Rio Ferdinand anaitamani kazi ya kukukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England maarufu kama "Simba watatu".
Mlinzi wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand anaamini kukosekana kwa mfumo imara na wa kueleweka wa timu ya taifa ya England ndio sababu inayopelekea timu hiyo kufanya vibaya kwenye mashindano makubwa na angelipenda kuifundisha timu hiyo. Ferdinand alikiri hayo kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson aliyekua akikinoa kikosi hicho hadi pale walitolewa kwenye michuano ya Euro 2016.
Sam Allardyce maarufu kama "Big Sam" ndiye kocha anaetajwa zaidi kumrithi Hodgson huku pia ripoti nyingne zikimhusisha kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann.
Lakini Rio ambaye ameshinda michezo 81 akiwa na timu ya taifa ya England alisema kwenye mahojiano na Copa 90 kua angelipenda kuifundisha timu ya taifa ya England "Three Lions".
"Unapokua hujui kikosi chako cha kwanza unapokwenda kwenye mashindano, na hujui mfumo wako mzuri, hapo kuna tatizo," Alisema.
Ferdinand pia alisema ili timu icheze vizuri na kila mchezaji kuonesha uwezo wako ni lazima misingi ijengwe kuanzia ngazi za chini kabisa, waelewe muundo na waelewe nini unataka timu ifanye. Alipoulizwa iwapo angependa kuchukua nafasi ya ukocha wa England alijibu: "Siku zote".
No comments:
Post a Comment