Posts

Showing posts from 2025

WAAFRIKA WAUNGANA NA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA NCHI GHANA. UMAJUMUI WA AFRIKA UNAPATA NGUVU MPYA?

Image
Moja kati ya bango likiwa na ujumbe kua "HATUDAIWI, HATUTOLIPA"  Bara la Afrika ni moja ila ikiwa Waafrika ni wamoja ni swali pana sana na inaweza kua vigumu  kufikia hitimisho la pamoja. Wakati wa Karne ya dhahabu kwa nchi za kiafrika naweza kusema ilikua ni kipindi cha miaka ya 1960s. Hapa tulishuhudia miito mbalimbali ya Waafrika kuungana na kua wamoja au kitu kimoja na  mwaka 1963 viongozi wa nchi huru za Afrika walifanikiwa kuunda Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) lakini baadae mwaka 2002 Umoja wa Afrika (AU) ulianza rasmi baada ya Sirte declaration kule Linya mwaka 1999.  Lengo lilikua ni kuwaleta Waafrika pamoja na kupigania haki na usawa katika nyanja za kimataifa. Kupitia mikutano na makongamano mbalimbali imekua dhahiri kua Afrika ina hitaji ukombozi mpya kwani sasa inaelekea kulekule tuliko toka kwenye miaka ya 1980s ambapo madeni ya nje yalizidhoofisha nchi za kiafrika na kufikia hatua ya kufilisika ndipo taasisi za kifedha za kimataifa na nchi wakopesha...

TRUMP NA MAREKANI VS NICOLAS MADURO NA VENEZUELA, JE, VITA IKO KARIBU?

Image
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro. Picha na Reuters  Kumekuwapo na sintofahamu kubwa juu ya kile kinachoendelea kati ya Marekani na Venezuela kufuatia matendo hatarishi ya pande zote mbili. Awali Marekani ilitangaza dau nono la dola milioni 50 ambazo ni sawa na karibu sawa na shilingi 12, 529, 390, 000/= kama zawadi kwa mtu yeyote anatakaye wezesha kupatikana na kukamatwa kwa Rais wa Venezuela ambae anatuhumiwa kwa ulanguzi wa madawa ya kuelevya. Lakini hilo limechukua sura mpya baada ya Marekani kutuma meli za kivita pamoja na nyambizi karibu na Venezuela kitu ambacho kimemlazimu Rais Maduro kuanza kukusanya wanajeshi wakijiandaa kwa makabiliano ikiwa Marekani itawavamia. 

UEFA IMEFANYA MABADILIKO YA MUDA WA KUCHEZA SIKU YA FAINALI

Image
Shirikisho la mpira barani Ulaya linalosimamia mashindano ya Ligi ya mabingwa Ulaya kwa maana ya UEFA wametangaza mabadilko katika muda wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu huu ya 2025/2026 ambayo itachezwa pale katika uwanja wa Puskas huko Budapest nchini Hungari. Mabadiliko haya ya muda yanafuatia tathmini ambayo UEFA wameifanya na kuamua kuweza kuwapa burudani mashabiki ambao hapo awali wamekua wakisumbuka kutokana na mechi baadhi kuchelewa kuisha hasa pale michezo hiyo inapoenda katika muda wa nyongeza na mikwaju ya penati. 

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

Image
Picha za smartphone mbalimbali Miongoni mwa masoko magumu kwa sasa ni pamoja na soko la simu janja au rununu (smartphones) ambapo kila kampuni ya utengenezaji wa siku inajitajidi kutoa simu zenye ubora wa hali ya juu. Lakini sio rahisi kama unavofikiria ikiwa utaulizwa ipi ni simu bora kwa sasa sokoni. Kwa sababu simu moja kutoka kampuni flani inaweza kua bora kwenye eneo moja au mawili hivi lakini ikashindwa kua bora katika maeneo mengine. Lakini kati ya vitu virahisi na hua ni kigezo cha watu kununua simu hua ni kamera. Hii hapa ni orodha ya simu 10 zenye kamera bora sana mpaka sasa. 

IRAN NA ULAYA ZAINGIA KATIKA MZOZO MPYA HUKU MAREKANI IKITAJWA PIA.

