Binadamu tunaishi kwa kubadilika sana kulingana na mazingira. Mgombea wa uraisi nchini marekani alishawahi kumsifu hasimu wake wa sasa katika kinyang'anyiro cha kiti cha uraisi kupitia chama cha Democrat, Hillary Clinton.
Jarida la Wall street journal limeandika kua mwaka 2008 Donald Trump alisema Clinton "anaweza kua raisi mzuri". Inasemekana maneno hayo aliyatoa kwenye kipande cha maneno kutoka kwenye kipindi cha radio kilichopewa jina la "Trumped" ambacho kilikua kinaruka hewani kuanzia mwaka 2004-2008. Hata hivyo maneno haya ya kumsifu Clinton yalikua yamerekodiwa tu hayakua yamerushwa hewani.
No comments:
Post a Comment