWEKEA VIKWAZO VIPYA.
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora.
Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.
Tuesday, 31 January 2017
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016
Baraza la mitihani la taifa limetoa matokeo ya kidato cha nne 2016. Kuangalia matokeo bonyeza hapa>>>http://tanzania.go.tz/result_csee_2016/CSEE_2016/index.htm
Sunday, 8 January 2017
MBARONI KWA KUANZISHA BENKI BANDIA.
Mahakama mjini Nanjing, China, imewafunga jela wanaume wawili waliowatapeli wateja kupitia benki bandia, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Wanaume hao waliotambuliwa kwa majina Zeng na He, walipatikana na makosa ya kujipatia yuan 435m (£51m; $63m) kutoka kwa wateja 400.
Subscribe to:
Posts (Atom)