Image
Kiongozi mkuu wa taifa la Iran Ayatollah Ali Khamenei. Picha na New York Times Ni takribani miezi miwili imepita tangu kumalizika kwa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran. Katika vita hivyo ilishuhudiwa pia Marekani akiingilia kati kwa kuvishambulia vinu muhimu ya Nyuklia vya Iran ikiwemk kile kinu kikubwa zaidi cha Fordow, Nantaz na Isfahan tarehe Juni 22, 2025 ambapo mashambulizi hayo yaliibua hisia mseto kutoka katika Jumuiya ya kimataifa. Kufuatia mashambulizi hayo Trump alisema wameharibu kabisa uwezo wa Nyuklia wa Iran na kwamba huo ulikua ni ushindi mkubwa sana kwa usalama wa dunia. Lakini kauli ya Trump inapingana na ripoti ya shirika la ujasusi wa kiusalama lililo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) yaani Defense Intelligence Agency(DIA). Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambayo kulingana na unyeti wa taarifa hawakutaka kutajwa walisema mashambulizi katika vinu vya nyuklia huko Iran vilirudisha nyuma mpango wa Nyuklia wa Iran kwa miezi kadhaa tu nyuma. Wakiamini ...

YOUTUBE ILITUMIA AKILI UNDE (AI) KUHARIRI VIDEO ZA WATU KWA SIRI

Image
Picha na AFP/Getty Images  Akili unde (AI) kama inavyofahamika imekua ni mapinduzi makubwa katika sayansi na teknolojia na kwa sasa ni ngumu kuwaza dunia bila Akili unde. AI sasa hivi inatumika katika tafiti za kisayansi, elimu, afya, viwandani, mtandaoni na karibu kila nyanja ya maisha ya binadamu kuna matumizi ya Akili Unde (AI) kwa kiasi fflani. Licha ya kua na fursa nyingi bado AI imeacha mwanya wa changamoto hasa zile zinazohusu hatimiliki na uhalisia wa mawazo au ubunifu kwani kam kitu au wazo litku limesanifiwa na akili unde ni ngumu kudai kwamba ni wazo lako licha ya kwamba uliielekeza namna ya kufanya. Katika changamoto mojawaponkubwa sasa inaikumba kampuni ya Google kupitia bidhaa yake ya YouTube.

MAANDAMANO MAKUBWA HUKO ISRAEL KUMSHINIKIZA NETANYAHU KUMALIZA VITA

Image
Mtu akionekana kuvuka barabara ambapo matairi yalichokwa moto siku ya maandamano Jumanne 26 Agosti 2025. Picha na Times of Israel/Idit Avishay/Pro Democracy Protest Movement  Maandamano makubwa yamefanyika leo kote  nchini Israel ambapo waandamanaji wamezuia barabara zote muhimu katika jiji la Tel Aviv wakiwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kukomesha vita huko ukanda wa Gaza na kuweka kipaumbele kuachiwa kwa mateka wa Israel ambao bado wangali wanashikiliwa na wanamgambonwa Hamas huko Gaza. Maandamano hayo yamendaliwa na kuratibiwa na Hostages and Missing Families Forum.  Waziri mkuu wa Israel anakaniliaa na shinikizo kubwa la umma kufuatia vita ambavyo ukomo wake bado haufahamiki huko Gaza. Hayo yanajiri huku pia kukiwa na msukumo wa jumuiya ya kimataifa wa kumtaka Netanyahu kuamaliza vita vya Gaza vilivyodumu kwa takribani miezi 22 hadi sasa. Jana serikali ya Israel ilikuri kufanya shambulizi katika hospitali ya Nasser huko Gaza ambap...

TAJIRI WA DUNIA VITANI TENA JUU YA AI. MUSK AZISHTAKI APPLE NA OPEN AI

Image
Picha kwa hisani ya mtandao  Mwishoni mwa wiki iliyopita niliandika kuhusu Open AI kumkaanga Elon Musk na Mark Zuckerberg juu ya kutaka kuiua kampuni chipukizi ya Open AI ambayo inamiliki programu maarufu ya ChatGPT. Na jana Jumatatu tunashuhudia kesi nyingine inayovutia miongoni mwa wataalamu wa kesi za teknolojia kwani tajiri namba moja duniani, Elon Musk amezishtaki kampuni za Apple na Open AI kwa kujimilikisha soko la Akili Unde (AI). Kwa mujibu wa Elon Musk Apple na Open AI ambao wanamiliki 65% ya soko la simu Marekani na 85% ya Chat bot huko Marekani mtawalia wamejimilikisha soko la huduma na kufanya iwe vigumu kwa kampuni nyingine kama vile xAI ambayo inaimiliki Grok kushindwa kushindana katika hali ya usawa. 

DONALD TRUMP KUKUTANA NA KIM JONG UN TENA?

Image
           Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini na Donald Trump wa   Marekani               walipokutana kwenye mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini 2019. Picha na Reuters Korea Kaskazini na Korea Kusini hazijawahi kuaa na mahusiano mazuri kwa historia ya hivi karibu na hilo ni sawa sawa kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Narekani. Korea Kaskazini ni miongoni mwa chache duniani ambazo zimetengwa zaidi na zenyewe zinajitenga na dunia nyingine. Ni nadra kuona mikutano ya kidiplomasia kati ya viongozi wakuu wa Kore Kaskazini na mataifa mengine isipokua China na Urusi. Lakini katika utawala wa Donald Trump alijaribu kukutanaa na Kim Jong Un karibu mara tatu huko Hanoi Vietnam, Singapore na katika mpaka wa Korea Kaskazini na Korea kusini kati ya 2018-2019. Ijapo hakuna kilichotokea baada ya mikutano hii. 

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

Image
Picha ya pamoja ya viongozi wa Ulaya na Rais wa Marekani ikulu ya Marekani tarehe 18 Agosti 2025. Picha na AFP  February 2022 Urusi iliivamia Ukraine kijeshi katika kile ambacho Moscow walikiita kama Operesheni Maalumu  (Special Operation). Na tangu wakati huo vita hio imeendelea na dalili za kukoma kwake bado zinaonekana ziko mbali kulingana na matokeo ya jitihada mbalimbali za kukomesha vita hivyo. Lakini kwa sasa vita vimeingia katika hatua muhimu na huenda ni hatua mbaya sana ambayo kosa kidogo la kimahesabu limaweza kuigharimu dunia kama ilivyokua Julai 1918 au Septemba 1939 ambapo vita vya kwanza na pili vilianza mtawalia. Kwa sasa vita vya Ukraine vina sura ya tofauti ambayo inahatarisha usalama wa dunia. Na haya ndio mambo ya hatari zaidi ambayo yanaweza kushindwa kuzuilika na kuleta vita ya tatu ya dunia.

VITA YA WAJUMBE VS KAMATI KUU YA CCM MWAGA MBOGA, NIMWAGE UGALI. MBUNGE WAKO ULIYEMTARAJIA YUKO SALAMA?

Image
Hatimae mchakato wa kuchuja majina kwa wagombea nafasi ya wagombea katika ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefikia tamati baada ya kamati kuu ya CCM hapo jana kuweza kupitisha majina ya wagombea wake katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyanyika mwezi Oktoba mwaka 2025. Katika mchujo huo kumeshuhudiwa mapinduzi baada ya majina ambayo wajumbe waliyakataa na katika ngazi ya taifa kamati kuu ya CCM yaani (NEC) imewarudisha tena kwa wananchi.  Bofya kwenye maandishi ya bluu (PDF) kusoma zaidi majina ya walioteuliwa kugombea 2025.  Majina ya waliopitishwa na NEC ya CCM kugombea ubunge 2025 Je mbunge wako uliyemtarajia "kaliwa kichwa" na kamati au wajumbe sasa ndiyo wameliwa kichwa? Tungefurahi kupata maoni yako. 

OPEN AI YAMKAANGA ELON MUSK NA MARK ZUCKERBERG HUKO MAHAKAMANI

Image
Sam Altiman muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Open AI. Picha na AFP na Getty Images  Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali nchini Marekani zinaonesha kua kampuni ya Open AI ambayo inamilki ChatGPT imetoa maelezo mahakamani kua tajiri namba moja duniani Elon Musk alijaribu kumshawishi hasimu wake kibiashara Mark Zuckerberg ambae ni mmiliki wa kampuni kubwa ya Meta (Facebook, Instagram, WhatsApp na Thread) ili wachanhiane au waingie ubia katika uwekezaji wa kuinunua Open AI ambapo Elon Musk aliweka dau la dola za kimarekani bilioni 97.4, hata hivyo kulinga na Open AI Zuckerberg hakua ameafiki hilo. 

KAMPUNI YA APPLE IMEISHIWA 'PAWA'. YAOMBA MSAADA KUTOKA GOOGLE

Image
  Picha kwa hisani ya mtandao/ Shutterstock   Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani, Apple Inc ambayo ni kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kielekroniki kama vile simu za iPhone na  Laptop za MacBook wako katika mazungumzo na kampuni kubwa pia ya teknolojia ya Alphabet Inc ambao ndio wamiliki wa Google kuhusu uwezekano wa kampuni ya Google kupewa kandarasi ya kuunda mfumo wa akili unde (AI) wa Apple ambao utakaotumika kuendesha Program ya sauti ya Apple maarufu kama Siri ambayo kwa muda mrefu Apple wamekua wakijaribu kuiboresha lakini hakuna mafanikio makubwa kutokana na vikwazo vya kihandisi katika mfumo huo. Apple yuko nyuma ya Google na Samsung ambao wana programu bora kwa sasa. 

MAJARIBIO YA JESHI LA MAREKANI YAMEENDA NDIVYO SIVYO. HII NI MBAYA SANA.

Image
MAJARIBIO YA JESHI LA WANAMAJI WA MAREKANI LIMEENDA OVYO VIBAYA MNO. SIO DALILI NJEMA. Picha na Petty Officer 2nd Class Clayton/ Us military   Wanasema 'siku njema huonekana  tangu asubuhi 'lakini hii sio kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani. Ikiwa ni miongoni mwa majeshi yenye nguvu zaidi duniani, mara zote hua liko mbele ya muda lakini kwa hiki kilichotokea hivi karibuni kinaacha maswali mengi miongoni mwa wataalam wa kijeshi.  Mwezi uliopita jeshi hilo lilikua likifanya majaribio ya boti zinazojiendesha zenyewe ambapo lengo kuu lilikua ni kua na kweza kua na uwezo wa kulidhibiti jeshi la wanamaji wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limeshuhudia maendeleo makubwa na ya haraka ya kimuundo, silaha na teknolojia. Sasa wakati wa majaribio hyo huko Pwani ya California kulitokea matukio yaliyotilia mashaka uwezo wa Jeshi la Marekani kumudu vita vya kisasa ambavyo vinahitaji teknolojia za kisasa zaidi na hilo tayari limegahrimu kazi za wa...

HATARI YA "AI" YA ELON MUSK: IMETOA SIRI JINSI YA KUMUUA BOSS WAKE ELON MUSK

Image
Picha kwa hisani ya mtandao/ Nacional.hr Kitu kikubwa kinachozungumzwa kwa sasa katika Ulimwengu wa teknolojia ni Akili unde au Akili mnemba maarufu kama Artificial Intelligence (AI). Makampuni makubwa kama Alphabet Inc. (Google) ,wana AI yao ambaayo ni Gemin AI, Microsoft wana Copilot, Open AI wana ChatGPT, xAI wana Grok, Meta wana Meta AI na pia kuna Deep Seek kutoka China. Kwa sasa biashara kubwa ni AI. Hakuna kampuni imekua ikitaka kua nyuma katika hili. Lakini kuna jambo moja kubwa la kitisha ambalo bado watumiaji hatuweza kuwekwa wazi juu ya dhamira halisi ya hizi akili unde na wengi wanatumia kwasabau zipo bila tahadhari. Lakini hivi majuzi kumeshuhudiwa mambo ya hatari ambayo Akili Unde imeweza kujaribu kufanya. 

BAADA YA MIAKA 113 KANISA LAHAMISHWA BILA KUVUNJWA.

Image
Kanisa la Lutheran la Kiruna huko Sweeden likiwa tayari kusafirishwa. Picha kwa hisani ya Forbes Katika hali ambayo sio ya kawaida kanisa moja la kihistoria huko nchini Sweeden limehamishwa kutoka sehemu mabo lilijengwa na kupelekwa sehemu nyingine baada ya miaka 113 la kuwepo katika eneo ambapo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1912. Kuhamishwa kwa kanisa hilo la Lutheran ni kutokana na kuwepo kwa uchimbaji wa madini ya chuma chini ya kanisa hilo na maeneo mengine ya jirani. Mpango wa kuhamisha kanisa hilo bila kubomoa umekua ukiendelea kwa takribani mwaka mmoja ambapo wataalam wamekiri kwamba haikua kazi rahisi. 

WANAJESHI WA URUSI WAPEPERUSHA BENDERA YA MAREKANI KWENYE MSTARI WA MAPAMBANO HUKO UKRAINE

Dunia inastaajabisha sana na wakati flani matukio kadhaa yanaweza kuonekana kama mchezo wa kuigiza au mzaha lakini baadae hugeuka kua ni maisha halisi ya baadhi watu. Katika kisa kimoja cha kushangaza sana imetokea huko katika mstari wa mbele wa mapambano kati ya majeshi ya Ukraine na majeshi ya Urusi ambapo kifaru cha Marekani Armoured Personnel Carrier (APC)  kilioneka kikiwa mwendo huku kikiperusha bendera mbili nyuma. Moja ikiwa ni ya Urusi na nyingine ikiwa ni ya hasimu na adui namba moja wa Urusi ambaye ni Marekani. Hili halikutazamiwa kuona kwamba linatokea kwa sasa lakini limetokea na kupokelewa na ukosoaji mkubwa kutoka Ukraine wakilaani tukio hilo. Hayo ni kwa mujibu wa Russia Today (RT).

UMOJA WA ULAYA, UINGEREZA, NATO, TRUMP NA ZELENISKY WANAMKABIA JUU PUTIN, WATAWEZA?

Image
Kutoka kushoto ni Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Layen, waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Finland Alexander Stubb, Rais wa Ukraine Volodymr Zelenisky, Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, waziri mkuu wa Italia Giorgina Meloni, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na katibu mkuu wa NATO Mark Rutte .  Huenda siku ya Jumatatu 18, 2025 ikawa miongoni mwa siku kubwa kabisa katika siasa za kimataifa na diplomasia. Misukosuko ya Ulaya inawaleta viongozi wa nchi kubwa za Ulaya pamoja na Ukraine nchini Marekani na wote wakisubiri kwa hamu kuweza kusikia kile ambacho Rais wa Marekani Donald Trump alikua akitazamia kuamua juu ya hatma ya vita vya Ukraine na zaidi ya yote juu ya hatma ya Ulaya na NATO. Mgogoro wa Ukraine ni mgogoro mbaya zaidi kwa Ulaya tangu kuisha kwa vita baridi mnano 1991. Wangeliweza kukaa na kusubiri Volodymr Zelenisky na Trump wajadiliane na wapewe mrejesho lakini kamwe hilo halikuonekana kutokea kwani wote wal...

DUNIA INAHAMIA WASHINGTON KWA MUDA: WASHINGTON NI YA MOTO

Image
DUNIA INAHAMIA WASHINGTON KWA MUDA: WASHINGTON NI YA MOTO Rais wa Ukraine kushoto akifurahia na mwenyeji wake Rais Donald Trump wa Marekani, ikulu ya White House Agosti 18, 2025. Picha na Reuters Leo jijini Washington inatazamiwa kua ni moja kati ya nyakati ngumu na muhimu zaidi tangu vita vya Pili vya dunia vilivyomalizika mwaka 1945. Wakati kulishuhudiwa nyakati ambapo viongozi wengi wa dunia wapishana katika makao makuu ya nchi kama kubwa au miji iliyokua na ushawishi kama vile Potsdam huko Ujerumani na Yalta huko Crimea nchini Urusi.  Baadae Washington ikawa kitovu cha mikutano mikubwa ya kuamua hatma ya siasa na maendeleo ya dunia kwa kua miji ya Ulaya kama vile Berlin, Brussels, Vienna na London ilikua imepoteza ushawishi wake. Na Washington imebakia kama kielelezo cha Ushawishi duniani ambapo viongozi mbalimbali hukutana. 

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

Image
AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? HATIMAYE AFRIKA IMEANZA KUZINDUKA. Ramani ya dunia  Tulipokua shuleni tulijifunza mengi juu ya Afrika lakini mengi ilikua ni upotoshaji wa kukusudia au kutokukusudia. Hilo linajidhihirisha pale unapotazama ramani ya dunia. Utaambiwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani nyuma ya Asia lakini ukitazama ramani utagundua Amerika ya Kaskazini inaonekana kuwa ni kubwa kuliko Afrika. Lakini je Afrika ina ukubwa gani? Na kwanini sasa Umoja wa Afrika unahitaji taasisi kuu ulimwenguni kote kutumia ramani mpya ya Afrika kulikoni?  Tunarejea takribani miaka 456 hivi nyuma kuanzia sasa. Tunakutana na mwaka 1569, na hapo tunakuja kukutana na mtu mmoja aliyepata kua ni mwanajiografia na mchora ramani kutoka Flanders (Kijiografia eneo hili liko Ubelgiji na kijamii na kiutamaduni limekaliwa na watu asili ya Wadachi). Mtu huyu alitwa Gerardus Mercator ambaye ndiye aliyechora ramani hii ya dunia ambayo katika karne ya 18 ilirasmishwa kutumika katika maswala ya usa...

TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?

Image
TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?   Rais wa Marekani Donald Trump akiongea jambo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin baada ya mkutano wao huko Alaska 15 Agosti 2025/ picha kwa hisani ya Ikulu ya Marekani   Rais wa Marekani Donald T rump na Rais wa Urusi Vladimir Putin ni miongoni mwa majina makubwa katika medani ya siasa za kimataifa kutokana na hulka yao na namna wanavyochukua maamuzi magumu katika nyakati ngumu. Na hivyo kufanya dunia kua na viongozi shupavu kama wanne hivi kwa maana ya nyongeza ya Xi Jin Ping wa China pamoja na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini. Ila kwa sasa ni Trump dhidi ya Putin wakikaa wawili nani mbabe wa mwenzake?